Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema nyasi za Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kupandwa upya.
Makonda amesema hayo leo wakati akizungumza na viongozi wa vyama na mashirikisho mbalimbali ya michezo nchini.
Amesema watapanda nyasi ili kufikia viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Waziri huyo amesema pia Serikali itabadilisha mkandarasi kwa ajili ya kufunga viti vipya katika uwanja huo.
Makonda pia amewataka viongozi wa michezo kufanya kazi kwa weledi ili kusapoti mchango mkubwa unaotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Pia soma: Serikali kuufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa kupisha ukarabati kuelekea AFCON 2027