Makonda: Nisemeni, mkichoka mtanyamaza

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.

Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.

Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.

Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.

Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.

Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.

“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.

Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana wachapakazi.

“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,” amesema Makonda.

Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.

Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya mazoezi.

Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Chanzo: Habari leo
 
Nchi zilizoendelea hawaangalii cheti kipoje bali wanaangalia uwezo wa mtu wa kufanya kazi lakini sisi tunaoangalia uzuri wa cheti wakati huyo mtu hana uwezo wa kufanya kazi husika ndio umetupelekea tuwepo hapa tulipo. Piga kazi Makonda achana na kelele za mitandaoni.
 
Kusoma nisome mimi
Homework nifanye mimi
Mtihani nifanye mimi
Vyeti uchukue wewe
Majangaa!
Mbona Majangaa!

Uongozi ni uaminifu wa dhamana, kama uaminifu wako unatiliwa shaka una option mbili

1. Kudhihirisha kuwa unapaswa kuaminiwa, kwa kujisafisha kwa ushahidi dhidi ya tuhuma unazopewa

2. Kujiuzulu ili kulinda imani ya umma kwa serikali yao!!
 
Watu wengi ktk mitandao ya jamii wamepata hamasa kubwa kutaka kujua ukweli wa Paul Makonda au kwa jina la hivi karibuni, Daudi Al Maarifu Bashite and family.

Mimi hoja yangu ya msingi, iko kati kwa Kati, ningemshauri Mkuu wetu wa Mkoa ajihakiki
Kitu kimoja na mapendekezo haya, binafsi na wengi humu ndani, ninahisi wataweza kuniafiki na kuunganisha Nguvu, tukaipeleka hii proposal ya kuondoa ukasi unaomkwaza Mkuu wa Mkoa na kuweza kumsaidia Rais aweze kufanya maamuzi ya busara, kwa mtendaji wake Mkubwa inavyodaiwa na upande wa utetezi wa Makonda, na kila mtu anakua mshindi, makonda anashinda, nchi inashinda, na watu wanapata ushindi.

Sasa swala la msingi kabla ya kutoa hio proposal naomba niwahikishie wanabodi, wazingatie haki ya uhuru wa maoni yetu, hata kama yako ktk misingi ya uchachu wa kile ambacho hatuna mapenzi nacho kwa upeo wa fikra zetu.

After all jamii forum motto " we dare to talk"

Ushauri wangu ni kama ifuatavyo,

Kama tunavyofahamu sehemu kubwa ya elimu ya juu ya wasifu wa Makonda, ameweza kufikia ngazi ya cheti na diploma ktk chuo cha uvuvi Bagamoyo, na ukiangalia tuna tatizo kubwa la wavuvi wetu hapa Tanzania kukosa taaluma ya uvuvi na hatma yake umaskini uliobobea, na hili tunaliona wazi ktk vyombo vyao wanavyotumia wavuvi wetu kando ya ziwa victoria, magogoni dar es salaam, na sehemu nyengine za kando ya bahari na maziwa, ukizingatia utajiri wa bahari tunao na tumezungukwa na maziwa makubwa africa na hata ulimwenguni.

Na kwa bahati, nzuri hata Muheshimiwa Rais alijihusisha na kesi moja ya kukamata wavuvi na wataalam wa uvuvi wa standard juu Tanzania toka nje ya nchi wa bara la Asia, na kutuona sisi rasimali yetu ya samaki ni kubwa lkn bado tunavua na vidau na mashua za upepo, yaani talent and resources wasted.

Kwa bahati mbaya, Yale masamaki tuliyataifisha na kuyala kama vitoweo na ule mzinga wa Meli ya uvuvi uliishia pale magogoni na kuingia kutu na hatma yake ukaozea pale pale, na hii ilikua big mistake kwa upande wa Muheshimiwa alipokua waziri kwa kipindi kile, anyway hatma yake wale vijana wakafungwa na sisi inasemekana tukaambulia fine kubwa toka mahakama za nje kufidia maamuzi yaliyochukuliwa kwa wakati ule lkn tulibahatika na utowezi wenye neema na baraka, all isn't lost.

Sasa Nini kilitakiwa kifanyike, tujifunze na makosa tuliyofanya, after all, makosa ni sehemu ya mafunzo.

Moja tulitakiwa tusiwafunge wale vijana wala kuitelekeza ile meli, Bali tulitakiwa tuwaamuru wawafundishe kama sehemu ya uhukumu, vijana wetu wa magogoni ustad wa uvuvi kama sehemu ya adhabu zao, na meli ile itumike hapa Tanzania kwa kipindi cha hukumu yao wakati wakitoa mafunzo yao, gharama yetu diesel and service ndogo ndogo.

Pili kijana wetu mpendwa Paul Makonda na ujuzi wake wa kisiasa angeteuliwa kuwa captain na hatma yake, hivi sasa tungekua tumepata kufanya history kubwa ya Kuwa na mtaalam wa mambo ya uvuvi kwa meli kama ya bakhresa, au ilikua ndogo kidogo?

Sasa nini ushauri wangu kuhusiana na hizi shutma kubwa zinazomkabili na kuweza kumsamehe Paul Makonda ktk makosa yake, only if proven kama ameazima vyeti vya watu hatimae kujiunga na chuo cha uvuvi hatma yake kuwa mvuvi stadi ktk ngazi ya Diploma.

Muheshimiwa Rais atoke nae ikulu hadharani na waandishi habari wawepo, aingie kwenye dau moja pale ferry avuke hadi kigamboni na arudi na changu wawili na pono wa tano au samaki wa aina yoyote, tusiwe wabaya kiasi hicho, pono kupatikana msimu huu wa mvua ni tabu kidogo, alimradi avue samaki saba, Saba kwa nini that's another topic of discussion.

Akifanya hivyo taifa zima litamsamehe, na atakua ameprove one thing, yeye ni mvuvi stadi.

Pili, Muheshimiwa Rais ateue rasmi wizara maalum inayoshughulikia uvuvi, na Muheshimiwa Paul Makonda awe ktk wizara hio na apatiwe mandate ya kusaidia vijana wetu kando ya ziwa, ktk kozi za muda mfupi yaani mpaka miezi sita, jinsi gani ya kuvua samaki, kuwahifadhi na hatma yake kupata soko la nje, na kutuwezesha nchi yetu kupata fedha za kigeni, na hilo litatupa fursa ya kuwawezesha vijana wetu walioamua kujishghulisha na shughuli za uvuvi kutoka kimaisha,

You never know, uvuvi wetu utatuweka on the map, na kuwezesha wavuvi wetu na wao waanze kutanua misuli yao na boti zao za uvuvi kama za bakhresa waweze kufika hadi bara la Asia, kama ile boti iliyokufa magogoni, wakitushitaki na sisi tutalipwa mafidia kama wao.

Na hapo kila mtu, will have a new hero in town. Na vijana wetu wengi watatoka kimaisha, and our hero Paul Makonda will be a talk of the international media. He made it to the top!
 
Back
Top Bottom