Makonda; Ni nani atakayewahoji wahojaji?,Na nani atakayewataja watajaji?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
Ni nani atakayewahoji wahojaji?
Na nani atakayewataja watajaji?
Ukiwa mtaalamu wa saikolojia unaweza kuona namna vita ya dawa ya kulevya iliyoanzishwa na RC Makonda inavyokwenda kushindwa vibaya. Vita hii haikupaswa kuwa ya kishabiki na kikuda hata kidogo.
Kwa ufupi, sehemu rahisi ya vita hivi ni vile wauza madawa ya kulevya huwekewa mtego, wakinasa hukamatwa na kutiwa nguvuni na kushitakiwa kunako ushahidi mezani. Kisha mahakama hutoa hukumu kwa mujibu wa sheria.

Vita hii ni ya kiintelijensia zaidi, kwa sababu mabosi wa dawa za kulevya ni watu wakubwa wenye mtandao wa kidunia. Wapo maaskofu, wachungaji, mawaziri na wabunge, na maafisa usalama, wakuu wa vitengo ndani ya jeshi la polisi na jeshi la wananchi. Na hapa naweza kusema kuna watu ndani ya vyombo husika wanamchora tu huyu kijana na kucheka kindani ndani.
Unaweza kudhani unapambana na madawa ya kulevya kumbe unayapamba. China wananyonga watu wa biashara hiyo na huko ndiko kwenye soko kubwa. Unataka kupambana kwa kutajataja majina? Ok! Let's go kwenye hizi mbio za panya.
Na tatizo la mbio za panya hata ukishinda unabaki kuwa panya.
 
Kwa wenye ufahamu wa jicho la tatu la ufahamu madhubuti tasnia hii ya ungaunga ndo inaelekea ukingoni,tujiandae episode ya 9.
 
Back
Top Bottom