Makonda ni Magufuli ajaye

Mie bado nitaendelea kutatizwa na tafsiri ya ujana katika siasa!
Vijana wengi wana hari au mori ya kuwajibika na wana mtazamo chanya kuhusu dhana maendeleo ndo maana katika nchi za wenzetu unawakuta vijana wengi kwenye taasisi za umma na inawasidia sanaaa japo pia wazee hubeba dhana ya hekima ,busara,na maarifa hivyo basi na sisi inabidi tuwaunge mkono vijana wetu katika hili dhana ya maendeleo na hapa ndipo utakuta vijana makini kama MWIGHURU ,JANUARY, MAKONDA,POLEPOLE,NAPE,UMMY,KIGWANGALA,JAFFO na wengineo.
 
Nadhani Makamba ni kaliba tofauti na hao wengine uliowataja. Kwa mfano tangu serikali hii iingie madarakani hajaongea sana. I hope kwamba anakubali kuwa kuna mushkeri mkubwa wa kutofuata katiba. Kwa hao wengine sina la kusema.
 
Nadhani Makamba ni kaliba tofauti na hao wengine uliowataja. Kwa mfano tangu serikali hii iingie madarakani hajaongea sana. I hope kwamba anakubali kuwa kuna mushkeri mkubwa wa kutofuata katiba. Kwa hao wengine sina la kusema.
Wote hawa wanadhamira ya dhati kutufiksha katika uchumi wa kati ila sema kila moja ana aina ya uongozi wake kutokana na majukumu aliyopewa sema ukikaa makini na kuwatathmini utajua hawa vijana wanawajibika inavotakiwa namna ya JANUARY anavoongoza wizara yake inatakiwa iwe tofauti na NAPE AU MWIGHURU wanavoongoza wizara zao kwa sababu ni wizara tofauti ila wote wanatumia katiba moja tuu!!!
 
Hazina labda ya upigaji na usanii wa kisiasa maana jamaa nae bado tu nakumbuka nyumba za serikali ile boti ya bagamoyo na alivyotueleza wakazi wa kigamboni tupige mbizi makonda ni mchumia Tumbo tu ila kwa Serikali hii ya mizuka ndio utamuona mfanyakazi ila hana jipya bonge la msanii km bosi wake
 
Mhm
 
Kweli ni Magufuri ajaye..??

Kweli unamfananisha rais wako na vitu vya ajabu??
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako mengi lakini bado haujanipa maana ya kijana katika siasa..

"Mwighuru" na hao uliowataja ni vijana??

Tafsiri ya kijana katika siasa ni kuwa na "hari" na "mori"..??
 
kwani sio nyota?
 
Uyu dogo yupo vizuri sana, sio mnafiki alimshughulikia ma MVi na vibaraka wake katika kipindi ambacho ma MVI ana tisha. Kijana hakuogopa pembe za ma MVi akazikatilia mbali, Watanzania mwezi October 15 wakamalizia. Ni mmoja ya vijana wachache wenye Uthubutu. Alafu cha ajabu kila ukimchukia yeye ndio anazidi kupanda daraja la Uongozi. Na akifanikiwa kulimudu ili jiji basi muda si mrefu atakua na nafasi ya kupendekezwa kugombea Urais.
 
Zungumzia pia yale matukio makuu mawili. Alipompiga Warioba kwa upuuzi alioongea. Na alipofunga viatu vya Riz1 kwa nidhamu. Kweli ni kiongozi 'shupavu'.

Na nyie ndo aina ya waTanzania mnaosababisha taifa letu liendelee kwa kasi hii 'inayoridhisha'.

Shukrani kwa mleta mada.
 
Wakati sisiemu wanaandaa kina Makonda, ukawa wanaandaa kina Kubenea, sugu, msigwa, lema etc, hapo obvious no future kwa ukawa.
 
Hao wahusika walikanusha upuuuzi wenu ila bado mnafosi.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako mengi lakini bado haujanipa maana ya kijana katika siasa..

"Mwighuru" na hao uliowataja ni vijana??

Tafsiri ya kijana katika siasa ni kuwa na "hari" na "mori"..??
Ngojea nikupe mfano Mzuri kama wewe ni mkazi wa dar imepita kama wiki tatu hivi tulimwona mkuu wa wilaya Ndugu H.POLEPOLE kwa moyo mkunjufu alijitolea usiku kuyaongoza magari ambayo yalikuwa yapo kwenye foleni nzito akayapanga vizuri na foleni ikaisha ni vigumu kumkuta mtu kama profesa mbarawa kuwepo kwenye matukio kama haya ndo tunafikiria na kuja na jibu sahihi kuwa vijana wanaplay part kubwa sanaa katika kuwajibika kwa nyakati tofauti bila kujali usalama wao au itikadi za kisiasa na wazee hubeba dhana ya maarifa, hekima na busara katika uwajibikaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…