Wadau, leo wakati nakuja mjini asubuhi kulitokea kitendo ambacho kilishangaza na kustua abiria wengi katika daladala tuliyopanda... Hivyi unafahamu kuna style imeibuka kwa makonda kubeba shilingi kumi kumi esp asubuhi n usipokuwa aware unapotoa 250 n esp usipoangalia, konda hujifanya kukuonesha shs 10 plus ile 50 yako n kudai hukumpa 250, insteady 60/=????
Kwa bahati nzuri jamaa nahisi alikuwa makini leo ambaye alifanyiwa kitendo kile na kudai c kweli kwa sababu alipotoka kwake alikagua pesa alizobeba na hiyo shs 10 haikuwa yake. ilikuwa mzozo mkubwa though fainali konda ilibidi abwage manyanga.... Lakini, kwa style hii tutafika???