Makonda azidi kujikita kutetea wanyonge

Makonda azidi kujikita kutetea wanyonge

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Wananchi hao wametoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, huku baadhi wakitoka Rufiji mkoani Pwani ambao wameandaliwa utaratibu maalumu.
Baadhi yao wamesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na wenyeviti wa mitaa wanaopokea rushwa na kuwapendelea wenye fedha nyingi.

Mkazi wa eneo la Chasimba wilayani Kinondoni, Bakari Mussa amesema mgogoro kati yake na aliyevamia kiwanja chake uliamuliwa na Mahakama naye alishinda lakini amejitokeza mtu wa tatu anayedai aliuziwa eneo hilo na aliyeshindwa kesi.

"Tumekuja kupata msaada wa kisheria kuhusu masuala ya ardhi, tumeshindwa kuendeleza ardhi yetu kwa sababu ya zuio la Mahakama aliloweka huyo mtu. Ninatarajia kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa," amesema Mussa.

Kiongozi wa timu ya wanasheria, Georgia Kamina amesema mwamko wa wananchi ni mkubwa na waliojitokeza wote watasikilizwa.

Amesema timu yake ina wanasheria 150 kutoka Shule ya Sheria, ustawi wa jamii, maofisa kazi, Jeshi la Polisi na wanasheria wengine wa kujitegemea, hivyo wana uwezo wa kuwamudu wote.

Kamina amesema wengi waliosikilizwa wana matatizo ya ardhi, mirathi na ajira, ambao baada ya kusikilizwa hupewa ushauri wa kitaalamu wa namna ya kumaliza matatizo yanayowakabili.

"Tutatoa huduma wiki nzima kuanzia leo Januari 29 hadi Februari 2,2018. Tumejitolea kumsaidia mkuu wa mkoa kuifanya kazi hii," amesema.

Awali, akizungumza na wanasheria hao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka kutohukumu wananchi wanaowasikiliza badala yake watoe ushauri wa kitaalamu.

Amesema mwisho wa siku waandae ripoti kumshauri hatua za kuchukua zilizo ndani ya mamlaka yake na kubainisha njia nyingine zilizo nje ya mamlaka yake.

Chanzo: Mwananchi
 
Kweli mh Paul Makonda amegusa hisia za watu.
Tatizo la migogoro ya aridhi ni kubwa ajabu.
Kulitatu azuie Serikali za mitaa wasijifugulishe na migogoro ya aridhi kabisa,
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
 
Wewe! Mbona upo nje na hushituki? Hebu soma hoja iliyopo kama ina husiana na ulichokiandika! Lumumbans ni shida na ugonjwa wa ajabu usio na tiba kabisa. Dogo tafuta tuition au kibarua cha ulinzi uwe busy, vingevyo wehu upo kwenye paji lako la uso!
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
trump hakukosea ... hivi unajua ulichoandika ? kinahusikaje hapa.
 
Wanyonge gani hao wanatetewa? Mewafanya vijana wengi waliomaliza chuo kuhangaika mitaani halafu leo unasema wanyonge.
Watu wamefukuzwa kazi kwa kutumia cheti feki lkn wapo watu wanatumia cheti feki kwasbb wao ni special
 
KWA hiyo hapo kuna mahakama wanatoa maamuzi

Ova
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
Mkuu hii bangi uliyotumia ni hatari sana, yaani mada ni habari za makonda wewe unakuja na cdm na dk slaa. Kweli umevurugwa
 
Kweli mh Paul Makonda amegusa hisia za watu.
Tatizo la migogoro ya aridhi ni kubwa ajabu.
Kulitatu azuie Serikali za mitaa wasijifugulishe na migogoro ya aridhi kabisa,
Waraka ulisha tolewa muda mrefu sana nadhani 2009 Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilielekezwa kwa Wenyeviti wa S/Mtaa kuwa wasifanye mauzo ya Ardhi/Nyumba na Badala yake yakafanyike kwa Mwanasheria wa Manispaa au wengine..............Ni Utovu wa Maadili na tutashugulika nao.................!!!
 
Aisee inamaana ukiwa na shida au tatizo Tz ya Leo wewe ni mnyongee...?
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
Dalili za mimba huaanza pole pole mara kutapika na mara kichefuchefu cha hapa na pale. Ndugu wahi hospital ukapate dawa kabwa hujapata kifaga cha mimba
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
Tukisema CCM ni mataahira watu huwa wanabisha.
 
Laana ya kumtukana Dr Slaa na kumuita mr mihogo itawaandama milele Chadema.

Slaa alivunjwa mkono na mke wake kuharibikiwa mimba akiwa anaipigania chadema lakini akaishia kutukanwa matusi na bavicha!!

Laana hii haitawaacha salama chadema.
Ndugu yangu kama hao unaoishi nao wote hakuna hata mmoja alishawahi kukuambia/kukushauri ukapime magonjwa ya akili , bas tambua utakua unaishi na jamii ya watu wanafiki sana.
 
Wanyonge gani hao wanatetewa? Mewafanya vijana wengi waliomaliza chuo kuhangaika mitaani halafu leo unasema wanyonge.
Watu wamefukuzwa kazi kwa kutumia cheti feki lkn wapo watu wanatumia cheti feki kwasbb wao ni special
Acha ujinga wewe,ukimaliza chuo sio lazima uajiriwe,mtu aliesoma hawezi kulia ajira
 
Acha ujinga wewe,ukimaliza chuo sio lazima uajiriwe,mtu aliesoma hawezi kulia ajira
Kweli ww ni tango pori. Kwahiyo ulitaka mtu akae asiwe na ajira? Unajua ni ajira gani nazungumzia? Ndiyo tatizo la kutumia cheti cha mtu. Pole sana Shithole
 
SHERIA IPI?hi iliyopo tu hawaishimu wao.waanze kwanza wao ndyo waje wananchi cyo kuleta drama ya mizizi yangu imejichmbia hadi chn
 
bwana mdogo makonda anajitahidi sana natamani iwe hivyo nchi nzima naamini zulma itaisha

Matatizo ni mengi nchi mzima, Wakuu wengine wa Mikoa wajifunze kwa Paul Makonda.
 
Back
Top Bottom