Makonda atoa kazi kwa wakuu wa wilaya, atakayeshindwa kupangiwa wilaya nyingine

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda ametoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya kuwa wasome ilani ya CCM, wasome hotuba ya Magufuli ya kufungua bunge na pia wasome mazingira yao ya kazi kwa wiki mbili.

Baada ya hapo watatengeneza mpango kazi wa mkoa ambapo kila baada ya miezi 3 watakuwa wanafanya presentation kwenye ukumbi wa Nyerere convection kuhusu kazi walizofanya mbele ya wananchi na atakayeshindwa watampangia wilaya nyingine.
 
Safi sana, sasa hatutaki kusikia oooh nimekamata machangudoa kadhaa au wavuta unga kadhaa, tunataka kusikia utatuzi wa matatizo ya wananchi kama vile wauza unga wangapi wamekamatwa, madawati na madarasa, madawa na watumishi wa hospitali, uchafu, maji safi, rushwa, miundombinu, ujambazi n.k.
 
huyo mama hapo pembeni naona amenuna......atakaeshindwa atapangiwa wilaya nyingine? ina maana kuna wilaya kazi yao kubwa itakuwa kuchukua walioshindwa kufanya kazi?
Nadhani ni kama ue msemo wa mzee wa 'kumpangia kazi nyingine' mtu aliyemtumbua akimaanisha ndio bye bye hapo
 
huyo mama hapo pembeni naona amenuna......atakaeshindwa atapangiwa wilaya nyingine? ina maana kuna wilaya kazi yao kubwa itakuwa kuchukua walioshindwa kufanya kazi?
Mfano Mkuranga ni tofauti na kinondoni,kule unakimbizana na walanguzi wa korosho tofauti na mtiti wa kinondoni au ilala
 
Dar es Salaam tumekosa kiongozi.

Yule aliyetoka alikuwa na busara zaidi ya huyu.

Na mbaya zaidi ndo jiji ambalo ndo taswira ya Tanzania au Afrika Mashariki ukiliacha Nairobi.

Mawaziri, Mabalozi, Wabunge, Wafanyabiashara wote wanaishi mkoa huu.

Ni bora tusingekuwa na viongozi kama hawa.
 
Utaweza soma mazingira ya kazi ya wilaya nzima for two weeks, naona mambo ya mwendo kasi yanaendelea
 
Anawaambia wenzie wakishindwa watapangiwa wilaya nyingine, yeye kaweza nini mpaka awaambie wenzie hivyo? Siasa inatawala amekalia matamko mapya kila siku utekelezaji zero nae apangiwe mkoa mwingine
 
Back
Top Bottom