Makonda atoa kazi kwa wakuu wa wilaya, atakayeshindwa kupangiwa wilaya nyingine

Sasa tuelewe kuwa ni kazi tu au Matamko tu?

Wapi Viwanda?
Wapi Daraja la Aga khan to Coco Beach
Ujenzi wa Coco Beach ndiobasi tena panabakia vile vile na uchafu uchafu wa maganda ya mihogo na Mafuta yaliyokaangiwa mihogo mwezi mzima yanajaziwa tu yakipungua... Rwanda Biashara za kichafu chafu kama za pale ni Marufuku
 
Sasa tuelewe kuwa ni kazi tu au Matamko tu?

Wapi Viwanda?
Wapi Daraja la Aga khan to Coco Beach
Ujenzi wa Coco Beach ndiobasi tena panabakia vile vile na uchafu uchafu wa maganda ya mihogo na Mafuta yaliyokaangiwa mihogo mwezi mzima yanajaziwa tu yakipungua... Rwanda Biashara za kichafu chafu kama za pale ni Marufuku
kazi ndio inaanza, ila mizuka bado ipo juu
 
huyu anachekesha sana. yeye ndo atltawapangia wilaya nyingine? ndie kawachagua??? hahahha hizi sifa zingine duh, naona ana utani

una miss point...makonda ni mwakilishi wa rais, ni rais wa mkoa, kwa hiyo kufanya maamuzi yeye ata report kwa JPM...na JPM lazima masikilize, maana ni macho yake

hope umeelewa sasa
 
Dar es Salaam tumekosa kiongozi.

Yule aliyetoka alikuwa na busara zaidi ya huyu.

Na mbaya zaidi ndo jiji ambalo ndo taswira ya Tanzania au Afrika Mashariki ukiliacha Nairobi.

Mawaziri, Mabalozi, Wabunge, Wafanyabiashara wote wanaishi mkoa huu.

Ni bora tusingekuwa na viongozi kama hawa.


kafanya nini??

weka hoja acha bwabwabwa
 
Hii kidogo imekaa vizuri, mh Makonda kwa hili nakuunga mkono.
Idara nyingine zote za serikali zianzishe huu utaratibu kwa watendaji wake mfano halmashauri mkurugenzi ahakikishe kila mtu anamchango kwenye halmashauri yake na sio kusubiri mwisho wa mwezi kwani hii inaweza leta ubunifu na kuajiri watu sahihi..
 
Hii dunia ina maajabu sana hasahasa hapa kwetu Tanzania

Ni Tanzania pekee ambapo unazima bungelive kwa kudai watu hawatafanya kazi halaf unafungulia Makonda live

Sasa bora bunge tunaona jinsi pesa za walipa kodi zinavyofanya kazi kuliko Makonda live tunapoona mbwembwe nyingi vitendo sifuri

Duuuuuu! Nchi ya kufikirika
 
Badala ya kujenga mshikamano na viongozi mbalimbali wa mkoa na wa kuchaguliwa na wananchi wa dar kwa lengo la kuleta maendeleo haraka yeye anagombea majukumu yote ayatekeleze yeye, nilikuwa namuheshimu sasa nimeanza kumdharau
 
makonda mzee wa Kiki hivi.. lile la walimu kusafiri bure liliishia wapi ?
 
Madaraka hulevya zaidi ya pombe, ngoja niendelee kujipulizia shisha hapa najua hawezi kunikamata
 
kwahiyo makonda anapangia wakuu wa wilaya sehemu za kufanya kazi,kwa mamlaka yapi aliyo nayo au ndo mizuka inamuongoza
 
Mama Mjema Mkuu wa Wilaya ya Ilala tunampa hongera mwanamama kuendelea na kazi yadhihirisha anaiweza isingekuwa hivyo asingerudi! Sasa ili RC Makonda asije 'akamhamishia wilaya nyingine' wananchi wa wilaya ya Ilala wanamuomba ashughulikie barabara za Wilaya hususan za jimbo la Ukonga ambazo zilisahaulika kwa muda mrefu. Pia anaombwa awaangalie TANESCO Ukonga kwa miwani mikali kwa sababu maeneo ya Kivule, Frame Kumi, kwa Kichonge na Minazini wananchi hawaelewi zoezi kuleta umeme linakwendaje. Wananchi wanashukuru sana kwamba nguzo zimefika hadi baadhi ya maeneo ya Minazini lakini utaratibu wa usambazaji wa nguzo haueleweki. Waliambiwa watengeneze barabara za mitaa ili nguzo zipite. Wapo waliofanya hivyo lakini chakushangaza nguzo hazijaletwa zimeishia mtaa wa Minazini na nyingine zimeruka mitaa zimeenda Magole hadi kwenye eneo tata la VIKIUTA ambalo lina mgogoro watu walivamia na kukata viwanja wakawauzia watu! Wananchi ambao wana barabara tayari lkn nguzo hazijawekwa wamebaki wanajiuliza inakuwaje wakati walishalipia elfu sita za fomu na elfu thelathini za michoro tangu mwaka jana lilipotangazwa zoezi la ujio wa umeme! Wakihoji hawapewi jibu na utaratibu unaoeleweka. Mkuu wa Wilaya awasaidie wananchi hawa kwa sababu elfu 36 ni nyingi mno kwao kupotea bila kuuona umeme wakati wenzao jirani wameshawekewa nguzo.
 
Yaani makonda anashangaza mimi nimejiuliza kwamba
Je mtu akishindwa na kazi Daressalaam huwa anapelekwa mkoa au wilaya gani?
Yeye anao ushawishi/ukaribu kiasi gani kwa raisi na amiri jeshi mkuu kuamua kwamba nani abaki na nani aondoke?Nakama anauwezo wa kumshawishi raisi kiasi hicho nikwanini atuambie isiwe siri yake?
 
Hivi kwa nini huyu dogo na aliemteua wote hawana ka ka kadogo tu?? Utasemaje wapangiw wilaya zingine? Ina maana hizi w za dar ndio first class? H aliemte alisema Dar ndio Tanzania!!huwezi kusema vile ukiwa wew ndio No1! Nawaombea sana busara!!!
huyo mama hapo pembeni naona amenuna......atakaeshindwa atapangiwa wilaya nyingine? ina maana kuna wilaya kazi yao kubwa itakuwa kuchukua walioshindwa kufanya kazi?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda ametoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya kuwa wasome ilani ya CCM, wasome hotuba ya Magufuli ya kufungua bunge na pia wasome mazingira yao ya kazi kwa wiki mbili.

Baada ya hapo watatengeneza mpango kazi wa mkoa ambapo kila baada ya miezi 3 watakuwa wanafanya presentation kwenye ukumbi wa Nyerere convection kuhusu kazi walizofanya mbele ya wananchi na atakayeshindwa watampangia wilaya nyingine.


Yeye anafanya presentation wapi. Au ndio nini hii
 
Back
Top Bottom