Makonda atoa kazi kwa wakuu wa wilaya, atakayeshindwa kupangiwa wilaya nyingine

wana bodi nimemsikiliza sana mhe Makonda hotuba zake nyingi alizotoa kwanza kama hili la shisha alidai alipokuwa doubletree amemwona msichana mzuri sana mdogo akivuta shisha na sasa amepiga marufuku uvutwaji wa shisha.

Shisha huvutwa sana na vijana na wazee ambao wanajiweza kifedha je mhe Makonda je umetumwa na tajiri amabye mtoto wake ulimwona akivuta shisha?

Nasema kwa vile sikuoni ukija huku uswazi ukaona watoto ambao ndio wengi kuliko hawo wavuta shisha wachache wakivuta,bangi, gundi, unga na wanywaji viroba.

Tumekukaribisha uswazi kufuturu nasi lakini tukaambiwa uko busy siku mbili baadae unapiga picha na tajiri wa kiarabu akikufrutisha kwake.

Njoo uswazi ujionee watu wanavyobakwa kila usiku wewe unayazungumzia ya masaki na doubletree au uswazi sio dar???
 
Mihemko na matamko ya matumaini yasiyo na mashiko. Dar sio rahisi kama watu wengi wanavyofikiri
 
Asante Mungu Kanuni ya Imani nimeishika kikamilifu , haya ya wanadamu hayatabiriki. Yetu Macho in future with regards to this nation!
 
Kumpangia wilaya nyingine? Kwa hiyo yeye na Rais wanafanya kazi hiyo ya kupanga vituo pamoja?
Kweli ule usemi kuwa babu akimuendekeza sana mjukuu ataishia kumshika koro.dani hadharani uko sahihi
Rais anapokea taarifa za utendaji wa wakuu wa wilaya kwa mkuu wa Mkoa. Anaweza kusema mkuu wa wilaya fulani changamoto za mji mkubwa zimemshinda na Mh Rais akaona ampeleke kwingine. Hapo alipo Makonda anayo nafasi ya kumjadili Mkuu wa wilaya lakini mkuu wa wilaya hawezi kukaa kikao cha kumjadili mkuu wa mkoa. Hivyo anachokisema ni sawa.
 
Makonda hana uwezo wa kumpangia DC wilaya nyingine.
Huko ni kuingilia maamlaka ya uteuzi wa ma DC.
 
Makonda ameteleza.
Picha inaonyesha kwenye upangaji Wakuu wa Wilaya alialikwa!!!

Ilipaswa iwe siri
 
Ideally, raisi humtaarifu RC anampango wa kumpatia DC yupi. Na RC anao uwezo wa kumshitakoki DC kwa raisi. Kipengele hicho ndicho kinampa nguvu Paul Makonda. He knows what he is saying but am not sure about what he is doing! He seems to be enjoying to the full.
 
Yeye vipi?kwani yeye ndo aliewateua?huyu Makonda hapa Dar siku zake zinahesabika,naona anatafuta kuwa maarufu kuliko hata Raisi mwenyewe,hayo mambo si wangeandikiana barua huko maofisini,na sisi wananchi tungeona matunda tu,Makonda bado kidogo tu utumbuliwe,alitumbuliwa Kitwanga uje kuwa wewe Makonda?
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda ametoa maelekezo kwa wakuu wa wilaya kuwa wasome ilani ya CCM, wasome hotuba ya Magufuli ya kufungua bunge na pia wasome mazingira yao ya kazi kwa wiki mbili
Baada ya hapo watatengeneza mpango kazi wa mkoa ambapo kila baada ya miezi 3 watakuwa wanafanya presentation kwenye ukumbi wa Nyerere convection kuhusu kazi walizofanya mbele ya wananchi na atakayeshindwa watampangia wilaya nyingine

Kumbe kuna wilaya za kupokea viongozi vi.la.za?
Ndiyo maana huwa ninasema uDC ni uongozi wa kwanza tutakao ufuta kwenye katiba mpya ukada wao mwisho kwenye katiba mpya.
Tunataka watu wafanye kazi kwa maslahi ya Taifa na siyo chama.
 
Back
Top Bottom