Makonda atafungwa jela kimaigizo, atateuliwa uwaziri kutokea jela, CCM watasema ni shujaa

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
MAKONDA ATAFUNGWA JELA KIMAIGIZO, ATATEULIWA UWAZIRI KUTOKEA JELA, CCM WATASEMA NI SHUJAA.

Mkakati huu ulianza rasmi mwaka 2012 mimi Deogratius Kisandu nikiwa bado CHADEMA, moja ya mkakati huo ambao nilikuwa na usikia ni kuwa tukifanikiwa kumleta Deo Kisandu CCM tutakuwa tumefanikiwa kumzima na kumuinua kijana wetu yaani (Paul Makonda). kwakufanya hivyo mimi Deo nilipata suluba nyingi sana ndani ya Chadema na kulazimika kukimbilia NCCR Mageuzi kwa Kaka Mbatia.

Nikiwa huko bunge la Katiba lilipo karibia wakasema jina la Deo Kisandu litolewe atatupindua maana jamaa yuko vizuri sana, weka makonda, wakati huo wakiwa tayari wameshamuundaa Mama Samia kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Bw.Paul akaambiwa atunze siri na hivyo akaambiwa kwa kuwa Deo Kisandu huwa akitabiri jambo huwa lazima litokee hivyo kwa kuwa tumemtema bunge la katiba, utakapokuwa unachangia kwenye bunge la katiba mtaje mama samia kuwa anafaa kuwa makamu wa rais na ndivyo alivyofanya kwenye bunge la katiba kwa kumtaja mama samia na fikiri video hiyo ipo, kwa kufanya hivyo walikuwa wakimtengeneza kuwa mwenye busara mpaka kuweza kutabiri.

Nilivurugiwa mipango yangu na CCM kupitia NCCR Mageuzi na kushinikizwa kujiunga CCM na hapo ilinibidi iwe hivyo na mwaka 2014 september nilijiunga na CCM, hapo ndipo mipango yote ikapangwa ya kunidhalilisha na kunifedhehesha. Wakamwambia makonda ahakikishe atakapopewa wilaya ya kinondoni ahakikishe anamu copy na ku paste Deo kisandu kwa kila kitu, huku wao viongozi wa CCM wakiendeleza propaganda juu ya kumchafua Deo Kisandu.

Nikawasikia wakisema tuwachonganishe wapinzani mpaka wamuue Deo Kisandu halafu wakifanikiwa ndio tunasema ukweli na hapo makonda anakuwa shujaa wetu.

lakini wakawa wanapanga kuwaharibia watu wote wenye mapesa waliogoma kuichangaia CCM wakiwemo matajiri na wakamuahidi bw. makonda kuwa atawalipua wote baadae na baada ya hapo makonda atafungwa jela na kutoka kwa msamaha wa rais na kama itashindikana basi atateuliwa kuwa Waziri akiwa gerezani, na wakamuahidi kuwa huko gerezani (segerea) ataishi vizuri tu na atakula vizuri tu au wanaweza kumsafirisha nje ya nchi mpaka kifungo kikaribie kuisha au msamaha wa rais ukaribie amabapo na tangazo la kutangazwa kuwa waziri wa kwanza kutokea gerezani kwa kuweka historia.

Hivyo hiki kinachoendelea ni maigizo ya kumtengeneza shujaa wa CCM kutokea gerezani na ndio maana mpaka sasa Bw, makonda anasema kwa jeuri juu ya matajiri na watu maarufu maana anajua fika ninikilichopangwa. kwahiyo watu watamfungulia kesi na atafungwa na baada ya hapo atatolewa na kutawazwa kuwa waziri na hapo CCM watakuwa wamepata shujaa kwa kumpiku Deogratius Kisandu.

Na walivyotegemea kuwa Deo Kisandu atakufa imeshindikana na wakashangaa huyo Deo Kisandu kaanzisha chama cha siasa kiitwacho arena for Correcting africa-Tanzania yaani ACA, hapo ndipo wamechanganyikiwa na kuona labda ule mpango wao umeanguka maana Deo kainuka kivingine, hivyo ili kuwahi ushujaa wao wa kubumba ndio wameanza na mazingaombwe haya ya kutajawa wahusika wa madawa ya kulevya kwa mbembwe zisizo na msingi wa kimaadili.

wakati ukifika mtanielewa labda Mungu atengue mipango yao hii.

Deogratius nalimi Kisandu.
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.
 
Huna lolote na umefilsika kifikra na kisiasa. Hako kachama kako ka mfukoni unafikiri utamteka nani?
 
Haingii akilini kuwa polisi wadogo waliofukuzwa ndiyo walikuwa wakiwasaidia majina makubwa na maarufu yaliyotajwa kwenye vita hii ya madawa... tusidanganyane...

Ukiwa na pesa huwezi kumshirikisha mfuga mbwa lazima utamtafuta mwenye mbwa.. tuende mbali zaidi
 
Back
Top Bottom