Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuita na kuongea na Waandishi wa Habari huko Dodoma ni kulazimisha kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwakuwa Waandishi waliazimia na kuamua kutoandika habari zake kutokana na mambo yaliyojitokeza Clouds Media. Leo amewapata Waandishi wa Habari wa Dodoma na kusema mbele yao.
Makonda, akiwa nje ya mkoa wake na akiwa hana mamlaka ya kufanya hivyo (kadiri ya uelewa wangu), ametangaza kuwepo kwa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia hapa nchini. Kiprotokali, Mkuu wa mkoa si Msemaji kuhusu ziara za viongozi wa kimataifa. Wahusika ni Wizara ya Mambo ya Nje na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.
Kwakuwa taarifa aliyoitoa Dodoma inamhusu Rais na Tanzania kwa ujumla, taarifa hiyo itaripotiwa kwenye vyombo vya habari lakini yeye Makonda atatajwa kama mtoa taarifa. Nasisitiza kuwa Mkuu wa mkoa Makonda wa Dar es Salaam hana mamlaka wala wajibu wa kutangaza ziara za viongozi wa kimataifa.
Kwanini alazimishe kuandikwa na kutangazwa?