Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemtaka Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Abel Ngilangwa kuipa Simba majibu ya kinachoendelea kuhusu mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.
Makonda amesema kuwa msajili anatakiwa kabla ya mwezi huu kumalizika, awe ametoa majibu kwa Wanasimba.
βMsajili wa michezo nilitaka mkamilishe taratibu za Simba. Na nilitaka niwahakikishie kwamba katika kipindi ambacho sheria na kanuni zitafuatwa sana ni hiki cha uongozi wangu.
βKamilisha na ikiwezekana kabla ya mwezi huu uwape majibu Wanasimba. Tunachotaka sisi tuone timu hizi zikifanya vizuri. Kabla ya mwezi huu, jambo hili liwe limekamilika,β amesema Makonda.
Yani hapo Mangungu akishaondoka basi Simba inarudi kwenye ubora wake,haiwezekani mtu mmoja anyooshewe kidole na watu wote alafu watu wachache wasio itakia Simba mema watoke wamtetee.
Yani hapo Mangungu akishaondoka basi Simba inarudi kwenye ubora wake,haiwezekani mtu mmoja anyooshewe kidole na watu wote alafu watu wachache wasio itakia Simba mema watoke wamtetee.
Kwani kanuni za uwekezaji kwa timu za wanachama zilitengenezwa na nani?
Msajili anatakiwa kutekeleza mabadiliko ya katiba kwa haraka au kutoa majibu kwanini anakataa hayo mabadiliko.
Kwani kanuni za uwekezaji kwa timu za wanachama zilitengenezwa na nani?
Msajili anatakiwa kutekeleza mabadiliko ya katiba kwa haraka au kutoa majibu kwanini anakataa hayo mabadiliko.
Sasa hilo linawahusu wanachama wa klabu na sio jukumu la serikali kuna vilabu vingi vina matatizo kibau lakini serikali haina habari navyo.
Ni kupeleka tu siasa kwenye michezo ili ionekane kwa watu kwamba serikali inajali mpira wakati ni kutafuta kiki tu baada ya yale mauaji ya Oktoba 29, unafiki mtupu.