Makonda: AFCON 2027 tutawasuprise

Makonda: AFCON 2027 tutawasuprise

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
912
Reaction score
3,150
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema kuwa Tanzania ipo katika maandalizi makubwa na ya kipekee kuelekea mashindano ya AFCON 2027, akisisitiza kuwa maandalizi hayo hayajawahi kushuhudiwa hapo awali Nchini na kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mashindano hayo yanakuwa ya kiwango cha juu na yenye kuacha alama ya kipekee Barani Afrika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo April 13, 2026, Jijini Dodoma, Makonda ameeleza kuwa Serikali imejifunza kutokana na uzoefu wa Mataifa mengine yaliyowahi kuandaa mashindano hayo na tayari imebaini mapungufu yaliyokuwepo ili kuyafanyia kazi na kutoa wito kwa Watanzania kushirikiana na Serikali katika kufanikisha maandalizi hayo ili kuhakikisha Nchi inanufaika kupitia tukio hilo kubwa la kimataifa.

“Lakini Mungu huyu tunayemuabudu nina uhakika tutakuwa naye mpaka kwenye mashindano ya 2027 AFCON hapa Tanzania, mashindano hayo kwa namna Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tulivyojiandaa, haijawahi kutokea na kama kuna pahala mnasubiri ‘surprise’, Watanzania ni AFCON 2027, yaani tutawasuprise, itafika mahala mpaka mtakuwa mnalalamika punguza.”

Soma Pia: Makonda: Serikali imelipa CAF Tsh. Bilioni 82, Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON 2027

“Tumegundua na tumeshawasoma Watanzania wanapenda nini, tumeshajua ‘gap’ lililopo na tumeshajua wenzetu walifanya nini, sasa kazi mnayo na Watu wote wenye vipaji vyao baada ya kuwa tumekamilisha baadhi ya hatua za ndani kama za kiutendaji, tutaanza sasa kuomba mje mtuunge mkono.” Amesema Makonda.

 
Hizi ni kelele/mikwara ya kutafuta mianya ya kupiga
 
Back
Top Bottom