Makombora ya Iran yanafika kila kona Israel

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
Kamanda mkuu wa Jeshi la Iran Mohammed Aly Jafari amesema kuwa makombora yote ya Iran yana uwezo wa kulenga popote pale ndani ya Israel.

Ameyasema hayo wakati walipokuwa katika mazoezi maalum ya ukamilishaji wa urushwaji na majaribio ya makombora mbalimbali ya balistic.

Ilijumuisha maelfu ya kambi na vituo vya makombora vilivyopo mita 500 chini ya ardhi.

Mwishoni mwa mwaka jana Iran ilizindua kombora jipya la masafa marefu liitwalo @Eimad lenye uwezo mkubwa wa kukwepa mfumo kama iron dome na mingineyo.

Iran mara kadhaa imeonya kuwa endapo Israel itaishambulia ardhi yake basi itaangamizwa na kuzingirwa na vikosi vya Iran kwa maelfu ya makombora.


Chanzo: Radio Tehran
 
Mwarabu na mwajemi kwa kujipa promo hawajambo. Vita sio maneno mazee; ni action. Hizbullah na midevu yao wana full support ya mwajemi tangu enzi lakini kila siku wanachapwa kama watoto na kuruta wa Israel. Wana hamu ya kujaza tu wajane na mayatima hao wanaoana na kuzaliana ka kuku. Anyway, mwanamke mjane au aliyeachika ana soko sana Uajemi kuliko ambaye hajawahi kuolewa.
 
Hivi Israel ambayo ni kama mkoa wa dar es salaam haigopi kujibizana na Iran ambayo nj kubwa sana kijiografia?
 
Hizo ndio zinafanya kazi gani mkuu?
(Arrow 3) ni defence system (made in Israel) yenye uwezo wa ku intercept long range target Kwa umbali. Wa thousand.. miles... development yake tangia. Miaka 80s..to the present..
 
Mwarabu na mwajemi kwa kujipa promo hawajambo. Vita sio maneno mazee; ni action. Hizbullah na midevu yao wana full support ya mwajemi tangu enzi lakini kila siku wanachapwa kama watoto na kuruta wa Israel. Wana hamu ya kujaza tu wajane na mayatima hao wanaoana na kuzaliana ka kuku. Anyway, mwanamke mjane au aliyeachika ana soko sana Uajemi kuliko ambaye hajawahi kuolewa.


We jipe moyo tu..unafikiri IRAN ARMY ni jwtz etii? Siku inafutwa israel ktk map ya dunia ndio utawajua waajemi kina nani...
 
Iran hana lolote vikwazo vimemlemaza sana baada ya kuondolewa kaanza kelele.Majuzi meli zake za kivita zilitia nanga Dar ukizitazama unabaki kucheka jinsi zilivyochoka.
Yani zile meli zinazamishwa hta na Mkuki
 
iran missile can intercept arrow system
Mkuu samahani kidogo
Hivi haya makombora yamewahi kurushwa Israel kwenye vita yeyote ile yakaweza kupenya?

Maana nachofaham hivi juzi Ndo yamefanyiwa majaribio na test zaidi zinakuja sasa ni lini yamethibitishwa kupenya air defense za Israel?

Kama unasikiliza na kuziamini kauli za kamanda wa Iran kuhusu hizo missiles then Kuna tatizo, kwa kawaida duniani kote nchi mtengenezaji ni lazima aisifu silaha aliyotengeneza

Tunapaswa kuwasikiliza analyst ambao ni independent na sio nchi mtengenezaji

Kwa mawazo yangu arrow ina weza ku punch hayo makombora kwa sababu arrow imekua integrated Kuna arrow 1 & 2 , hizi mbili zimetengenezewa kwa high advanced radar
Uwezo wa system ku intercept makombora ni Kutokana na ubora wa radar system, namaanisha early detection

Arrow imeongezewa layer sasa imekua ni mult layer defense system na layer zote zinafanya kazi simultaneously ku punch intercontinental ballistic missiles na zaidi ya yote Israel imewekeza sana kwenye hii arrow particularly sababu ya Iran pekee na makundi anayoyafadhili

Sasa hivi sura ya vita imebadilika sana imekua ni tofauti na miaka ile Israel akiwashinda kiuraisi maadui zake wa middle east na ghuba ya uajemi, maadui wa Israel karibia wote wamehamia kwenye makombora kama last resort na wanayaboresha kila uchao, wakati wa operation cast lead kati ya hamas na Israel 2009 na pia vita na hezbollah nyuma ya hapo, makundi haya yali disrupt shughuli mbali mbali na kufanya raia kukimbilia kwenye mahandaki kila mara na vifo vilikua vingi

Tume iliyoundwa na kuongozwa na veteran wa six day war eliyau winograd ilikuja na mapendekezo ya kutengeneza sophisticated missile defense system Tatu
Arrow 1 & 2 ya long range na irome dome ya short range, kazi hii imeshakamilika ipo kwenye majaribio baharini

Hii ina maana gani?

Ina maana, kwa mujibu wa war planners ndani ya Israel security establishment wanaamini ikitokea vita na Iran ni lazima hezbollah ataingilia kama proxy kwa kurusha makombora mengi ya masafa mafupi na ya kati, wakati huo bosi wake Iran atavurumisha makombora ya masafa marefu ya ballistic, it is particularly on this note Israel ametengeneza air defense system based on those three cenarios

Kwamba arrow one itakua ikipangua ballistic missiles from Iran, arrow two itapangua makombora ya hezbollah ya masafa ya kati na iron dome itapangua makombora na maroketi kutoka Gaza kwa hamas yote haya yanafanyika simultaneously sababu systems ziko integrated

Iran anavyoboresha makombora yake Israel anafanya hivyo hivyo pia
Ndio maana wachambuzi wengi wanaiweka Israel mbele ya Iran kwenye military technology, watu wengi wanadhan makombora ya ballistic anayo Iran pekee Israel hana, hii si kweli Israel anamiliki Jericho 2 ballistic missiles zenye kuweza kwenda na hata kuvuka Iran na ni smart guided missiles

Lakini pia makombora pekee hayawezi kuamua mshindi wa vita, wengi tunafahamu kuwa Israel kwa Muda mrefu ana maintain air superiority over Iran ndio maana amekua akitishia ku bomb Iran kwa Muda sasa, anafanya hivyo akijua Iran angani ni mweupe kabisa labda kwa sasa hivi ameondolewa vikwazo sasa Iran anaweza kununua ndege mpya kutoka Russia, na pia huenda akapokea oda ya s-400 ambayo alishalipia siku nyingi Russia alishindwa ku deliver Kutokana na Iran kuwekewa vikwazo

Mwisho

Iran na Israel wote wanamiliki intercontinental ballistic missiles

Lakini nani kati ya hawa wawili ana vitu vya ziada?

Jibu ni Israel, ana airforce ya kisasa kabisa, anaweza kurusha hata ndege 100 kwa mara moja juu ya anga la Iran pre emptive airsrikes na kuharibu kabisa ballistic missiles installations, airfields, radar installations then anaendelea na kwingineko

Ana integrated defense system ya kisasa kabisa arrow

Ana silaha za nyuklia, tunazungumzia 200 war heads wakati Iran tunajua alikua kwenye program hiyo na sasa ameiacha

Tuwe objective kwenye argument zetu, ushabiki ukitawala hatuwezi kutoa professional opinion wenzetu wakafaidika na mawazo yetu

Thanks
 
ImageUploadedByJamiiForums1457681416.672549.jpg
 
Yani zile meli zinazamishwa hta na Mkuki

Narudia tena msemo wa trump japo maneno mengine sijakubaliana naye ht kidogo....ni hivi! sisi waafrika hatuna akili, tunajua kula, na kufanya ngono! hebu tafakari dogo sio unakuja na maneno ya kijiweni hapa,,,huwezi kumlinganisha MUIRAN na israel ambae western coutries wapo nyuma yake, chochote kitakachotokea pale hizo nchi zipo ready kumsaidia,
 
Iran hana lolote vikwazo vimemlemaza sana baada ya kuondolewa kaanza kelele.Majuzi meli zake za kivita zilitia nanga Dar ukizitazama unabaki kucheka jinsi zilivyochoka.
We unafikiri Israel ikiwekewa vikwazo na USA itaweza kujiendesha wakati haina rasilimali yoyote? Iran wamewekewa vikwazo vikali ambavyo visingewezesha nchi yao kuendelea ingawa walistahimili hadi sasa USA wakaona walegeze msimamo wao kuhusu Iran Nuclear Deal. Iran kwa vikwazo ilivyowekewa ni sawa na kutengwa na jumuia ya kimataifa. Sasa sipati picha siku Israel ikiwekewa vikwazo na mataifa ya magharibi itakuwaje? Maana bila mataifa ya magharibi Israel haiwezi kufanaya kitu.
 
Mwarabu na mwajemi kwa kujipa promo hawajambo. Vita sio maneno mazee; ni action. Hizbullah na midevu yao wana full support ya mwajemi tangu enzi lakini kila siku wanachapwa kama watoto na kuruta wa Israel. Wana hamu ya kujaza tu wajane na mayatima hao wanaoana na kuzaliana ka kuku. Anyway, mwanamke mjane au aliyeachika ana soko sana Uajemi kuliko ambaye hajawahi kuolewa.
Hezbollah ipi hiyo? Ile ya Lebanon?Kama Hamas na Fatah sawa, siyo Hezbollah.
Google Hezbollah Israel War, soma kwa makini mwanzo hadi mwisho.
By the way, US ndiyo anaempa kiburi Israel. Mwaka US akijitoa( lakini hatajitoa najua hilo), Israel hana chake.
 
Back
Top Bottom