Adrian Stepp
R I P
- Jul 1, 2011
- 2,764
- 2,600
Wakuu,
Tarehe 26 August niliandika niliweka bandiko kuhusu sakata la makinikia:
Kinacho endelea hivi sasa juu ya "Sintofahamu" kati ya wawekezaji na serikali kila mfuatiliaji anakijua..
Nitoe rai kwa serikali na watunga Sera kuamka na kuanza upya ili huko mbeleni tuepukane na kadhia hii ya "Mtu mzima kuvuliwa taulo" .
Kuendelea kujifariji kipuuzi kwamba Tanzania ni taifa changa na kelele za wanasiasa kutumia umasikini kama sifa ..zama hizo zimepitwa na wakati!
Wakati ni sasa! Nilisema, Ninasema na Nitasema kwamba kuanza upya si ujinga!
Jumapili njema!
Tarehe 26 August niliandika niliweka bandiko kuhusu sakata la makinikia:

Wadau, Nimeona nyuzi nyingi sana jukwaani zikizungumzia juu ya mazungumzo kati ya serikali na "wanaume" wa Canada.
Awali kama taifa tulifarijika sana na msimamo uliotolewa na Mh.Rais baada ya uwasilishwaji wa zile ripoti mbili.
Wanasaikolojia hasa wabobezi wa majanga wana kauli mbiu zao endapo unatarajia kitu ama jambo Fulani kwamba 'Be ready, Think ahead, Take care, Brace yourself' hasa katika changamoto mbali mbali za maisha.
Serikali yetu ilitutaarifu juu ya mazungumzo na wale "Wanaume" wa Canada ..Matarajio ya walio wengi ilikua ni kupata mrejesho japo kwa muhtasari wa nini kilijiri na hatua zinazofuata.
Serikali si kwamba haina majibu ila ni suala la muda tuu kwamaana ya si kila taarifa inapaswa kwenda kwa mlaji ( Mwananchi).
Katika misingi ya negotiation kwanza unapaswa kujua nini unataka lakini ni muhimu zaidi kutambua what the other party wants most! Nk
Huenda ni kweli tumeibiwa vyakutosha, tumetambua wapi tulipo chemka..sasa tusonge mbele..wakitupatia hata $5 b hewala maisha yaende na tufunge mkanda upya kwa kuweka sheria na kuziba upigaji kwenye rasilimali..
Tuanze upya! Miaka 3 ya mwisho ya utawala wa awamu ya 4 suala la gesi lilipigiwa chapuo mno..
Hivi unafaham kwamba mpaka 2014 rasilimali ya gesi asilia huko Mtwara ilikua ni ujazo wa futi trilioni 26.99 sawa na mapipa bilioni 4.86 ambayo thamani yake ( kwa wakati ule) ni $ bil.400.81 ambazo ni sawa na Tsh.tril.626.71 ambazo zingeweza kutosheleza bajeti ya nchi kwa zaidi ya miaka 40 mfululizo!!
Tuanzie kwenye gesi..madini kama tunavyo aminishwa kwamba tumepigwa vyakutosha tunaweza tukaweka tu mfumo madhubuti wa uchenjuaji na usimamizi wa mapato.
Nawaza tu kama miaka yote ndg zetu was Nyamongo kule North Mara mgodi uliokua na akiba ya madini ya dhahabu iliyokadiriwa kufikia wakia milioni 36 ambayo imeifanya Tanzania kua ya 3 duniani nyuma ya Ghana na Afrika kusini kwa uzalishaji lakini hata miundombinu ni duni..
Najua wengi wenu hamfahamu kwamba eneo la Mkuju lina hazina kubwa ya madini ya Urani yanayokadiriwa kufikia paundi Mil 182 kitu ambacho inatufanya kama taifa kuwa wa 3 barani Afrika baada ya Niger na Namibia!
Nikweli huenda tuliibiwa, lakini tuki-determine to make a fresh start we can make it!
Ukitupilia mbali sababu lukuki zitolewazo na wanasiasa duniani kote wanapo pigana vita yoyote ile msingi mkuu ni UCHUMI!
TULIANGUKA..TUMEINUKA..TUTAZAME NYUMA ILI TUSIANGUKE TENA..TUSONGE MBELE...KUANZA UPYA SI UJINGA!
Chonde chonde mnaotaka Noah zenu msinitovuge macho!
![]()
Kinacho endelea hivi sasa juu ya "Sintofahamu" kati ya wawekezaji na serikali kila mfuatiliaji anakijua..
Nitoe rai kwa serikali na watunga Sera kuamka na kuanza upya ili huko mbeleni tuepukane na kadhia hii ya "Mtu mzima kuvuliwa taulo" .
Kuendelea kujifariji kipuuzi kwamba Tanzania ni taifa changa na kelele za wanasiasa kutumia umasikini kama sifa ..zama hizo zimepitwa na wakati!
Wakati ni sasa! Nilisema, Ninasema na Nitasema kwamba kuanza upya si ujinga!
Jumapili njema!