Makinika! Sio kila changu ni binadamu

Kuna simulizi ya kweli ya jamaa mmoja nilisikia Clouds kwenye PB,jamaa alipanda Daladala ,kwenye siti akakaa karibu na demu mmoja mzuri sana kavaa hijabu,Jamaa akasema uzalendo ukamshinda akamuuliza jina akatajiwa wakaendelea na stori demu alipofika kwenye kituo akataka kushuka jamaa akamuomba namba ya simu ila demu hakumpa akamwambia tutakutana tu

Anasema zimepita kama simu mbili hivi anaona simu ngeni inaingia,kupokea anauliza nani demu akasema ni mimi Fulani tulikutana kwenye daladala,Jamaa akashangaa sana akauliza namba zangu umepata wapi?demu akasema we potezea tu,basi jamaa hakujali sana maana demu alikuwa amemchanganya.

Jamaa akaanzisha uhusiano na demu ila alimpa masharti kadhaa,nadhani baadae alihisi huyu demu sio wa kawaida sasa akawa anataka awasimulie washikaji basi kila akikaa na washkaji alitaka tu kuanza kusimulia demu anapiga simu hapo hapo anamwambia najua unachotaka kuwaambia na ukisema utajuta kwa kitakachokupata.
Jamaa anasema alihangaika sana na hio hali sikumbuki mwisho ilikuwaje ila kwa ulichokisema Mshana naamini kabisa kuna watu tunakutana nao barabarani, kwenye mabasi,masokoni nk lakini sio binadamu kwahio tuwe makini sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]aah wapi, mkuu mimi sijawahi date na watu dizaini hizo. Katika vitu sipendi ni ulozi na ushirikina.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na ndio maana huwa nawasihi sana wale wanaotaka kuona wachawi live waachane na hiyo habari maana hawataona wachawi tuu wataona kila kitu kisichoonekana kwa macho ya nyama na ndio mwanzo wa uchizi
 
Dah kwa hali hii turud tu CHAPUTA [emoji23]
 
Aisee ni kama kila kona tunawindwa kuna kipindi nikiwa uchumi wa kati , niliajiri mwanamke mmoja kunisaidia kufua baadhi ya nguo na usafi wa ndani, alikuwa kama anajilengesha halafu mimi sina mpango kuna siku aliniletea chakula πŸ—πŸŸπŸšπŸ› sijui kilibaki walikuwa na sherehe kukila ndio ikawa kosa sijui kilikuwa na nini ila alinimiliki karibia mwaka mmoja na nusu.

Mwanzoni alikuwa hata hanivutii ila ilikuwa nikimuona kama nachanganyikiwa najiona nipo juu ya dunia mshahara wake ulikuwa 30,000 kwa mwezi maana alikuwa anakuja na kuondoka, ila alifikia hatua akiomba hata 300,000 siku hiyo nitazunguka kama ni kukopa lazima azipate, alinipa raha yule mwamamke ila uchumi uliyumba na nilikuwa sipingi mawazo yake. Naiskia ana duka la jumla siku hizi Tabata na mimi ndio kama naanza kujitafuta upya maana mikosi na uzembe viliniandama, sasa hivi naishi kwa akili sana na hawa viumbe...hata shuleni tulifundishwa kisa cha "ngoswe penzi kitovu cha Uzembe" πŸ™‰
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…