HAYA BHANA 🙏🙏🙏

HAYA BHANA 🙏🙏🙏

life255

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
461
Reaction score
1,172
Haya bhana… nimekata tamaa kidogo. 😅

Kuna muda unafika unaona umejaribu kila upande, umefikiria kila njia, lakini bado mambo yamekaa kimya.

Kwa sasa sina cha kujifanya. Nimechoka, nimebanwa, na nimekata tamaa kwa kiasi chake. Lakini pamoja na yote hayo, bado naamini kuna jambo moja ambalo halijawahi kuniacha:

Mungu yupo tu. 🤲

Labda si kila mlango unaofungwa ni mwisho wa safari. Wakati mwingine unaweza usielewe kinachoendelea leo, lakini kesho ukaja kuelewa kwa nini ulipitia hapo.

Kwa wanaopitia kipindi kigumu kama mimi, msikate tamaa kabisa. Tunaweza kuchoka, tunaweza kulia, tunaweza kukaa kimya… lakini tusikubali hali ya leo itufanye tuamini kwamba kesho hakuna.

Bado tunapambana. Mungu mbele.
 
Unachosema ni kweli ila ni mwiko kukata tamaa hasa kwenye harakati za kuimarisha uchumi na maendeleo yako.
Kuna kipindi nilikuwa kwenye nyakati uliyopo sasa ila nashukuru sikuwahi kukata tamaa hata mara 1 kwa sababu hakuna wa kukutoa hapo ulipo zaidi ya wewe mwenyewe. Jipe motisha unaweza weka kila kitu kando piga kazi bila kujali elimu yako, hadhi yako kwa wanaokuzunguka. Kwa kifupi usichague kazi fanya kazi yoyote halali ukomboke vinginevyo hata ufanye maombi kutwa mara 3 haitosaidia.

Pia usiogope maneno na mawazo ya watu juu yako kwa sababu wewe ndio unajua A to Z kuhusu unachokipambania.
Kila la heri mkuu.
 
Asante Sana
 
Usikate tamaa ila usiyachukulie maisha siriaz sana mkuu huwa yanais kama unataka kushindana nayo. Tumia hesabu kali sana kutafuta pesa usitumie nguvu. Good luck
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom