Nilizungumza jambo hili hapo kabla na hapa nitarudia! Lets not try to undermine this old woman
.tutake tusitake huyu mama anajua anachokifanya! Uzoefu mkubwa ndani ya bunge unamfanya awe conversant na sheria na kanuni kadhaa za bunge! Huyu mama, kanuni nyingi zipo kwenye her finger tips! Hutaki, unaacha! Tatizo la huyu mama si Umakinda wake, bali ndo tatizo la akina mama wengi! Kwa wale madereva, wanafahamu hili vizuri sana! Ukiwa barabarani, ni heri ukamatwe na Trafiki wa kiume kuliko wa kike! Hawa watu hawana dogo; wanasimamia sana misingi na wata-sticky hapo hata kama wakati mwingine busara ingelazimisha kuivunja misingi hiyo!
Ningependa kukirudia nilichokisema awali:
"Ni jambo lililo wazi kwamba watu hukosa haki zao kwa kutofahamu sharia! Aidha, mara kwa mara hoja zenye maslahi kwa taifa zimekuwa zikigonga mwamba bungeni kwavile tu baadhi ya wabunge wetu huwa wanakosa ufahamu wa sheria au kanuni za bunge! Kwa bahati mbaya, huku mitaani wengi wetu si wajuvi wa sheria wala kanuni za bunge na badala yake tumekuwa kama bendera zinazofuta upepo!
Hoja ya Zitto Kabwe, juu ya saini 70 kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu naiunga mkono kwa 100%! Ni jambo lililo wazi kwamba, Waziri Mkuu pamoja na mawaziri wake wameshindwa kazi. Busara na uungwana wa siasa za kidemokrasia ni wao kuachia ngazi kwavile kilichotokea si majungu bali ni matokeo ya ripoti halali toka kwa taasisi za serikali zilizoainisha uozo na ufisadi serikalini. Kwa bahati mbaya, inaonekana kwamba Kanuni za Bunge haziruhusu kufanyika kwa Vote of No Confidence kwa sasa! Spika wa Bunge, amefafanua hili!
Hapa, tuweke siasa za vyama pembeni na kuangalia maslahi ya taifa! Wapo watakaomponda Spika lakini yeye alichofanya ni kuangalia kanuni zinasemaje. Ni matumaini yangu Zitto Kabwe hakutoa pendekezo hilo kwa ajili ya kutafuta cheap popurality ya kisiasa!
Hivyo basi, ikiwa Zitto alitoa pendekezo hilo kwa ajili ya maslahi ya taifa, basi aweke siasa pembeni na kufuata kanuni zinasemaje. Zitto na CHADEMA wasije wakarudi nyuma kutokana na kanuni kutoruhusu na kuamua kutumia mwanya huo kutangaza kwamba Spika na CCM wamekwamisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ili kumlinda. Kikao kijacho cha bunge hakipo mbali unless kama ipo namna ya kuitisha kikao cha dharura kushughulikia suala hilo. Hapa, ningependa kutoa wito kwa Zitto Kabwe na wengine wote (wabunge) wenye nia ya kweli ya kutokomeza ufisadi nchini kwamba wapigane kufa ama kupona kuhakikisha hoja inafikishwa bungeni kwenye kikao kijacho. Hapa, siasa ya vyama iwekwe pembeni na kuangalia maslahi ya Taifa. Ikiwa CHADEMA watataka kuitumia hoja hii kwa maslahi ya kisiasa basi hakika malengo yake hayatakuwa na manufaa yoyote kwa wananchi. Kuitumia hoja hii kisiasa itawafanya wabunge wa CCM kutounga mkono kwa vile wataona ni kuipaisha CHADEMA. Hata kama CHADEMA watazunguka dunia mzima kuelezea kukwamishwa kwa mpango huo, bado halitakuwa jambo lenye mbolea kwa maslahi ya taifa. Naamini, wapo viongozi wa CHADEMA na mashabiki wao ambao wangependa kuona CCM wanaikwamisha kura hii ili wapate sababu ya kushitakia kwa wananchi.Mawazo hayo hayana msingi na wala maslahi kwa taifa.
USHAURI WANGU: Watokee wabunge wa CCM wasio na woga na walio tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio chama. Wabunge hao wajiunge na wabunge wa upinzani (kuunda kamati isiyo rasmi) katika kutafuta uungwaji mkono toka kwa wabunge wenzao ili kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ifanyike kwa mujibu wa sharia na kanuni za bunge! Pakiwepo na kamati ya aina hii isiyo rasmi, basi ile sura ya kisiasa itaondoka na hivyo kufanikisha zoezi zima la kuuwajibisha uongozi ulioshindwa."
Hivyo basi, ikiwa pana nia ya dhati ya kufanya jambo hili kwa ufanisi na kuleta positive results, basi hapana budi Mheshimiwa Zitto afuate kanuni za bunge zinasemaje! Akiacha kufanya hivi, hoja itapigwa chini na hapo wa kulaumiwa sio Spika wa Bunge bali ni Zitto mwenyewe kwa kufanya jambo kinyume na taratibu.....sina shaka yoyote kama atafanya hivyo basi atakuwa amefanya makusudi.....ama kwa maslahi ya chama chake au kwa maslahi ya CCM! Anaweza ku-opt kufanya hivyo kwa makusudi kwavile anafahamu fika Watanzania wengi hatuatilii mambo. Hivyo, anaweza kwenda kinyume na kisha hoja kupigwa chini! Kwavile serikali haina kitengo cha proganda na kile cha CCM is dead; basi CHADEMA wanaweza kutumia mwanya huo kueneza propaganda kwamba serikali, spika na kwa kushirikiana na CCM wamezima hoja ya kuuwajibisha uongozi mbovu ulituhumiwa kufuja mabilioni ya Watanzania! Propaganda hii haitakuwa na maslahi kwa taifa hata kidogo!