Makinda kutoa Tamko kuhusu Mbunge wa Bahi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda kutoa Tamko kuhusu Mbunge wa Bahi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jun 10, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Makinda kutoa tamko Mbunge anayetuhumiwa kwa rushwa

  Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai amevunja ukimya na kueleza hatma ya Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Badwel anayetuhumiwa kwa rushwa kuwa itajulikana wakati Bunge litakapoanza Jumanne ijayo.Akizungumza kupitia Kituo cha Radio one jijini Dar es salaam jana, Naibu Spika wa Bunge huyo alisema tayari Spika wa Bunge Anne Makinda amelichukulia uzito wa hali ya juu suala hilo na ameahidi kulitolea ufumbuzi wa haraka.
  Alisema kimsingi wajumbe wa Kamati ya Bunge Hesabu ya Serikali za Mitaa (LAAC) bado wanaaminiwa na chombo hicho licha ya mjumbe wake huyo kupata tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja.Ndugai alieleza kitu kitakachofuata ni kulifikisha katika Kamati ya Uongozi wa Bunge na Tume ya Huduma ya Bunge ili kupata ushauri kabla ya kutoa maamuzi ya jambo hilo.
  Hata hivyo, alisema ni mapema kuanza kumhukumu mbunge huyo kabla ya kupatikana na hatia na kuwataka wananchi kutulia wakati mahakama inaendelea kusikiliza kesi yake kwa ajili ya kuthibitisha jambo hilo."Naomba tusubiri wakati tunaelekea Dodoma kwenye kikao cha Bunge ndipo itajulikana ni hatua gani tunachukua, lakini hapa ieleweke kwamba sio kila mtu anayekwenda mahakamani au polisi basi atakuwa mkosaji, hapa, hapana huo utakuwa mtazamo finyu," alisema Ndugai.

  Alikiri kuna baadhi ya wabunge wa kamati hiyo wamehojiwa na Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini (takukuru), lakini alieleza jambo hilo limekuwa la kawaida kwani kuna wabunge wengi wamehojiwa katika masuala mbalimbali lakini hawahusishwi na makosa.
  "Kuna wengi wamehojiwa na Takukuru kwa nia nzuri, vile ni vyombo vya dola na kitu kizuri nchi yetu vyombo vya dola ni rafiki, lazima wapewe ushirikiano," alisema.
  Aidha aliwataka watu kutowahusisha wajumbe wote wa kamati hiyo kuwa wanahusika na vitendo hivyo kwani anavyoamini ndani ya Kamati hiyo wapo wajumbe wenye heshima zao, waadilifu na makini katika ufanyaji wa kazi zao.Juni 4, mwaka huu Badwel alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kula njama ya kuomba na kupokea ya shilingi milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Spora Liana.Wakati huo huo, akiongea juzi katika kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na ITV, mmoja wa wajumbe wa Kamati la LAAPS, David Kafulila alitangaza kujitoa kwenye Kamati hiyo.
  Alisema kuwa kujitoa kwake kumetokana na yeye kuona kuwa Kamati hiyo imekosa hadhi kutokana na kutiwa na dosari na mbunge huyo na kwamba anaona wananchi watakosa imani.Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Idd Mohamed Azzan, amesema kuwa kamati yake haijatetereka wala kukosa mwelekeo baada ya kuondoka kwa Kafulila.Azzan aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu kuwa, kamati yake haijakosa mwelekeo na kama kuna tatizo ni la mtu mmoja mmoja sio la kamati nzima."Huwezi kuvunja kamati kwa sababu ya matatizo ya Kafulila, lakini mwenye jukumu la kuivunja au kuongeza wajumbe ni Spika wa Bunge sio sisi," alisema.Aliongeza kuwa, kamati yake ipo imara na inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa jamii.Mjumbe wa kamati hiyo, mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi, kwa upande wake alisema kuwa, anashangazwa na vyombo vya habari kumfanya mbunge huyo kuwa habari wakati hauzi.

  Aidha, alisema kuwa kamati yao haina tatizo na kwamba mwenye tatizo ni Kafulila ambaye amekuwa akihudhuria vikao siku anayopenda.
  "Historia ya mtu angalia alikotoka, alianza Chadema, akaenda NCCR-Mageuzi kote ameharibu ni ugomvi tu na viongozi wake huku ndani ya kamati amegombana na watu," alisema na kuongeza:"Kafulila kwenye kamati hii alikuwa mzigo, mahudhurio yake ni mabomu zaidi ya vikao kumi hajahudhuria, na hata akija hakai zaidi ya saa mbili anaondoka, kwa kweli huyu ni mtu wa namna yake," alisema.Aidha, alisema kama kweli Kafulila alikuwa anataka kuisaidia serikali kuhusiana na kauli alizozitoa dhidi ya kamati hii angetekeleza siku ya tukio na sio kusubiri vikao vya bunge."PCCB Handeni iliulizwa juu ya madai aliyotoa mbunge huyu na ilisema kuwa hawana taarifa, huyu ni mvurugaji tu," alisema.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Kesi ya mjusi imepelekwa kwa kenge
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Inavyosemekana kuna wajumbe (Wabunge) wengine katika hiyo LAAwatafikishwa mahakamani hivi punde kwani huyo badweli hakuwa peke yake, alifanya kwa niaba ya wengine kama wanne hivi akiwemo Makamu M'Kiti Idi Azzan.
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  ni sahihi kusubiri maamuzi ya mahakama kwanza ili kutoa tamko la kikanuni za bunge hasa ukizingatia kuwa yote hii ni mihimili ya serikali
   
 5. a

  andrews JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM HAWAACHI KUOTA MCHANA KWEUPE,KATIKA KAMPENI ZAO ZA KUWAPUUZA WATANZANIA WAMEANDAA ULAGHAI MWINGINE ILI WAPATE KURA ZA WAPUMBAVU.
  1.KUANZISHWA BENKI YA WAKULIMA
  2.KUANZISHA BENKI YA VIJANA
  KATIKA UANZISHWAJI BENKI HIZO SERIKALI INA MPANGO WA KUWAHADAA WATZ KWA KUWAAMBIA WATAWAKOPESHA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU,KUANZIA MILLION 1MPAKA 15.LAKINI KATIKA UOMBAJI HUO UNAHUSISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KAMA MAWAKALA WAO ILI UPATE MKOPO,CHA KUCHEKESHA ZAIDI INAAMINIKA CCM IMEJIPANGA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA URAIA NA HASA CHA KUPIGIA KURA KAMA MTAJI WA KUWAPATA HAO WALENGWA.NA KUHAKIKISHA WANAOCHUKUA MIKOPO WOTE WATAIPIGIA CCM UCHAGUZI KUANZIA UDIWANI WA 2014 NA UCHAGUZI MKUU 2015.LAKINI WAJUMBE WENGI WANA WASIWASI KUWA VIJANA WALIO WENGI WAMEELEVUKA SANA NA WATAKULA PESA ZAO NA KUWAPIGIA WAPINZANI.CCM ILITUMIA MKUTANO WA JANGWANI KAMA KIPIMA JOTO SASA WAMEANZA KUINGIWA NA WASIWASI MAANA MKUSANYIKO ULE HAUKUKAMILIKA BILA YA PESA SASA WANAJIULIZA BILA VIKINDI VYA SANAA KWELI WATAKUBALIKA,MJUMBE ALIYE KARIBU NA NAPE KASEMA CHADEMA INAWANYIMA USINGIZI KULIKO HATA MAGONJWA YA WAZAZI WAO AU WANANDOA WAO.
  BINTI MREMBO LUMUMBA CCM
  :confused2:
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Kamati ivunjwe
  wajumbe wachunguzwe....japo wa kuwachunguza nao ni tatizo
  ripoti zote walizopitisha ziangalie kwa macho mawili
  kesi ya baduwel ina ushahidi wa red handed itolewe hukumu mara moja
  JIMbo tunalihitaji please!!!!!
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Atoe ufumbuzi kwani walikuwa wote wakati anapokea rushwa? Au wao wamekuwa mahakama sasa?
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  unabold, unatumia red na unatumia capitals.... HUU NI UPAYUKAJI
   
 9. M

  MTENGE Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama kniajipanga kumsafisha ili kuondoa aibu kama walivyofanya alivyotuhumiwa bungeni spika akakaa kimya
   
Loading...