Makinda is overqualified | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makinda is overqualified

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Prophet, Apr 20, 2011.

 1. Prophet

  Prophet JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  wanamshangaa kwa jinsi anavyoliongoza bunge, hawajui wasifu wake.
  wanapandwa jazba kwa kudhani anakosea sheria, hawajasoma wasifu wake.
  wanaacha kufuatilia kinachoendelea ndani ya vikao vya bunge, eti limekosa umaarufu wake wa zamani, hawajafuatilia wasifu wa huyu mama.
  Eti na TBC1 wanaona wanapoteza muda kurusha matangazo yasiyo na waangaliaji wengi..... Walimnadi wakati wa uteuzi/uchaguzi wakiwa wameruka vipengele muhimu vya wasifu wake.

  wasifu wake unajieleza, Mh. Msekwa amemaliza kabisaaaa kwa kuusoma hadhalani...... Kiongozi wa kutunga sheria asiye mwanasheria. Wabunge watunga sheria kutokuwa wanasheria si tatizo, ila kiongozi wao lazima azijue sheria hizo tena kwa vyeti vinavyoonesha kuwa anaweza. Kama hii si hoja basi katika vyeti vyetu viwe vinapata update ya kufudhu taaluma fulani kwa kigezo cha UZOEFU na si ufaulu wa mitihani. Hivi ndivyo spika wetu anavyotaka hali iwe.
  Uwepo wa mwanasheria mkuu bungeni si hoja kulingana na majukumu aliyonayo pale bungeni. Ukweli utasimama daima kama alivyosema Shaaban Robert katika shairi lake la Ukweli (kama sijakosea, ila sintajuta kama nitakuwa nimekosea kwa kuingilia fani za kina mpoto). Ukweli huo ni kuwa kiongozi wa watunga sheria awe mwanasheria, muongoza njia lazima aijue njia.
  Hata siku moja hautaweza kutunga kitabu (Novel) eti kwakuwa umesoma novel nyingi sana, wala huwezi kuongoza filamu kwa kigezo tu cha kuwa mteja mzuri wa cinemax na alibaba. Ukibisha angalia bongo movies na linganisha na huko ambapo kuliwafanya waamini kuwa hata wao wataweza bila ya kuliona darasa hata moja la tasnia ya filamu.
  Makinda kubali yaishe, kila mtu anajua upo hapo kishabiki tu na nidhamu ya woga ya Chamachetu cha mapambo chajenga wizi.
   
 2. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Parliament of Tanzania. Kweli she's over-qualified. Maana alimaliza IDM in 1975, and never schooled again - neither a long nor short course. She's really OVERQUALIFIED, no wonder anabwabwaja tu bungeni, more dominating, more aggressive, incompetent in handling Bunge etc.....
   
 3. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,964
  Trophy Points: 280
  hiki ndicho chama cha magamba mtashangaa mengi mwaka huu, na hili halikutoka chadema maana wangeambiwa wamekurupuka
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Ila wa kulaumiwa nani? Maana Msekwa alikuwepo kwenye kamati ya CCM iliyowaengua wanashria na kumpitisha huyu mama...
   
 5. U

  Uswe JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  is this TRUE?
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red kama ni kweli basi hata mafisadi walipaswa kuihurumia nchi japo kidogo na si kutuingiza "chaka".
  Sio kwamba nadharau IDM maana kuna watu walifanya Diploma pale na wamejiendeleza na sasa wengine ni Professors na Dr (PhD) UDSM na kwingineko na they are compitent enough! Ila inaelekea mama alipelekwa pale kupata kadiploma ka kutafutia kazi za kusimamiwa na sio kusimamia watu wengine kama SPIKA.
  Kwa maana hiyo naanza kupata mwanga wa madudu ya mama huyu, si kosa lake bali WEZI WA NCHI HII.
  Kweli mlimuona Mzee 6 na hata Marando hawafai mbele ya Makinda!!???
   
Loading...