huyo mama si wangemwamisha kwanza huko Kijitonyama maana kuishi mbali na town halafu na hiyo misafara kwa kweli inakera, Leo msafara wake ulikuwa unapita rightside ya barabara kwa jinsi foleni ilivyokuwa imefunga.
mkuu, ni lazima sana kutumia hayo maneno?
Sasa Madcheda unapinga kwamba CAG hana Escort au Mutungusha hakumuona na Escort last week? Kwani Ulishinda Ali Hassan Mwinyi week yote nzima ukiangalia magari yanayopita na hukumuona CAG akipita? Hebu niweke sawa kidogo kamanda.
Wakuu, kila siku huwa napishana na makinda asubuhi akienda ofisini Dar. Huwa anakuwa kwenye Benz au sahangingi bila msafara wa polisi.
Leo jioni nimepishana na msafara wa pikipiki ya polisi na shangingi mbili nyeusi. Shangingi moja plate number yake ilikuwa imeangikwa S.
Sikuweza kuona nani walikuwa ndani kwenye kila gari. Dereva wangu aliniambia alimuona Makinda kwenye ile gari yenye plate numba ya S. Sina hakika kama ni kweli.
Kwa mwenye taarifa za uhakika, je ni kweli Makinda amepewa ulinzi na msafara wa polisi?
Soon Rastam nae atakua na msafala
Viongozi wenye stahili ya escort ni rais, makamu wa rais na waziri mkuu. Viongozi wengine hupewa escort pale wanapolazimika kuwahi katika shughuli muhimu ilhali ikihofiwa barabara zitakuwa hazipitiki kirahisi. Viongozi hawa ni spika wa bunge, mkuu wa majeshi, jaji mkuu, IGP, baadhi ya mawaziri, mabalozi na wakuu wa mashirika ya umoja wa mataifa.
hata angepewa escort ya jeshi la wananchi,tatizo ni nini?si ni kiongozi wa mhimili mkubwa wa nchi au?
mh. Sita alipoomba ulinzi walimkebehi kwa vile rostam hakuridhia, sasa makinda mtu wao ameboronga wanahangaika kumlinda, kama hizi taarifa ni za kweli inasikitisha.
Maspika wote waliotangulia sijawahi ona wakiwa na ulinzi/msafara, mh. Sita tunasali nae kkkt kinondoni alikuwa anakuja bila escot, hata msekwa sikuwahi ona akipewa escort (isipokuwa kuna siku alikaimu urais kwa mujibu wa katiba, labda kama nae kakaimu)
na bado mchecheto utazidi si amekubali kutumika na wenye dhambi, hakuna baraka hapo ni hofu tu kwa kwenda mbele.
Majambazi wakiwa wanapelekwa kisutu... na wafungwa wakiwa wanawahi chakula segerea...
Jamani, huyu ni kiongozi wa mhimili wa dola (utawala), kuna ubaya gani wa yeye kuwa na msafara na ulinzi?
Ufujaji wa nini,hv unajua hata ww ukiwa na jambo lako la dharura ,kwa mfano uko post unatakiwa kwenda tegeta unapita kwa rto unamweleza unapatiwa swipa jaribu siku 1 utaona.inasikitisha ....sana....tanzania ni ufujaji tuuu