Makete kuangukia mikononi mwa CHADEMA

Makete kuangukia mikononi mwa CHADEMA

sawa mtweve,,,muda uliotumia kureplay inaonyesha,we ndo mtweve

Kwamba kwa kujibu haraka inaleta tafsiri ya kuwa mimi ni Ahadi Mtweve mwenyewe basi vigezo hivyo hata darasa la saba hawezi kuvitumia.

Zilipotolewa tuhuma Ahadi kuhusu kazi yake ya awali Lindi na Mtwara mimi nimempigia yeye na akanipa namba za baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wenzake pale Lindi na Mtwara.

Labda kama kuna hoja nyingine nje ya hii sawa!
 
Makete anayekubalika ni Jackson Mbogella Mpiganaji Aliyejitolea Maisha Yake Kuwatetea Wanyonge wa Makete kwa Kupambana na Ufisadi Uliokuwa Umetamalaki Wilayani hapa kwenye taasisi za kanisa KKKT na Halmashauri ambapo mapambano hayo yalipelekea watu kufukuzwa kazi.

Jackson Mbogella ndiye chaguo la Wananchi wengi hapa Makete na wameapa iwapo ukawa watamsimamisha mgombea mwingine basi kura zao zitarudi ccm.

Jackson Taifa Mbogella anamtaji wa wapigakura kutoka vyama vyote hii inatokana na msimamo wake aliyouonesha wa kuupinga ufisadi kutoka rohoni na wanyonge wa Makete bado wanakumbukumbu za namna Jackson alivyowapigania haki zao

Ndugu yangu nikuunge mkono Mbogela ni kijana anayekubalika hata kwa CCM na wanna nchi wa kawaida. Namfahamu toka tuko SUA Kabla ya kufanya Kazi na iliyokuwa taasisi ya masuala ya HIV/AIDS there in Makete. In case if CDM will take another candidate apart from Mbogela CDM will loose that jimbo asubuhi saa 4
 
Nafuatilia sana siasa za Makete, ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa watakaopiga kura Makete baada ya kujiandikisha huko.

Huyo Jackson anadhani ataweza mgombea kwa kutangaza nia kwenye facebook na whatsapp? Au mnataka kuleta mabishano ya kufurahisha jukwaa. Huyo Jackson kama kweli anaipenda Makete aende huko vijijini akajenge Chama, anategemea kushinda kwa kupigiwa kura na CCM kama hao wapambe wake wanavyosema kuwa asipopita wataichagua CCM?

Kupambana kwenye mitandao bila kujenga chama ni kufifisha mapambano ya kuleta ushindi Makete.
 
Habari hizi si za kweli nadhani mreta mada ameamua kumpigia debe Ahadi Mtweve. Hakuna chombo cha habari kinachomzungumzia hata kimoja na wala si facebook wala WhatsApp wanaomwongelea.

Mimi binafsi ni mwenyeji wa Wilaya ya Makete na vile vile nipo kwenye mitandao karibu yote ya watu wenye asili ya Wilaya ya Makete. Sijamsikia zaidi ya Group ya WhatsApp ya Makete Platform na Makete Yetu Forum ambako alitoa CV yake nusunusu. Walipomwambia aeleze sehemu alizowahi kufanyakazi; hakuwa tayari kuwambia watu waliyomwuliza. Hili limewatia shaka watu wengi kuwa huenda hakuondoka vizuri alivyokuwa tigo na voda.

Wilaya ya Makete haiwezi kumpa mtu wa kujifunzia kuitawala. Wanachotakiwa ni kuanza na Udiwani ili wakomae kwanza kabla ya kukurupukia Ubunge. Vijana wote waliyotia nia kugombea Ubunge Wilaya ya Makete bado hawana sifa za kuwa Wabunge. Wengi wao wanasukumwa na njaa na uchu wa kuwa wabunge. Ubunge sio makalio kwamba kila mtu atakuwa nayo.

Wilaya ya Makete tupo makini sana hivyo hatuwezi kuruhusu watu wasiokuwa na sifa kutuongoza eti tu wanataka kuwa wabunge.

Mleta mada naomba uangalie vizuri taarifa zako. Usije na wewe ukawa unasukumwa na njaa ili ushibishe tumbo lako.

lli Chadema iweze kushinda uchauguzi Jimbo la Makete hawana budi kuanza na kujikita kwenye level ya Kata (Udiwani), zaidi ya hapo watashindwa kila mwaka wa uchaguzi. Ikumbukwe kuwa Wakinga ni wagumu kukubali mabadiliko. Wagombea Ubunge kupitia Chadema waliotangaza nia kwa mwaka huu hawana Agenda waliyoibeba kwa ajili ya kuwafanya wakubalike na Wanamakete. Ninachoona mimi wagombea hawa wana mihemko tu ya kutaka ubunge!
 
Mnataka wote wagombee Udiwani ili Mahenge apite bila kupingwa? Naona wapambe mmeanza kuweweseka wacha vijana wawashe moto. Madiwani watakaosimama wanatosha na ushindi wa kishindo kwa madiwani wa CHADEMA haukwepeki.

Komaeni makamanda hakuna kuchaguliana pa kugombea hapa. Peopleeees!!
 
Nafuatilia sana siasa za Makete, ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa watakaopiga kura Makete baada ya kujiandikisha huko.

Huyo Jackson anadhani ataweza mgombea kwa kutangaza nia kwenye facebook na whatsapp? Au mnataka kuleta mabishano ya kufurahisha jukwaa. Huyo Jackson kama kweli anaipenda Makete aende huko vijijini akajenge Chama, anategemea kushinda kwa kupigiwa kura na CCM kama hao wapambe wake wanavyosema kuwa asipopita wataichagua CCM?

Kupambana kwenye mitandao bila kujenga chama ni kufifisha mapambano ya kuleta ushindi Makete.

Ngugu yangu kwa jinsi unavyoandika na kujibu hii thread naomba niungane na one of the members in this thread who said wewe ndiye unajipigia promo and its obvious unataka Ubunge kwa kila Hali...
 
Makete anayekubalika ni Jackson Mbogella Mpiganaji Aliyejitolea Maisha Yake Kuwatetea Wanyonge wa Makete kwa Kupambana na Ufisadi Uliokuwa Umetamalaki Wilayani hapa kwenye taasisi za kanisa KKKT na Halmashauri ambapo mapambano hayo yalipelekea watu kufukuzwa kazi.

Jackson Mbogella ndiye chaguo la Wananchi wengi hapa Makete na wameapa iwapo ukawa watamsimamisha mgombea mwingine basi kura zao zitarudi ccm.

Jackson Taifa Mbogella anamtaji wa wapigakura kutoka vyama vyote hii inatokana na msimamo wake aliyouonesha wa kuupinga ufisadi kutoka rohoni na wanyonge wa Makete bado wanakumbukumbu za namna Jackson alivyowapigania haki zao

Huyu anagombea kupitia ACT -Wazalendo na si Chadema
 
As matter of fact Kama wewe si Mtweve ... Kamuulize Mtweve how many times when in villages ameulizwa where is Mbongela ... The candidate? ... These are some of the signs to show how Mbogela is accepted... Km unataka kuwa mtu mwema just accept the fact siyo porojo tu
 
Mkuu Singwa ebu jibu hoja usitulazimishe kumkubali mgombea wako. Hapa tunatoa analysis na si kusifia wagombea Mkuu!
 
As matter of fact Kama wewe si Mtweve ... Kamuulize Mtweve how many times when in villages ameulizwa where is Mbongela ... The candidate? ... These are some of the signs to show how Mbogela is accepted... Km unataka kuwa mtu mwema just accept the fact siyo porojo tu

Najua wewe huijui Makete na ni mchanga wa siasa za Makete. Jackson hata kwao kata ya Iniho hapati kura, kufahamika kwa baadhi ya watu pale Iwawa ndo ushindi?

Ni lini umethibitisha kutajwa kwa Jackson huko vijijini? Acheni uongo, mtasababisha Jackson akose kazi na pia akose nafasi hata ya kugombea kwa kumpa sifa za uongo!
 
Ila tukifikia hatua ya Makete kwende mikononi mwa CHADEMA basi hakuna ubishi nchi imeishakombole Oktoba tupo Ikulu
 
Nipo hapa kutoa clarification kwa mujibu wa post yangu na kile ninachokijua kuhusu bwana Ahadi Mtweve, kama kuna hoja ileteni hapa niijibu!
 
Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa Tigo branch za Lindi na Mtwara wanasema huyo jamaa alikuwa ni mchapakazi sana, hapendi uvivu, mtetezi wa wateja na asiyependa mizaha kwenye mazingira ya Kazi. Tabia yake hiyo ilimfanya achukiwe na baadhi ya wafanyakazi wenzake.
asante sana mkuu .
 
Ila tukifikia hatua ya Makete kwende mikononi mwa CHADEMA basi hakuna ubishi nchi imeishakombole Oktoba tupo Ikulu
mkuu habari ndio hiyo , ccm chali nchi nzima , tegemeo lao sasa ni polisi na BVR.
 
Hutakiwi kujibu hoja unatakiwa kwenda kwenye uhalisia kijana,uchu wa madaraka ni tatizo la watanzania wengi,nimesoma post cjaona cha maana zaidi ya uroho wa madaraka mliokua nao,
Hzo write up zimemfaidisha nan?
 
Najua wewe huijui Makete na ni mchanga wa siasa za Makete. Jackson hata kwao kata ya Iniho hapati kura, kufahamika kwa baadhi ya watu pale Iwawa ndo ushindi?

Ni lini umethibitisha kutajwa kwa Jackson huko vijijini? Acheni uongo, mtasababisha Jackson akose kazi na pia akose nafasi hata ya kugombea kwa kumpa sifa za uongo!

You sounds kuwa na hasira ...
 
Nimeongea na wafanyakazi kadhaa wa Tigo branch za Lindi na Mtwara wanasema huyo jamaa alikuwa ni mchapakazi sana, hapendi uvivu, mtetezi wa wateja na asiyependa mizaha kwenye mazingira ya Kazi. Tabia yake hiyo ilimfanya achukiwe na baadhi ya wafanyakazi wenzake.

Acha kutetea vitu usivyovijua.
 
Nimjuavyo ndugu Mtweve ni mtu anayekubali kukosolewa, ni mpiganaji na mzalendo na Makete. Kwa kunukuu maelezo yake

1. Ndiye katibu mwenezi wa kwanza aliyetumia elimu yake kujenga chama kwenye kata yake ya Matamba na kusababisha CDM kuwa na nguvu sana ukanda huo.

2. Amejitoa na kwenda jimboni kujenga chama kijiji kwa kijiji tangu mwaka 2013 (rejea wall yake ya facebook)

3. Ndiye mmoja wa waanzilishi wa Uwanji Development Trust taasisi inayosomesha wanafunzi zaidi ya 70 kwa level ya secondary hadi chuo wanafunzi wote wanatoka Makete

4. Ameshakuwa kiongozi ndaninya chama kwa ngazi mbalimbali kama CV yake inavyoonyesha.

5. Amekuwa mchapa kazi tangu akiwa kazini kwake kwenye maeneo aliyofanya kazi Vodacom na Tigo
 
Muulize kwa nini alifukuzwa tigo Lindi.
 
NCHI NILIZOTEMBELEA
Ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Mozambique, Zanzibar na Malawi.
Kwa CV hii inaelekea haijui nchi yetu. Nchi hapo kwenye red haipo. Labda angekuwa anagombea jimbo la Mchambawima Znz angepewa kura zote. Kwa hili ameonyesha very low Profile ya uelewa wake hasa kwa GT.
 
Back
Top Bottom