Makavu Makavu kwa CHAKUUWAWA

Sep 28, 2012
87
0
Makavu Makavu kwa CHAKUUWAWA

CHAKUUWAWA ndicho CHAma cha KUukaburu Umri wa WAtu WAzima ambacho kimeasisiwa na January Makamba na mwenzake Zitto Kabwe.

1. Hawa waasisi wa huu upuuzi walilewa sifa zetu (wazee kwa vijana) kuwaona kuwa wanajitahidi katika medani za siasa ama kwa kuonekana kuwa ni watetezi wa wanyonge au ni wabunifu. Walijisahau na kujiona kuwa kilichowafikisha walipofika ni umri wao wa kuzaliwa baada ya uhuru wa nchi yetu!CHAKUUWAWA- Kiuwawe!

2. Hawa ni makaburu wa umri maana wanadhani kuwa wao walipata hati milki ya kuamrisha uogeleaji wa mbegu za baba zao na urutubishaji wa mayai ya mama zao ili mimba zao zitungwe kabla ya uhuru! CHAKUUWAWA- Kiuwawe!

3. January, hujui kuwa kwa kuwabagua watu wazima katika jamii kwa kejeli kuwa hawafai kugombea unatufanya tufikirie kwa upya kama kweli ulifaulu vyema shule yako uliyosoma katika kozi ya maridhiano na ujenzi wa amani, ICAR George Mason University, US. Kwani badala ya kutangaza amani unatangaza ubaguzi uletao matabaka na vita. Katika utangulizi wa tovuti yako, (January Makamba.com), mwishoni umekiri kuwa “I will finish by admitting that my last name (i.e. MAKAMBA) has helped me because of the ready-made network of willing helpers”.

Kwa hiyo jina la Makamba liliweza kukubeba pengine ukaingia Foreign Affairs na kuwa karibu na Waziri JK na ukapata fursa ya kuwa katika Kampeni za JK (2005) na kuleteleza kuitwa Ikilu na kuzawadiwa wadhifa nyeti wa (Personal Assistant to the President – Special Duties) na kusababisha Rais, Ikulu na CCM (T) kwa ujumla kukupa shavu katika Kampeni yako ya pesa ndefu na msukumo mkubwa kama inavyoonekana kule Bumbuli, (Bumbuli songa - by Jobiso - YouTube) na kama ilivyotegemewa ugagawiwa Unaibu-Waziri tena Wizara kama injini ya maendeleo ya nchi ‘Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia’. Je ambao hawana majina ya (ready- made network) ya kuwabeba kwa nini unawazuia wasitumie umri wao mrefu wa maisha yao ya kuwatumikia watanzania ili Wananchi wapate kuamua kama waliridhishwa na huduma zao au la? Kwa nini mnatatulazimisha tuwashindanishe watu kwa kiashirio cha usasa wa mimba iliyomzaa mgombea? Kwa nini uliamua bila aibu kupanda mbegu ya unyanyaswaji wa kiumri pale UDSM.CHAKUUWAWA- Kiuwawe!

4. Zitto kwa kuwabagua watu wazima, unatekelezaje kwa vitendo, mafunzo uliyopata katika Module 2 ya MLB hapo Bucerius Law School, Germany(accredited in 2000) au nawe umesoma kwa ‘correspondence’ bila kuzama na kupata ufahamu wa mada husika e.g the topics of relevance of values and human rights maana ulisoma (2009 - 2010), wakati wewe tayari ulishakuwa Mbunge (fulltime work) toka 2005.

Kwa siku za hivi karibuni wananchi hatuhitaji king’amuzi kukusoma kuwa wewe kijana aka Prezo hakika ni mtu wa namna gani. Kama mwenzako mmelewa sifa na umejidhihirisha uwanachama –mapacha wako (dual membership) ndani ya CHADEMA & CCM kwa kuleta mtafaruku mkubwa BAVICHA kwa kumtukana Dr. Slaa kuwa ni ki-Babu na kujinyanyua kwa kiburi kuwa wewe ndiye unafaa. Kamwe huwezi kujilinganisha na Dr. Slaa hata ungetafuta ubashiri wa nyota toka kwa Marehemu Yahya (check kura ya maoni hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/298724-kura-ya-maoni-zitto-vs-dr-slaa-3.htm. Zito una 25% wakati Dr. Slaa ana 85% ya kura zote. Mwaga kipunga dakika za mwisho yule moderator anayekutetea kila mara achakachue uonekane wewe ndie uko juu kama ulivyozoea kucheza na media, bado hutaweza kumkaribia Dr. Slaa kwa kila vigezo vya uongozi bora. Kiukweli hata tungeweka kura ya maoni kati yako na Mnyika au Mdee utapigwa chini kwa kiasi kikubwa. Hata huko CCM kamwe hutapata nafasi yeyote kwa jinsi ulivyodharau watu wazima na wazee waliokufundisha siasa akiwemo rafiki yako Salim A. Salim ambaye naye alizaliwa kabla ya Uhuru na mbaya zaidi ni mchezo wako wa uanachama –pacha ambao wewe ni janga la vyama vya upinzani. CHAKUUWAWA- Kiuwawe!

Naweza sema, kheri mzee mwadilifu, mwenye uwezo na uzoefu wa uongozi bora kuliko kijana kihuluku sadifu cha kifisadi; CHAKUUWAWA- Kiuwawe! Wakati ukifika, Wananchi waachwe, wataamua wagombea wenye sifa za uongozi bora ambazo ni zaidi sana ya birthday zao!
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,947
2,000
"Wakati Ukifika, Wananchi Waachwe Wataamua Wagombea Wenye Sifa Za Uongozi Bora Ambazo Ni Zaidi Sana Ya Birthday Zao" Best Line Ever.


Merry X-Mass To You All. CHAKUUWAA - Kiuwawe
 
Sep 28, 2012
87
0
"Wakati Ukifika, Wananchi Waachwe Wataamua Wagombea Wenye Sifa Za Uongozi Bora Ambazo Ni Zaidi Sana Ya Birthday Zao" Best Line Ever.


Merry X-Mass To You All. CHAKUUWAA - Kiuwawe

Puppy unaona hii thread itafichwa mbali sana lakini nitaiibua popote watakapoiweka maana inachoma mkuki moderator yeyote anayetaka kuichakachua. Na nitaipeleka katika mitandao yote . Tusichezewe hapa na watu wasaliti wanaotukana watu wazima na wazee wakati wao ni walafi wa nyadhifa. Unajua JF inapendwa kwa sababu watu wanaammini kuwa wanaweza kusema yaliyo moyoni na akilini (ya ukweli) hapa lakini kama kuna mbinu chafu msishangae JF nayo ikafa siku za usoni na watu wakaanza kuijadili kama chombo cha wanaotumika!!! Mimi ni Ombudsman! Huwezi kuficha uzi huu tafadhali sana!:whistle:
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Puppy unaona hii thread itafichwa mbali sana lakini nitaiibua popote watakapoiweka maana inachoma mkuki moderator yeyote anayetaka kuichakachua. Na nitaipeleka katika mitandao yote . Tusichezewe hapa na watu wasaliti wanaotukana watu wazima na wazee wakati wao ni walafi wa nyadhifa. Unajua JF inapendwa kwa sababu watu wanaammini kuwa wanaweza kusema yaliyo moyoni na akilini (ya ukweli) hapa lakini kama kuna mbinu chafu msishangae JF nayo ikafa siku za usoni na watu wakaanza kuijadili kama chombo cha wanaotumika!!! Mimi ni Ombudsman! Huwezi kuficha uzi huu tafadhali sana!:whistle:


Ombudsman, mbona unajishtukia?
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,033
2,000
Nakuunga mkono mia mi hata cku moja cwezi kumzungumzia zito coz ni kinyaaaaa tu mshirikina mkubwa .
 

Pancras Suday

JF-Expert Member
Jun 24, 2011
7,845
2,000
CHAKUUWAWA kiuawe oyeeeee! Polele mzee sisi ndio vijana wa siku hizi tunaweza hata kumvua mzazi nguo hadharani
 

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,489
2,000
Wana laana za ulafi wa madaraka hawa vijana, na wanafikiri kwa umbali wa upeo wa pua zao,wanadhani wao watakuwa vijana milele? Vilaza hawa
 

kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,233
2,000
Hivi nikweli kuna wakati ZITO alitaka kugombea Ubunge Kinondoni badala ya Kigoma?
 

Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,947
2,000
Chakuuwa Kiuwawe na wakiificha hii thread basi hawaipendi Tanzania. Inafaa Kila mmoja wetu asikilizwe akiwazacho na kukisema kwa manufaa ya nchi yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom