Makato ya HELSB 15% kwa wafanyakazi ni dalili ya uongozi mbaya Tanzania

Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
4,818
6,464
Kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya kwa wafanyakazi hata ile morali ya kufanya kazi na uzalendo unapotea. Serikali yenye uongozi mzuri huwajali wananchi wake na hata inapoidhinisha makato kama haya 15% lazima ihusishe vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wenyewe na pia lazima ipandishe mishahara ili kupunguza ukali wa maisha kwa wafanyakazi wake.

Mkataba wa HELSB unasemaje kuhusu makato ya mnufaika wa mkopo? Unasema atakatwa 8% ya kutoka kwa mshahara wake. Kulipa deni ni jambo zuri na lenye manufaa, je mshahara wa mfanyakazi ukoje? Waziri kwa mwezi anapokea zaidi ya milioni mbili za kitanzania na ushee pamoja na posho lakini mfanyakazi wa kawaida serikalini anapokea laki nne bila posho na wengine wakiwa na posho.

Hivi kweli huyu mfanyakazi ataendelea lini? Posho mepunguza, wengine mewatolea kabisa, hakuna kupandishwa madaraja, na no increment. Mshahara wa miaka 2000 ndiyo huo huo analipwa mfanyakazi lakini huwezi kukuta raisi, mawaziri na wabunge wanalipa mshahara huo huo kila siku.

Wafanyakazi kwa sasa wamegeuka watumwa katika nchi yao, tumerudi kipindi cha enzi ya mkoloni wa mjerumani. Unafanya kazi upate ugali tu. KAZI YA KUFANYIA TUMBO TU NI KAZI MBAYA SANA NA NI NGUMU NA INAYOHITAJI UVUMILIVU WA HALI YA JUU (Mshahara unaopata ni kwa ajili ya kununulia chakula tu, ukitaka kufanya mahitaji mengine mfano kujenga nyumba, kununua mashamba mahesabu yanagoma)

Raisi na timu yako waangalie wafanyakazi kwa jicho la 3, hii nchi ya kwetu sote na hakuna mtu aliyejuu ya sheria.

N.B

Kama ni suala la kulipa deni mbona serikali bado inadaiwa? Tangu nikiwa mtoto wa miaka 2 serikali ilikuwa inadaiwa mpaka wa leo kwanini isilipe pesa inayodaiwa? Na Je, ushasikia serikali imeongezewa riba kwa kuchelewa kulipa deni au madeni?
 
Mrisho mpoto kaisha muongezea cheo kingine kua ni rais mteule wa mungu, ama kweli njaa mbaya saaana huyu anaweza hata tumika katika harakati za kubadilisha katiba ili sizonje wake aongezewe vipindi vingine kama kagame.
 
Katika hili Rais alipotoshwa...mbaya ni wabunge kukubali kulipitisha na hivyo kuakisi ile dhana ya wabunge kutetea matumbo yao tu.
 
Back
Top Bottom