Makatibu wakuu na manaibu wote wapewa semina elekezi Ikulu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,719
55,829
Balozi Ombeni Sefue afungua semina elekezi ya siku moja ya makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu Ikulu Dar es Salaam.

Hii ni tofauti na tangazo lililotolewa na Rais kwamba awamu ya tano haina semina elekezi, bali viongozi walioteuliwa wajielekeze wenyewe kwenye matatizo ya wananchi.

Nawatakia kila la heri.
View attachment 314395
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015

View attachment 314395 View attachment 314396
Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Last edited by a moderator:
Acha kukariri, semina elekezi zilifutwa kwa mawaziri ila kwa hawa makatibu wakuu walisema zipo na n 1day, ili waanze fanya kazi kwa kasi zaidi
 
Balozi Ombeni Sefue afungua semina elekezi ya siku moja ya makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu Ikulu Dar es Salaam.

Hii ni tofauti na tangazo lililotolewa na Rais kwamba awamu ya tano haina semina elekezi, bali viongozi walioteuliwa wajielekeze wenyewe kwenye matatizo ya wananchi.

Nawatakia kila la heri.

Correction Mkuu: Mheshimiwa Rais hakusema kuwa awamu ya tano hakutakuwa na semina elekezi bali alisema hakutakuwa na semina elekezi kwa Mawaziri aliowateua bali wakajielekeze wenyewe huko huko maeneo yao ya kazi.

Haja ya kuwapa semina elekezi Makatibu wakuu na manaibu Makatibu wakuu wa serikali ni la muhimu sana kwa sababu wao ndio watendaji wakuu wa serikali.
 
kk9.JPG

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015

kk9.JPG
kk9.JPG

Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Sasa mboa walituambia serekali ya Dr Magu hakuna semina wala warsha.
 
Sasa mboa walituambia serekali ya Dr Magu hakuna semina wala warsha.

Suala ni gharama. Hapo hakuna cha allowance. Dhana ya semina elekezi wakati wa JK na hii ya JPM ni mbingu na dunia. Na kama tukiwa wakweli, hii ya JPM haipaswi kuitwa semina elekezi ili kutofautisha na zile za JK
 
Correction Mkuu: Mheshimiwa Rais hakusema kuwa awamu ya tano hakutakuwa na semina elekezi bali alisema hakutakuwa na semina elekezi kwa Mawaziri aliowateua bali wakajielekeze wenyewe huko huko maeneo yao ya kazi.

Haja ya kuwapa semina elekezi Makatibu wakuu na manaibu Makatibu wakuu wa serikali ni la muhimu sana kwa sababu wao ndio watendaji wakuu wa serikali.
haijalishi awe waziri au katibu mkuu crush program ni muhimu sana,atakuwa kaishaona makosa waliyokwisha fanya mawaziri wake kama kigwa kugeuka mlinzi wa pale wizarani kwake kuzuia wafanyakazi waliochelewa wasiingie ndani au kumvizia dokta mwaka na kukimbizanana nae kwenye mitaa ya ilala,hiyo sio kazi ya waziri
 
Sasa mboa walituambia serekali ya Dr Magu hakuna semina wala warsha.
Kwani unadhani kuna gharama iwapo imefanyikia ikulu?? Zile za JK zilikuwa zinafanyikia Ngurdoto Arusha wakati mawaziri ofisi zao zote kuacha TAMISEMI ziko Dar.
 
Kwenye semina warsha ndiko ufisadi unapoanzia. Ile semina elekezi ya ngurdoto ilikuwa ndio uhalalishaji wa semina zote zilizofuatia na kuitia hasara za serikali. Ofisi za wizara zipo maeneo ya posta mpya katikati ya jiji la dar lakini wakurugenzi wanafanya semina kwenye hoteli ya bagamoyo na wanajifungia kwa wiki nzima!. Akili ya kutafuta allowance inazaa ile akili ya kutafuta mianya ya upigaji (wizi). Lakini kwa uongozi wa sasa hakuna atakayethubutu kuipeleka semina Bagamoyo au whitesands hotel.
 
One day plus maji na karanga kwisha kazi
Ninaona kila mmoja kawekewa kachupa ka maji ya Uhai ka shs 300/ kama sikosei, na ka sauce kenye nadhani ka-ugali! Mhh hamna hata mmoja aliyekala hako kaugali na kunywa hako ka maji!
 
Back
Top Bottom