Awamu ya kwanza ya wanajeshi wa Ufaransa wapatao 1,500 wameondoka nchini Niger baada mamlaka ya kijeshi iliyochukua madaraka ya nchi hiyo mwezi Julai, kuwaamuru Wafaransa hao kuo#tunaliwezeshataifa.
Mamlaka katika Mji Mkuu wa Niamey imesema kuwa askari hao wameanza kuondoka katika ngome zao nchini humo, wakiwa wanaenda “uelekeo wa Chad,” huku kikosi chao cha kwanza kikisindikizwa na wanajeshi wa Niger.
Kwa mujibu wa mtandao wa Aljazeera, jana Jumanne Oktoba 10, 2023, magari ya wazi pamoja na yale yenye vifaa vya kuzuia vilipuzi, yalionekana yakiwa yamewabeba wanajeshi hao wa Ufaransa, yakipita njia za vumbi na kuondoa katika mji huo wa Niamey.
Katika taarifa ilisomwa kwenye luninga ya taifa, utawala wa kijeshi nchini humo, umewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa msafara huo, ambapo wamesema, utahusisha askari 1, 500 watakao ondoka kwa njia ya barabara kuelekea Chad, ambayo ni safari ya mamia ya kilometa, huku ikiwalazimu kupita maeneo yenye hatari.
“Leo vikosi vilivyokuwa Ouallam, vimeondoka katika ngome yao, haya ni maandalizi ya kuondoka kwa awamu ya kwanza ya askari watakaotumia njia ya barabara kuelekea Chad, wakisindikizwa na vikosi vyetu vya ulinzi na usalama,” Jeshi la Niger limesema.
Mbali na wanajeshi hao watakaondoka kwa njia ya barabara, “ndege tatu maalum” zimesajiliwa katika uwanja wa ndege wa Niamey, kati ya hizo, mbili ni kwa ajili ya kuviondoa “vikosi maalum” na moja ni maalum kwa ajili ya “vifaa.”