Makao Makuu ya Wilaya Ilongero: Wananchi wauziwa mbuzi kwenye gunia

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Kuhusu makao makuu ya wilaya: wananchi wa ilongero wauziwa mbuzi kwenye gunia.

Chama na Serikali waendelea kufanyia kazi zao Singida Mjini na sio Makao makuu Ilongero kama ilivyoamuliwa.

Jana tarehe 20/03/2017 CCM Wilaya ya Ilongero wamefanyia kikao chao Singida mjini badala ya Ilongero ambako ndio walihamishia ofisi zao. Hiyo ni tisa, kumi ni leo ambapo kuna kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida/iIongero lakini kinafanyikia Singida Mjini huku amri halali iliyotolewa na Serikali, Wizara na Mkoa ni kwamba vikao vyote hivyo vifanyikie Ilongero. Chama walishahamishia viti na meza Ilongero lakini vikao vinafanyikia Singida Mjini.

Je hii ni dhihaka kwa Rais Magufuli??
Je wananchi wa Wilaya hii mpya wameuziwa mbuzi kwenye gunia??
Chama na Serikali vimewahadaa wananchi??

Rais magufuli tunaomba usikie kilio chetu wananchi tunaotaabika kufuata mbali huduma wakati ulishatoa agizo lakini watendaji wako wana kiburi wakiongozwa na mbunge Lazaro Nyalandu na Elia Digha Mwenyekiti wa Halmashauri.
 
Back
Top Bottom