Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,932
Ukitembea Tanzania vijijini utakuta huko kuna misikiti na makanisa ambayo wanavijiji huabudu Mungu wao. Misikiti na makanisa hayo yaliyopo vijijini ni yale ambayo yamekuwepo siku nyingi. Ningependa kujua hivi huko vijijini au mikoani kuna makanisa ya Lwakatare, Kakobe, Agape au Mlima wa Mabadiliko etc etc? Nauliza hivyo maana nikiangalia lifestyles za viongozi wa haya makanisa ya 'kisasa' hayaendeani na hali halisi ya mwananchi wa kawaida. Je ina maana wanavijiji, wakulima, wavuvi etc hawahitaji 'upako'? Nasikia kuna makanisa yanayoendesha 'lunch hour fellowship' huko mijini. Je inawezekana hawa viongozi kuanzisha pia fellowships hizo kwa wakulima, kwa mfano wakiwa nao wamepumzika mchana baada ya kupiga jembe nao kfanyiwa 'lunch hour fellowships?:thinking: