Kapyepye Mfyambuzi
JF-Expert Member
- Jun 18, 2020
- 542
- 918
Habari wadau?
Bila ya kupoteza wakati Naomba twende moja kwà moja kwenye mada kama inavyojieleza hapo juu.
Manabii Wa sasa Ku promote Mafuta, Maji, Chumvi, Leso (vitambaa) na Sticker (zenye picha zao Sio za Yesu) na kuhubiri Utajiri, Mali na Mafanikio Sio Injili/ Neno la Kristo, huku wakikazia Sana kwà waumini wao lile somo/ kipengele cha SADAKA, unapokaribia ule muda wa kutoa Sadaka mbele za bwana, unafikiri inaleta tija katika vizazi vijavyo katika kuiendeleza/ kuieneza na kuitangaza Injili ya Kristo?
Ni nini mtazamo wako? siku hizi watu hawapewi Neno la Kristo, wanapewa tu Maji, Mafuta, Leso na Sticker wanaambiwa tu watembee navyo, vingine waweke kwenye nyumba zao na magari yao watakua salama na watapata Mafanikio. Kuna tofauti gani na Mganga wa kienyeji ambae anampatia mteja wake hirizi nakumwambia aweke nyumbani kwake na nyingine atembee nayo atapata mafanikio?
Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kusema kuwa, eti hawa Manabii wa sasa wanafungua tu Jicho la Tatu (Third Eye) ndio wanakua na uwezo huo, tayari mtu anajipachika unabii anaanzisha kanisa anapiga noti. Sina hakika na hilo wajuzi wa mambo mnisaidie na hilo kama linaukweli huo.
Turudi kwenye mada
Nimekuwa nikiyafuatilia kwà muda mwingi sana haya Makanisa ya kiroho yanayoongozwa na Manabii kwenye media, ni nadra Sana kuwakuta wakiihubiri Injili na zaidi yake ni Miujiza, Upako na Uponyaji.
Halafu kinacho nifurahishaga huwa hawapendani utawakuta wanapigana vijembe (Nabii "A" ana mponda nibii "B" na nabii "B" anamponda nabii "C" japo wanatumia mafumbo) kila mmoja anawaambia waumini wake kuwa hapa mpo mahali sahihi, kwingine mnatapeliwa.
Sasa Mnajenga nyumba moja mbona mnagombania fito!?
Lingine kuna baadhi hata ya makanisa wameweka mpaka picha zao (Manabii) hukuti picha ya Yesu, Sana Sana watakuwekea alama ya msalaba tu na kuanzia nje hadi ndani ni mabango ya picha yake.
Mtanisamehe kwa nilio wakwaza.
Ni nini mtazamo wako katika vizazi vijavyo, kutakuwa na mafundisho kweli ya kumjua Kristo?