Makanisa ya kinabii na vifaa vya kiroho

Kapyepye Mfyambuzi

JF-Expert Member
Jun 18, 2020
542
918
Habari wadau?

Bila ya kupoteza wakati Naomba twende moja kwà moja kwenye mada kama inavyojieleza hapo juu.
Manabii Wa sasa Ku promote Mafuta, Maji, Chumvi, Leso (vitambaa) na Sticker (zenye picha zao Sio za Yesu) na kuhubiri Utajiri, Mali na Mafanikio Sio Injili/ Neno la Kristo, huku wakikazia Sana kwà waumini wao lile somo/ kipengele cha SADAKA, unapokaribia ule muda wa kutoa Sadaka mbele za bwana, unafikiri inaleta tija katika vizazi vijavyo katika kuiendeleza/ kuieneza na kuitangaza Injili ya Kristo?

Ni nini mtazamo wako? siku hizi watu hawapewi Neno la Kristo, wanapewa tu Maji, Mafuta, Leso na Sticker wanaambiwa tu watembee navyo, vingine waweke kwenye nyumba zao na magari yao watakua salama na watapata Mafanikio. Kuna tofauti gani na Mganga wa kienyeji ambae anampatia mteja wake hirizi nakumwambia aweke nyumbani kwake na nyingine atembee nayo atapata mafanikio?

Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kusema kuwa, eti hawa Manabii wa sasa wanafungua tu Jicho la Tatu (Third Eye) ndio wanakua na uwezo huo, tayari mtu anajipachika unabii anaanzisha kanisa anapiga noti. Sina hakika na hilo wajuzi wa mambo mnisaidie na hilo kama linaukweli huo.

Turudi kwenye mada

Nimekuwa nikiyafuatilia kwà muda mwingi sana haya Makanisa ya kiroho yanayoongozwa na Manabii kwenye media, ni nadra Sana kuwakuta wakiihubiri Injili na zaidi yake ni Miujiza, Upako na Uponyaji.

Halafu kinacho nifurahishaga huwa hawapendani utawakuta wanapigana vijembe (Nabii "A" ana mponda nibii "B" na nabii "B" anamponda nabii "C" japo wanatumia mafumbo) kila mmoja anawaambia waumini wake kuwa hapa mpo mahali sahihi, kwingine mnatapeliwa.

Sasa Mnajenga nyumba moja mbona mnagombania fito!?

Lingine kuna baadhi hata ya makanisa wameweka mpaka picha zao (Manabii) hukuti picha ya Yesu, Sana Sana watakuwekea alama ya msalaba tu na kuanzia nje hadi ndani ni mabango ya picha yake.

Mtanisamehe kwa nilio wakwaza.
Ni nini mtazamo wako katika vizazi vijavyo, kutakuwa na mafundisho kweli ya kumjua Kristo?
 
Wewe amini chako unachokiona sahihi hayo mengine waachie wenyewe ndio maana ya uhuru wa kuabudu.

Si vizuri kuwa mnbeya kwenye masuala ya dini.

Kama chako unakiona kizuri elezea hicho chako tu bila kuponda cha mtu mwingine wao wana hayo wewe una nini je waweza elexea cha imani yako tu bila kuingiza ya imani ya watu wengine? kama huwezi wewe mumbeya tu.
 
Hao ni matapeli tu na hayo makorokoro wanayowauziaga ni ma hirizi na mazindiko yakuwateka akili ili muendelee kupeleka sadaka bila kukoma.

Mimi Mwakasege tu ndio naweza kwenda msikiliza maana yule ni mwinjilisti wa kweli. Hao wanaokuambia wanafufua wafu ni matapeli tu.
Na makotokoro yao wana wafuasi wengi.kuliko wa Mwakasege!

Tena wafuasi wasomi na matajiri sio wajinga wajinga.

Mimi muumini wa Mwamposya nakanyaga sana mafuta na kunywa maji ya upako

Nilikuwa na mitatizo kibao na nilisaidika

Wewe hakijakubana cha kukubana mwenyewe utamkimbia mwinjilisti na kutafuta mtu anayeweza kuondoa hilo tatizo. Ukiwa na magumu huwezi kwenda kwa mwinjilisti hana uwezo huo. Yeye ni kupiga porojo tu
 
Zana za imani zipo.

Kwa waganga kuna tunguli na vingine.

Baadhi ya dini ni biashara.

Na dunia ya sasa mtu anataka kutatuliwa tatizo sio kupata injili
 
"Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo".

Kitabu kitakatifu biblia kimeweka wazi juu ya ujio wa manabii wa uongo.

Injili ya Mathayo inasema 24:4-5 "Yesu akajibu akasema angalieni mtu asiwandangaye kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni kristo nao watadanganyika wengi".
 
Ni hatari sana. Ila fresh walau tuna mitume wetu wa ndani siyo mitume wa wazungu ila shida ni kwamba bado wanamtaja mungu wa israel hapo ndipo nachanganyikiwa.
 
Hakuna matapeli wakubwa kama wale wanaosema waleteni wagoinjwa wataombewa.Yesu hakuagiza wagonjwa waombewe aliagiza waponywe.

Mathayo 10:8​

Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure.

Tatizo la sasa watumishi wengi hawana nguvu za kuponya ni kujitia ohhh tutakuombea !!!

Kwa sasa wako badhi ya Mitume na manabii wako kibao ambao hawaombei wao kazi yao kuponya tu,Na wanajua njia mbali mbali za kuponya mtu ambazo hao matapeli wengine wakina kusema wagonjwa wataombewa hawazijui ndio maana wana mikelele mingi kupinga wanaoponya tofauti na wao ambao husali misala mirefuuuuu yenye mikelele kibao isiyo na matokeo yeyote mtu anaondoka na migonjwa yake
 
Paulo mtume, ameelezea hatari za hao Manabii wa uongo kabisa. Nijuwavyo mimi, Yesu hakuja duniani kuleta uponyaji, wala miujiza;. Hivyo vyote vilishakuwepo tangu enzi za akina Nabii Eliya.
 
Hivi picha ya Yesu inapatikana wapi🤔🤔🤔🤔

Imani kitu kingine buana
Watu kibao wanatokewa na Yesu wanaijua picha yake ndio walichora hiyo picha na ikahakikiwa na waliotokewa na Yesu
 
Habari wadau?

Bila ya kupoteza wakati Naomba twende moja kwà moja kwenye mada kama inavyojieleza hapo juu.
Manabii Wa sasa Ku promote Mafuta, Maji, Chumvi, Leso (vitambaa) na Sticker (zenye picha zao Sio za Yesu) na kuhubiri Utajiri, Mali na Mafanikio Sio Injili/ Neno la Kristo, huku wakikazia Sana kwà waumini wao lile somo/ kipengele cha SADAKA, unapokaribia ule muda wa kutoa Sadaka mbele za bwana, unafikiri inaleta tija katika vizazi vijavyo katika kuiendeleza/ kuieneza na kuitangaza Injili ya Kristo?

Ni nini mtazamo wako? siku hizi watu hawapewi Neno la Kristo, wanapewa tu Maji, Mafuta, Leso na Sticker wanaambiwa tu watembee navyo, vingine waweke kwenye nyumba zao na magari yao watakua salama na watapata Mafanikio. Kuna tofauti gani na Mganga wa kienyeji ambae anampatia mteja wake hirizi nakumwambia aweke nyumbani kwake na nyingine atembee nayo atapata mafanikio?

Kuna jamaa yangu mmoja aliwahi kusema kuwa, eti hawa Manabii wa sasa wanafungua tu Jicho la Tatu (Third Eye) ndio wanakua na uwezo huo, tayari mtu anajipachika unabii anaanzisha kanisa anapiga noti. Sina hakika na hilo wajuzi wa mambo mnisaidie na hilo kama linaukweli huo.

Turudi kwenye mada

Nimekuwa nikiyafuatilia kwà muda mwingi sana haya Makanisa ya kiroho yanayoongozwa na Manabii kwenye media, ni nadra Sana kuwakuta wakiihubiri Injili na zaidi yake ni Miujiza, Upako na Uponyaji.

Halafu kinacho nifurahishaga huwa hawapendani utawakuta wanapigana vijembe (Nabii "A" ana mponda nibii "B" na nabii "B" anamponda nabii "C" japo wanatumia mafumbo) kila mmoja anawaambia waumini wake kuwa hapa mpo mahali sahihi, kwingine mnatapeliwa.

Sasa Mnajenga nyumba moja mbona mnagombania fito!?

Lingine kuna baadhi hata ya makanisa wameweka mpaka picha zao (Manabii) hukuti picha ya Yesu, Sana Sana watakuwekea alama ya msalaba tu na kuanzia nje hadi ndani ni mabango ya picha yake.

Mtanisamehe kwa nilio wakwaza.
Ni nini mtazamo wako katika vizazi vijavyo, kutakuwa na mafundisho kweli ya kumjua Kristo?
Tuombe isije kutokea cku Wakristo wakaamua kuhoji ithibati ya Ukristo wao. Watajuta.

Ukiisoma bibilia mbali ya changamoto ilizonazo za migongano utagundua kuna mengine lukuki yakiibuliwa na hawa Waongoza roho ambayo kwa akili za kawaida tu yanafikirisha kwa mtu aliye na utimamu wa akili
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom