Makanisa na kuunganisha ME na KE..!

Makanisa na kuunganisha ME na KE..!

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,522
Reaction score
14,005
Wadau habari zenu..?
Leo naomba nielezee kwa uchache uzoefu na utafiti wangu wa miaka takribani 7+ kuhusiana na baadhi ya WACHUNGAJI NA WAZEE WA MAKANISA kuhusika moja kwa moja na ukuhadi (kumtongozea) Mara nyingi pindi ikitokea kijana akajiunga na kanisa fulani na akapewa nafasi ya kujitambulisha kuwa yupo Single boy,basi watumishi hao wa bwana huanza kazi ya kutafuta msichana ambaye naye yupo single na kuwakutanisha na kuwaambia huo ni mpango wa Mungu na ni maono kuwa mchumba mwema atatoka ndani ya kanisa lao,pia hujipa utukufu kuwa kama walivyoahidi kuwa ni lazima mchumba apatikane.
Kisha ndoa hufungwa kanisani hapo,lakini mara baada ya maisha ya ndoa kuanza wengi huanza kuona tofauti kubwa ya maisha,kwani inawezekana mume au mke akawa na tabia mbaya ila hawakupata muda mzuri na mrefu wa kuchunguzana na kufahamiana zaidi,majuto huanza mara kesi inarudi kwa mchungaji na mwisho wa yote kuwa ndoa isiyo na furaha na iliyojaa majuo kwani ndoa haiwezwi kuvunjwa zaidi ya kupeana moyo kuwa kwenye ndoa lazima matatizo yawepo ila binafsi naamini haya matatizo yamesababishwa na watu ambao walikuwa wanataka kutengeneza muujiza FEKI. Kama uliwahi kuangalia muvi ya PENINA iliyochezwa na Kanumba utakubaliana nami na ni uhalisia wa maisha halisi ya baadhi ya watu..!! Vijana ambao bado hamjaoa/kuolewa kuweni macho na hili..!
 
Back
Top Bottom