Eng Nyahucho
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 688
- 1,152
MAMA YETU, SAMIAH SULUHU HASSAN (Makamu wa Rais), karibu Tarime, Mara, Tanzania..., lakini kamwe, kamwe...., usikubali kuingia kwenye sakata hili la ardhi inayoporwa, Tarime-vijijini.., waambie hao watu wakueleze vyema, kuna tatizo na mgogoro mkubwa sana kwenye ardhi hiyo.., jiepushe nayo;
Mheshimiwa makamu wa Rais, ardhi hiyo ya Bisarwi, kata ya Manga ina mgogoro, wananchi wamegoma kabisa kutoa ardhi yao kwa mwekezaji kwa njia za 'ujanja-ujanja'.., wananchi wanataka utaratibu wa uwekezaji huo wa kiwanda cha miwa ufuate taratibu zote zikiwepo za maridhiano ya kimsingi kati ya wananchi, halmashauri, serikali na mwekezaji.., sio vinginevyo..
Madiwani wa CCM ambao wengine sio wenye kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Tarime vijijini (wanatoka halmashauri ya mji wa Tarime wilaya) ile kata ya Manga iko halmashauri ya wilaya ya vijijini, kijiji cha Bisarwi.., wananchi wamegoma kabisa, wanataka utaratibu ufuatwe kwenye hilo, kuna mgogoro mkubwa hapo mama yangu, usijihusishe kamwe.., wananchi wanalalamika wanaporwa ardhi yao.., na hata Memorandum of understanding (MoU) imetiwa saini bila maridhiano ya wananchi, halmashauri na mwekezaji.., mheshimiwa Makamu wa Rais wasaidie hao wananchi kwanza, kabla ya kufanya lingine lolote..
Kitu kibaya zaidi.., watumishi wa umma wote leo katika halmashauri ya wilaya vijiji na mji wametakiwa kufika huko Bisarwi kwenye mkutano wako (Makamu wa Rais), hata watumishi wa hospitali ya wilaya wametakiwa kufika huko.., na wameelezwa kwamba kuna daftari la mahudhurio ya watumishi huko kwenye mkutano wako.., inasikitisha sana mheshimiwa Makamu wa Rais.., shughuli nyingi za serikali kuanzia kwenye vitongoji, kata, tarafa hadi wilaya zimesimama.., hakuna watumishi, watumishi
wamelazimishwa kwenda kwenye mkutano wako...,
Mama yangu Samiah, Makamu wetu wa Rais, kwa sababu wananchi wa jimbo la uchaguzi la Tarime-vijijini ambapo huo mradi unatakiwa kujengwa wamegoma kujitokeza kwenye mkutano, uongozi wa CCM wilaya ya Tarime umetoa magari ya kampuni ya Zakaria Express kusomba wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tarime kwenda huko Bisarwi kwenye mkutano wako.., tazama sasa.., namna hawa watu wanavyotamani kujipambanua mbele ya macho yako..., wanakudanganya hadharani mama yetu mpendwa..., mabasi hayo yapo kwenye ofisi ya CCM-Tarime sasa (picha nitaambatanisha)
Pia.., hawa watu wanakudanganya, wamekueleza kwamba unakwenda Tarime-mjini kufungua kiwanda cha chaki, Mama yangu, Mama Samiah, hakuna kiwanda hapo, kuna kiini macho.., tunapafahamu, kuna chumba kimoja cha uzalishaji chaki, kwa hadhi yako mheshimiwa makamu wa Rais haupaswi kamwe kufika kwenye udhalilishaji huo wenye kuitwa kiwanda.., ni chumba kimoja tu cha kutengeneza hizo chaki, tunapafahamu (kwa Rayah)..
Ieleweke vyema, wananchi wa wilaya ya Tarime hawana tatizo na uwekezaji.., wananchi wa Tarime-vijijini wanataka uwekezaji.., lakini wanataka uwekezaji wenye manufaa wenye kufuata taratibu zote za uwekezaji na wenye kuacha alama sio wenye kuzua migogoro baada ya mwekezaji kuanza kazi yake..., Nyamongo (North Mara) ni mfano mzuri sana, hatutaki migogoro sisi wananchi wa Tarime..., mheshimiwa Makamu wa Rais, tazama wananchi kabla ya kuwasikiliza hao wengine.., sauti ya wananchi ndio sahihi, wananchi wa Manga, Bisarwi sio vinginevyo.., kuna tatizo kwenye ardhi hiyo...
Kuna mengi.., lakini haya machache sasa yakufikie huko ulipo mheshimiwa Makamu wetu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu Hassan..., mimi Mwananchi wako wa kawaida.., kwenye mkutano wako wamejaa watu wasiohusika na huo mradi.., pokea taarifa hii..
Martin Maranja Masese [MMM]