Makamu wa Rais mama Samia Suluhu ataka wananchi wanufaike na GEITA GOLD MINE

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Makamu wa rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliwasili Geita jioni ya leo na akakutana na uongozi wa mkoa wa Geita, Inshu ni wananchi wanufaike na mgodi wao wa dhahabu Geita Geita Gold Mine.]
Image00001-1.jpg


Wakati nilipopita kwenye kampeni nilipita kwenye mgodi wa Geita Gold Mine nikaangalia hali ya watu wa Geita nikawa na majonzi makubwa…sikuridhika kuwa na mgodi mkubwa kama ule na hali ya watu wa Geita iko ilivyo hivi nikawa sikuridhika nilikuwa mkali kidogo;- Mama Samia Suluhu

Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado ninamaswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo niyawana Geita Mungu amewaumbia katika aridhi yao; Mama Samia Suluhu

Hatukatai kuwa na wawekezaji wachimbe lakini uchimbaji uwe na faida kote wao wapate na wananchi wapate kwa hiyo hatunabudi kusimamia vizuri na kuhakika kwamba wananchi wa Geita wanafaidika na rasilamali ambayo Mwenyezi Mungu amewapangia;-Mama Samia Suluhu Makamu wa rais
 
Ndiyo jukumu lenu mama mfanye geita gold mine iwanufaishe wananchi!
 
Kazi ya kuwaendeleza wananchi na kuwatoa kwenye lindi la umasikini ni la SERiKALl na wala haitatokea kuwa na muwekezaji labda muruhusu asitoe kodi ili atumaie hiyo kodi kufanya mambo ya kumwendeleza mwananchi.
 
Je serikali ya JPM ina ubavu wa kupitia upya mikataba ya madini na kuifanya yenye faida kwa wenye madini yao?
 
Nyumbu kwa kukosoa kila kitu hawajambo!

Wengine bado wapo mtoni wanakunywa Maji! Ngoja na wao waje!
 
Back
Top Bottom