Makamu wa Rais aongoza Waombolezeji katika mazishi ya Marehemu Jenista Mhagama

Makamu wa Rais aongoza Waombolezeji katika mazishi ya Marehemu Jenista Mhagama

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
261
Reaction score
199
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAKAMU WA RAIS AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MAREHEMU JENISTA MHAGAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza waombolezaji kwenye Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tarehe 16 Desemba 2025.

Akitoa salamu za rambirambi mara baada ya mazishi hayo, Makamu wa Rais amesema marehemu Jenista Mhagama alikuwa mtumishi wa kweli wa watu wake ambaye aliwatumikia na kuwajali.

Amesema Serikali, Wananchi na Chama cha Mapinduzi, wamepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake hautasauhaulika katika nyadhifa mbalimbali ambazo amewahi kutumika.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali na Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuenzi mchango wa marehemu Jenista Mhagana kwa kuendelea kuwa watetezi wa wananchi wa chini, ambapo ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali kuhakikisha wananchi wa hali ya chini ndio wanakuwa kipaumbele chao cha kila siku.

Aidha Makamu wa Rais amewasilisha salamu za shukrani za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa kwa familia na wananchi wa Ruvuma kwa ujumla kutokana na maisha ya marehemu Jenista Mhagama. Amesema Rais Dkt. Samia ameguswa sana na msiba huo kutokana na mchango aliotoa marehemu Jenista Mhagama enzi za uhai wake.

Pia amewashukuru Viongozi wa Kanisa ambao wameshiriki katika Ibada mbalimbali zilizofanyika za kumuombea marehemu Jenista Mhagama kuanzia mkoani Dodoma hadi mkoani Ruvuma.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kumsimamia vema mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili aweze kuendana na kasi iliyotarajiwa. Amesema tayari Serikali ilikwisha kutoa fedha za za ujenzi wa barabara hiyo kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo katika uchumi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu ameishukuru Serikali,Bunge, Mawaziri, Wabunge, familia na wananchi wote kwa kujitoa na kuhakikisha Marehemu Jenista Mhagama anapumzishwa kwa heshima na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
16 Desemba 2025
Ruvuma.

IMG-20251216-WA0079.jpg

IMG-20251216-WA0092.jpg

IMG-20251216-WA0080.jpg

IMG-20251216-WA0091.jpg
 
Inastaajabisha, tupo kwenye kipindi ambacho msiba unakuwa msiba pale mtu mashuhuri akifa, na sio watanzania zaidi ya 10k
 
Malipo ni hapahapa duniani, walidhan waliyofanya tar 29/10 wao hawatakufa, hatimae wamefikiwa sasa.
 
Mila na desturi za makabila mengi zinapotea na kizazi cha miaka ya 1965-75.

Nakumbuka msiba wa baba yake Jokate. Marehemu (Jenista) pamoja na nyadhifa ya uwaziri wakati huo; alivyokuwa anabigirika kwenye udongo na machozi mbele ya camera.

Nilitegemea kumuona na Jokate kujibu Mapigo kwenye msiba wa shangazi yake au hata ndugu na jamaa. Walaah hakuna kujigalalaza tena kwenye udongo.

Mind you I do not promote senseless traditions

R.I.P Jenista (23 July 1967 - 11 December 2025) 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom