Makamu SAUT ataja chanzo cha migomo vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu SAUT ataja chanzo cha migomo vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 18, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Makamu SAUT ataja chanzo cha migomo vyuo vikuu


  Na Moses Mabula, Tabora

  MAKAMU Mkuu wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Dkt. Charles Kitima, amesema kwamba migomo ya wanafunzi inayoendelea katika vyuo mbalimbali hapa nchini inatokana na udhaifu wa uongozi wa serikali iliyopo
  madarakani. Dkt. Kitima alisema hayo jana kwenye Sherehe ya uzinduzi wa Chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Agustino tawi la Tabora. Katika hotuba yake Dkt.Kitima alieleza kuwa migomo hiyo ya wanafunzi pamoja na Wahadhiri vyuoni, inasababishwa na ukiritimba wa viongozi wa Bodi ya Mikopo ambapo fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi, wamekuwa wakizifanya kama zao binafsi Alisema kuwa kiongozi yeyote wa serikali ambaye anaona mwanafunzi hapaswi kupewa
  mkopo huyo hafai na anapaswa kuondoka madarakani vinginevyo nguvu ya umma itamwondoa kwa njia ya kupiga kura.

  “Yoyote asiye thamini elimu ya juu msimchague katika uchaguzi ujao, kumbukeni kwamba watoto wenu wasipopata elimu ya juu familia zenu hazitakuwa na mwelekeo” alisema Dkt. Kitima.

  Alisema kwamba katika mambo ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa na viongozi katika mikakati ya kimaendeleo kupitia Serikali, lazima kuweka elimu mbele, kwa kuwa ndio ufunguo wa maisha kwa kila mtu. Dkt. Kitima, alisema kuwa ili kuwa na taifa la wasomi ni lazima serikali ikubaliane na mfumo uliopo sasa duniani hivyo kusisitiza kwamba mikopo kwa wanafunzi ni lazima itolewe bila masharti yoyote. “Hili sio ombi ni haki yetu ni lazima na wasipotupatia mikopo tujitahidi tuwaondoe madaraka, ili tuweke serikali itakayowahudumia watoto wa masikini na kwamba yeyote anayetaka kuwa rais wa nchi hii, lazima awe mstari wa mbele kuwahudumia watoto wamasikini” alisema Dkt Kitima.

  Nae Waziri wa Ushirikiano waAfrika Mashariki Bw. Samuel Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, alisema kwamba atajitahidi kwa nguvu zake zote kuhakikisha suala la ukiritimba wa mkopo kwa wanafunzi linatoweka. Alisema kuwa tatizo lilipo sasa katika Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi linatokana na ukweli kwamba safu yote inayohusika na mikopo imejaa ubinafsi, undugu na ufisadi na kuongeza kwamba
  ataishauri serikali ikiwezekana Bodi hiyo ivunjwe ili kuondoa kero kwa wanafunzi vyuoni.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Point noted........................CCM lazima wakubali ndiyo chanzo cha migogoro vyuoni kwa kuwa na mfumo mbovu wa kupatikana viongozi...................hakuna uwazi wala fursa sawa kwa jamii yote..............................
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  We've a complete amateur decision makers!
   
 4. I

  Ilonza Senior Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inaonekana Samwel Sitta ni CHADEMA au mnasemaje wadau.km vp dr Slaa amchukulie kadi mapema.
   
Loading...