Makampuni ya simu wanawaibia sana wananchi

vyuku

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
501
225
Makampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania wanawaibia sana wateja wao kwa kuwakata pesa bila ya wao kujijua,kampuni iliyotia fora hasa ni Airtel na voda ambazo ukiweka salio tu wanaiba,tumejaribu kuwasikitikia baadhi ya watu tunaowaelewa wanaofanya kazi ktk kampuni hizo wamekiri ni kweli wanaiba kwa ajili ya kulipia gharama zao za matangazo na udhamini,ukitaka kubaini hilo weka salio kisha wacha usitumie hd siku ya pili kisha angalia salio lako.
 

mbwigule

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
235
195
Ni kweli kabisa. Chama dhaifu (CCM) kimetuzalishia serikali dhaifu, ya wala rushwa, matapeli, mamafia na takataka zinazofanana.
Watanzania wanalilia ukombozi wa pili kutokana na kukwazwa na yanayotendwa na watawala wetu wanaojifanya wafalme.
Ungetazamia nini wakati wanafanya uhalifu huo kweupe bila haya wala soni kwa sababu tu baadhi ya tuliowapa dhamana serikalini ndiyo wenye hisa nono katika makampuni hayo?
Inauma lakini ni lazima tuvumilie hadi ukombozi kamili ipatikane kwani baadhi ya wenye hisa wanaonekana kama ndiyo viongozi mbadala wa tulio nao? Karibu viongozi wote walioko serikalini wana hisa katika makampuni yanayowadhirikisha ili wakwepe majukumu ya kulipa kodi, ndiyo maana hakuna wa kumnyooshea mkono Lowasa anayemiliki hisa katika Vodacom na anayewalinda dhidi ya kulipa kodi. Wapo wengi wakiwemo kina Mwandosya, Maghufuli na wengine kibao. Wengine waliouchuma vyao mapema wameanzisha na Precision Air kwa gharama za kuliua ATC na wapo wakitamba mitaani kama madume ya nyani huku serikali hii hii ya vibaka hawa hawa ikifanya usanii wa kuwapeleka Mahakamani ili kijikosha. Hebu jiulize ni kesi ipi kati ya hizo serikali ilishinda?
CCM ni janga la taifa. Kwa rushwa imemaliza vifaru, tembo, imekausha mito kwa kutoa vibali vya watu kwenda bomoa hata kwenye vyanzo vya mito mikubwa kabisa kama Ruaha Mkuu na kuua maelfu mahospitalini kwa kunyimwa dawa kosa lao tu likiwa kukosa fedha ya rushwa!
Ndiyo maana wanahunyahunya wakijitahidi kutumia kila njia kuuua upinzani. Nasema tena CCM ni janga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom