Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,495
- 37,787
Huduma za upigaji na upokeaji simu zinaendelea kuboreshwa siku hadi siku. Miongoni mwa huduma inayofurahiwa kwa sasa ni ile ya baadhi ya makampuni kuwezesha mteja aliyepigiwa simu ikiwa offline kupata ujumbe kwamba fulani alikutafuta muda fulani. Huduma hii imesaidia katika mambo mengi ikiwemo kuokoa maisha, kuepusha mafumanizi nk.
Huduma nyingine inayofurahiwa ni ile ya kuruhusu simu kuingia wakati mtu anaongea na simu nyingine. Ili kuiboresha huduma hii binafsi naomba iwekwe option ya mtu anayepigiwa simu ya pili kuwa na uwezo wa kukata mawasiliano na anayeongea naye ili apokee simu mpya inayoingia kutokana na umuhimu.
Mfano mtu anaongea habari ya Simba na Yanga ghafla inaingia simu ya Bosi wake, awe na uwezo wa kukata mawasiliano yasiyo ya lazima ili kupokea simu muhimu.