Makampuni ya simu msitutese wateja!!

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
Hivi haya makampuni ya simu haswa tigo na voda yanaona yametushika sana!! hivi ni lini mitandao itatulia kusiwe na kukata kata? Hivi hamjifunzi kwa nchi zilizoendelea ambapo mtandao ukileta shida au kukata kata au upatikanaji wake ukawa dhaifu au kutopatikana kabisa hata kwa lisaa kampuni husika yaweza lipa mabilioni ya pesa?

Bando langu nimeweka kwa pesa yangu kwa nini mnipangie muda wa kuchati au kupiga simu? [HASHTAG]#tusipangiane[/HASHTAG] bana. au mna-play delay game ili kupata faida zaidi huku mkituaminisha kutupa huduma bora na nafuu.

Delay game - unaweka bado dk, MB na sms kwa siku moja inafika wenda jioni masaa matano kabla ya muda wa bando kuisha na ndo umepata nafasi ya kuwasiliana network inakata, sio sms wala cal zinazotoka hapo una salio la bando la kutosha. Network inakata masaa yote yaliyobakia, je hili salio mbona huwa hamrudishi kwa mteja wakati sababu ya kutokutumia bando lote kwa muda husika imeletwa na kampuni yenu? Nachelea kuamini matatizo mengi husababishwa na nyie makusudi na kusingizia kuwa yapo nje ya uwezo wenu au ndo siri za kampuni. Aya bana wacha niishie hapa lakini mmeniboa sana sio mara moja wala mara mbili na nimewapigia sana simu kuwajulisha wanaomba samahani tu utadhani samahani inarudisha gharama niliyotumia kuweka bando.

Mjirekebisheeeeeee aaagh!!!
 
Mkuu makampuni ya mawasiliano yanabana matumizi mpaka kwenye bando... Hali bado tete itabidi tuwazoee tu no way out
 
Jiunge Haliishi au halichachi

Linaweza kumaliza ule mchezo wao wa network kukata kata? Pale unapotaka kuwasiliana na mtu wa muhimu halafu network hakuna au umekubaliana na manzi kukutana sehemu hapajui na anategemea umuelekeze akiwa njiani simu inakata network ukizingatia ni manzi mpya!! hapo ndo panaumiza zaidi but huo ni mfano tu na inaweza kutokea unashida na pesa uko sehemu mbaya na huna njia nyingine zaidi ya kutoa kwenye simu hapo ndo utagundua unapangiwa..
 
Aisee hatari sana..Tafuta mtandao mwingine mkuu
 
Back
Top Bottom