Makampuni ya simu kukomaa na bei mbaya...

Makampuni ya simu kukomaa na bei mbaya...

sulphadoxine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,257
Reaction score
649
Serikali haina meno?


KAMA kuna jambo linalowakera sana Watanzania kiasi cha kuanza kuamini kwamba viongozi wetu ni dhaifu, basi ni kitendo cha Serikali kushidwa kuwa na kauli thabiti au amri inayoweza kusimamiwa na kutekelezwa mara moja kama sheria. Kwanini nasema hivyo, hii inatokana na ukweli kwamba kumekuwepo na rekodi ya matukio ya kushindwa kwa serikali kusimamia utekelezaji wa amri, kauli na maazimio yake yenyewe hata kuwafanya baadhi ya watu wenye utii na sheria za nchi, kuanza kuvunjika moyo na kuamini kwamba huwenda kuna baadhi ya watu na makampuni fulani ndani ya nchi hii, yako juu ya sheria! Mfano;


Wakati wa msukosuko wa kupanda kwa bei ya sukari miezi ya mwanzoni mwa mwaka jana licha ya nchi kuwa na viwanda vya sukari visivyopungua vitano, kulisikika kauli za viongozi kama waziri mwenye dhamana husika pamoja na ile iliyo kuu ya Rais kwamba yoyote atakayepandisha bei ya sukari na kuiuza kwa zaidi ya Shilingi za Kitanzania 1600/= atafungiwa biashara. Pamoja na ukweli wote kwamba kauli ya waziri ama Rais ni amri kuu ya serikali inayopaswa kutekelezwa mara moja, lakini cha ajabu na kushangaza sana bei ya sukari imeendelea kupanda mara dufu na kuuzwa kati ya Shilingi 2,000 na 2,500 kwa kilo sijawahi kusikia kauli zilizotengua msimamo huo.

Bei ya sukari iko juu licha ya uzalishaji mzuri wa viwanda vyetu na vibali vilivyotolewa kwa baadhi ya watu kuagiza bidhaa hiyo toka nje ya nchi! Nafasi haitoshi kuorodhesha na kusimulia matukio ya mifano ya misigano ya kukaidi amri za Serikali kama vile ‘michezo ya kuigiza' kwenye kushuka na kupanda kwa bei za petroli kulingana na bei elekezi za EWURA kwa mujibu wa hali ya soko la dunia , tofauti kubwa ya bei za vifaa vya ujenzi (saruji na mabati ya Tanzania) toka duka moja hadi jingine, kauli zinazotofautiana kwa gharama za kuweka na kununua nguzo za umeme n.k.


Hayo na mengine mengi ni mifano michache ya kuonesha namna ambavyo amri za Serikali zimekuwa zikipuuzwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuamini kwamba kuna madhaifu makubwa katika kusimamia utekelezaji wa amri za serikali, lakini nia ya makala hii ya leo ni kuzungumzia ulegelege wa Serikali kwa gharama za kupiga simu toka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, Januari 30, mwaka huu jijini Dar es salaam, kupitia Mkurugenzi wake, Profesa John Nkoma, ilitangaza kwamba gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja wa simu za mkononi kwenda mwingine nchini, kuanzia Machi Mosi mwaka huu zitashuka kutoka Shilingi 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika moja. Kutolewa kwa kauli hiyo ya Serikali kuliwafanya watu siyo tu kufurahia kupunguziwa gharama kubwa za mawasiliano ya simu za mkononi zilizowafanya wasione tofauti ya kero za bei zile za zamani za simu za TCCL kabla ya ujio wa makampuni ya simu za mkononi, bali pia kuondokana na kadhia ya kulazimika kutembea na rundo la simu (handsets) mfukoni zenye mitandao mbalimbali.


Siku hazikuchelewa ikawadia siku ya siku yaani Machi Mosi, 2013 ambayo ndiyo tarehe rasmi iliyotangazwa na serikali ya kushuka kwa gharama hizo za simu za mkononi kutoka shilingi za Kitanzania 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika moja, lo ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni! Hakuna kilichobadilika, bei ni zilezile, malalamiko ya pesa nyingi kukatwa kila ukipiga simu baada ya saa 12 jioni na kabla ya saa 4 usiku yako palepale! Ndiyo maana wananchi tunapenda kuuliza, hivi kauli hizo za Serikali wakati zinatolewa huwa ni dua ya maombi kwa wahusika ambao wana hiyari ya kutekelezwa au la, ama ni amri thabiti ya serikali ambayo imepitiwa, imetathminiwa na wataalamu na kujiridhisha kabla ya kuitangaza kwa wananchi kama amri? Kwa nini basi inashindikana kusimamiwa na kutekelezwa?


Hebu sikiliza baadhi ya maelezo mengine ya Mkurugenzi huyo wa TCRA kwenye taarifa yake hiyo, anasema kwamba uamuzi huo umefanywa na mamlaka hiyo baada ya kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa mawasiliano ya kampuni za simu za mkononi nchini wa mwaka 2013, pia kuanzia Januari Mosi mwakani gharama hizo zitapungua hadi Shilingi 32.40.

Nkoma anaendelea kusema katika taarifa yake hiyo kwamba ifikapo Januari 2015 gharama hizo zitashuka hadi shilingi 30.58, Januari 2016 zitashuka hadi shilingi 28.57 na Januari 2017 zitakuwa zimeshuka hadi shilingi 26.96 kwa dakika na kwamba uamuzi huo umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2013 sura ya 172. Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwa vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi wa TCRA, John Nkoma, anasema kwamba uamuzi huo utaanza kutumika Machi Mosi mwaka huu kwa mitandao yote ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya uamuzi namba mbili wa mwaka 2007 uliotolewa na mamlaka kufikia kikomo Febrari 28, mwaka huu.


Pamoja na maelezo yote hayo ya serikali, bado inasikitisha kuona makampuni hayo ya simu za mkononi yakizidi kuwakandamiza wananchi kwa bei zilezile kana kwamba hakuna tamko lolote lililotolewa na Serikali kuhusiana na sekta hiyo nyeti ya mawasiliano nchini, hivyo basi Watanzania tunataka kujua kama amri hiyo ya Serikali imekaidiwa kama ile ya mkuu wa nchi ya kushusha bei ya sukari?

Ama ni mimi ndiyo sikumuelewa vizuri Mkurugenzi wa TCRA, maana hata huu ukimya wa Watanzania kuhusiana na taarifa hiyo pia unanitisha sana, kwa sababu licha ya magazeti kuukumbusha umma kwa mara ya pili hapo Machi Mosi mwaka huu kwa vichwa vya habari vingi vilivyosomeka "BEI ZA MAWASILIANO YA SIMU ZA MKONONI, CHINI KUANZIA LEO" bado sijamsikia mtu akihoji kwa nini haoni mabadiliko yanayoashilia kuanza kutekelezwa kwa amri hiyo tangu tarehe 1, Machi? Hapo pia naliona tatizo kwa wananchi ambao kama hawazitambui haki zao watawezaje kuzidai? Huu ukondoo utatuisha lini Watanzania wenzangu? Pamoja na kuzitupa lawama zangu kwa udhaifu wa Serikali katika kusimamia kile inaachokiamuru kutekelezwa, lakini ujinga wa Wananchi kutotambua haki zao unakera mara mbili zaidi kuliko hata huo udhaifu wa serikali.
 
mkuu Na ile sheria iliyopitishwa na bunge Makampuni yote ya simu yawe REGISTRED DSM STOCK EXCHANGE,file limelaliwa ikulu!
 
Gharama ni kubwa pia hata ukipiga simu ndani ya mtandao mmoja wanakata utadhani umepigia mtandao mwingine mfano vodacom kwenda vodacom wanakata sh. 5 kwa sekunde muda wote ambapo ni sawa na sh. 300 kwa dakika. Mimi sielewi hapa inakuaje
 
..Kwa sababu tunakubali vimisaada vyao vya kijinga jinga kama kujengewa choo cha Ofisi ya Kata ndio maana wanafanya wapendavyo!
Na wameishajua U-DHAIFU wetu.
 
ofcoz watanzania bado 2melala! ila najiuliza how can us react coz tukiandamana 2napigwa mabomuu! 2saidiane 2fanyeje?
 
ofcoz watanzania bado 2melala! ila najiuliza how can us react coz tukiandamana 2napigwa mabomuu! 2saidiane 2fanyeje?

Msiseme mnaandamana afande atakuja na mabomu semeni Demonstration hawezi kuja na mabomu atayaacha.
 
TCRA imekuwa kama mbwa koko. Hata heshima ya Prof. Mkomo haionekani. Labda wanapambana na mashambulizi toka kwa wamiliki ta TV baada ya analogi kuzimwa.
 
Serekali yetu imejaa ubabaishaji tu, ki ujumla haina kichwa wala mkia
hakuna haja ya kutangazia uma kuhusu jambo lisilo na uhakika ya nini kukurupuk kama chura? siku hizi watu hulazimika kujiunga na mavitu kama extreme ili kupunguza gharama. kwa ni nihaya makampuni yanatufanyia hivi mara muda huu wapunguze mara muda mwingine waongeze maradufu. WAKOME WAKOMAE!
 
Back
Top Bottom