gadrock
Senior Member
- Oct 7, 2016
- 151
- 103
Habari wana jf,
Leo nimeona niwaeleze kile kinachoendelea upande huu wa research zinaoendeshwa na makambuni binafsi.
Viwanda na makampuni huzalisha bidhaa mbalimbali na kuziingiza sokoni, viwanda hivi hupendelea kujua kama bidhaa zao zinafanya vizuri au vibaya katika soko la ushindani (Market research). Hii huwasaidia kufahamu:
Kwanza makampuni haya hayana wafanyakazi wa kudumu, hivyo huwalazimu kuwaajiri vijana kwa muda ili kufanikisha kazi yenyewe.
Vijana hawa hulipwa ujira mdogo sana yaani kama kampuni/kiwanda kilichotoa tenda hiyo budget yake ni Tshs. 60,000/= kwa siku, na kijana akutane na wateja 10 - 15 kwa siku, makampuni haya huwapa vijana Tshs. 20000/= hadi 30000/= huku kijana akitakiwa kukutana na wateja 20 - 30 kwa siku.

- Ni kwa namna ganni wanazeza kuboresha bidhaa zao.
- Ni wapi hasa bidhaa zao zinahitajika kwa wingi (demand), na ni kwa namna gani wanaweza kukidhi uhitaji huo.
- Inawawezesha kufahamu ushindani uko kwa kiwango gani.
- Pia inawezesha kupunguza uwezekano wa kupata hasara.
Kwanza makampuni haya hayana wafanyakazi wa kudumu, hivyo huwalazimu kuwaajiri vijana kwa muda ili kufanikisha kazi yenyewe.
Vijana hawa hulipwa ujira mdogo sana yaani kama kampuni/kiwanda kilichotoa tenda hiyo budget yake ni Tshs. 60,000/= kwa siku, na kijana akutane na wateja 10 - 15 kwa siku, makampuni haya huwapa vijana Tshs. 20000/= hadi 30000/= huku kijana akitakiwa kukutana na wateja 20 - 30 kwa siku.
- Kitendo hiki kimekuwa na athari kubwa sana kwa makampuni na viwanda mbalimbali hapa nchini, kwani mwisho wa siku wanaletewa tafiti za kupika vyumbani. Hivyo kiwanda kinakosa tathmini ya nini kinaendelea sokoni.
- Makampuni / viwanda vinashindwa kufanya maamuzi sahihi yatakayoendana na hali halisi ya soko.
- Makampuni /viwanda vinapata hasara ambazo zingeweza kuepukika kama wakipata matokeo halisi ya tafiti.