MAKAMPUNI YA KUSAMBAZA GESI KUWENI WABUNIFU

MAKAMPUNI YA KUSAMBAZA GESI KUWENI WABUNIFU

Uta Uta

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2016
Posts
3,742
Reaction score
8,798
Habari wanajamvi?

Nishati ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kwa sisi wa hali ya chini tunatumia zaidi kuni na mkaa kama chanzo cha nishati ya kupikia n.k kwani ndizo zinapatikana kwa bei rahisi, ingawa zina changamoto ya uchafuzi wa mazingira na miti kuisha maporini. Sasa tuna mbadala wa nishati ambapo ni gesi asilia, hii ni nzuri kwani haichafui mazingira ingawa changamoto kubwa ni bei juu hivyo wa kipato kidogo tunashindwa kumudu. Na hasa gharanma kubwa ni pale unaponunua gesi kwa mara ya kwanza, nadhani gharama za kuununua ule mtungi.

Bei ile ya kujazia mara ya pili na kuendelea wengi tunamudu. Sasa ninyi wasambazaji wa gesi kuweni wabunifu badala ya kumtandia libei likubwa mteja kwa mara ya kwanza na wengi hapo ndipo tunaogopa, uzeni gesi tu ghalamaya ya mtungi tulipe kidogo kidogo. Kwa mfano kama gesi ni ths 22,000/ na mtungi ni tsh 30,000/ na kufanya jumla ya tsh 52,000 ambazo mteja anatakiwa azilipe kisu kimoja kwa mara ya kwanza, mnaweza uza tu kwa tsh 25,000/ kwa mteja wa mara zote iwe ya kwanza au ya kumi ina maana 22,000/ gesi na 3000 mtungi, mteja akija jaza mara 10 anakuwa ameshanunua mtungi huku anachekelea na wengi tutamudu kununua gesi na kuacha na kuni na mkaa
 
Bei hiyo mpaka yule bibi Wa msimbati aachie gesi yake aliyoifunika kwenye kile kikombe chake.
 
Niliona Nigeria gesi inauzwa kwa kilo mitaani, unaenda na mtungi,unawekwa kwenye mzani unajaziwa kilo unazohitaji.
 
Habari wanajamvi?
Nishati ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kwa sisi wa hali ya chini tunatumia zaidi kuni na mkaa kama chanzo cha nishati ya kupikia n.k kwani ndizo zinapatikana kwa bei rahisi, ingawa zina changamoto ya uchafuzi wa mazingira na miti kuisha maporini. Sasa tuna mbadala wa nishati ambapo ni gesi asilia, hii ni nzuri kwani haichafui mazingira ingawa changamoto kubwa ni bei juu hivyo wa kipato kidogo tunashindwa kumudu. Na hasa gharanma kubwa ni pale unaponunua gesi kwa mara ya kwanza, nadhani gharama za kuununua ule mtungi,
Bei ile ya kujazia mara ya pili na kuendelea wengi tunamudu. Sasa ninyi wasambazaji wa gesi kuweni wabunifu badala ya kumtandia libei likubwa mteja kwa mara ya kwanza na wengi hapo ndipo tunaogopa, uzeni gesi tu ghalamaya ya mtungi tulipe kidogo kidogo. Kwa mfano kama gesi ni ths 22,000/ na mtungi ni tsh 30,000/ na kufanya jumla ya tsh 52,000 ambazo mteja anatakiwa azilipe kisu kimoja kwa mara ya kwanza, mnaweza uza tu kwa tsh 25,000/ kwa mteja wa mara zote iwe ya kwanza au ya kumi ina maana 22,000/ gesi na 3000 mtungi, mteja akija jaza mara 10 anakuwa ameshanunua mtungi huku anachekelea na wengi tutamudu kununua gesi na kuacha na kuni na mkaa

Ni wazo zuri sana, ila je swala la dhaman yako kwa mfanyabiashaa ya hiyo Gas itakuwa nini.?

Nasema hivyo nikiwa na maana, kuwa nshawahi kufanya hivyo, na wateja wakawa hawarudishi marejesho, huku wakihama hata sehemu yao waliyozoea kununulia. Wengine walikuwa wanahama hata nyumba. Baada ya hapo humpati tena.
 
Mitungi kupigwa chapa maalum kabla hujamaliza,ili ukikimbia usihudumiwe popote kujaza gezi,mtungi wako uwe useless.
 
Back
Top Bottom