Makame anashauri Polepole angemuiga Dr. Mpango kujiuzuru

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,039
Mgombea mwenza wa urais kupitia chama cha ADA TADEA, Ally Makame, amesema kuwa hatua ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kujiuzulu hadharani ililenga kuleta mvutano kati ya wananchi na serikali.

Your browser is not able to display this video.


Soma pia: Ndugai, Majaliwa na Mpango wamepigwa bao na Polepole
Akizungumza katika kipindi cha Maswali na Majibu kinachorushwa na Jambo TV, Makame amejibu swali kuhusu sakata la Polepole kwa kutolea mfano namna ambavyo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango alivyoandika barua ya kujiuzulu.

Makame amesema Polepole anajua vyema utaratibu wa kujiuzulu kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma, lakini aliamua kuvunja taratibu hizo kwa makusudi na kuweka barua mtandaoni, akiamini kufanya hivyo kutamletea umaarufu wa kisiasa.

Chanzo: Jambo tv
 
Huyo Ana***mbwa Sio Bure,
Anaacha Kuzungumzia Sera Zake Ili Achaguliwe Anawatetea Mbogambog
Hivi Ndio Vyama Vya Mifukoni Na Madhara Yake Ndio Haya,upinzani Unaonekana Hauna Maana.
 
Mtu wa TADEA anaongelea mambo ya ccm wapi na wapi? Wapinzani aina hii ccm B ndio wanachelewesha mabadiliko maana awajulikani rangi zao halisi.
 
Reactions: K11
Hilo zee Makame nalo punga tu, mambo ya CCM yeye yanamhusu nini.
 
Reactions: K11
Ndio maana tunasema kuwa hivi vyama pinzani vidogo vidogo ni vyama vya mfuko wa CCM
 
Mtu wa TADEA anaongelea mambo ya ccm wapi na wapi? Wapinzani aina hii ccm B ndio wanachelewesha mabadiliko maana awajulikani rangi zao halisi.
Kwanini msiwashughulikie ?
 
Polepole ametumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu.

Kama unaona amesema kitu fulani si sawa, mpinge kwa hoja, usipinge haki yake ya kikatiba na kibinadamu ya kutoa hoja.
 

Huyu ni mwenzetu eee
 
Dr. Mpango hajajiuzulu bali ameamua kustaafu muhula huu ukiisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…