Inawezekana Makamaba anajikosha, lakini mimi naona mbali zaidi ya hapo.
Siasa ni mchezo wa ushindani na bahati mbaya ni mchezo mchafu. Lakini kama mchezo wowote, kunakuwa na ushindani. Mchezaji mzuri na anayeheshimika ni yule anayekubali "kushinda na kushindwa".
Tunamwona Makamba anajikosha kwa sababu Watanzania bado hatujakua kidemokrasia kiasi cha kukubali kushindwa, kwa hivyo anapotokea mmoja akakubali anaonekana "ametoka sayari nyengine". Ikiwa Makamba kayasema haya kwa dhati yake ninampongeza, ndio ukomavu wa kidemokrasia huo.