Makamba, Membe, Bashiru....

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Hawa ndo watakaotaga yai la mgawanyiko CCM kama wasipokuwa makini na kauli zao za kwenye vyombo vya habari.
Mwl Nyerere alisema anayetaka kubebwa kama mgonjwa au maiti aachwe abebwe tu kama wabebaji wapo tayari kubeba kwa hiari Yao.

CCM ya sasa inapendwa sana kila kona Tanzania, kama hii ni kweli basi hakuna haia ya kuhangaika na wanaotangaza nia ambao hesabu zinaonyesha kuwa hawatapata watakao waunga mkono.

Hofu ya nini?
 
Sasa kwani ilikuwa lazima uanzishe thread? Sijaona chochote chenye kustahili kuanzisha thread kwenye maandishi yako.
 
analysis yangu ndogo sana ya kijana wenu ni kuwa Membe hamaanishi kugombea 2020;

ila kuna mtu katika kambi yake ndie anayemtengenezea njia kwa 2025.
 
Sasa kwani ilikuwa lazima uanzishe thread? Sijaona chochote chenye kustahili kuanzisha thread kwenye maandishi yako.
We we unatamani watu wote wawe kimya kwenye mambo fulanifulani. Hii sio sawa, kama huoni kitu sio wote wana makengeza.
 

Ni kweli
 
Kwa analysis yangu dhaifu, Makamba ni janga la Taifa
 
Ccm na Jiwe wote hawapendwi ,ili kaeni mkijua kabisa ,yaani MTU anayevunjia watu nyumba kwa sababu yoyote ile hawezi kupendwa ,mtu anayefukuza wafanyakazi kwa sababu yoyote ile iwe darasa la saba au vyeti feki ,hawezi kupendwa maana nao ni binadamu na wana haki zao , MTU anayekataa kuongeza mshahara na madaraja ya watumishi hawezi kupendwa ,MTU anayenyima mikopo wanafunzi wa elimu ya juu hawezi kupendwa ,MTU anayepunguza mzunguko wa fedha hawezi kupendwa , MTU anayefungulia watu kesi za uhujumu uchumi kwa visasi hawezi pendwa ,MTU anayetoa kauli za ajabu kama ile ya wahanga wa tetemeko hawezi pendwa ,MTU anayeteua watumishi wa umma wasio na vigezo hawezi pendwa , MTU ambaye hakemei mauaji na watu kufungwa kwenye viroba hawezi pendwa ,MTU anayefunga wanasiasa kisa wamemkosoa hawezi pendwa ,MTU anayekiuka haki za binadamu na uraia hawezi pendwa ,yako mengi sana yanayofanya asipendwe hata afanyaje hapendwi tena kwa kujitakia mwenyewe .
 
ilifika wakati nikafikiri kuwa na PhD unakuwa huna akili, SASA nakaribia kuthibitisha by counterexamples

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…