Makamba: Lowassa ni mroho wa madaraka

Makamba: Lowassa ni mroho wa madaraka

kinachomhangaisha january makamba ni cheo alichohaidiwa na maghufuli na sio kingine.
 
Magufuli anatumia mamilioni kulipa wasanii ili kubadirisha upepo wa kampeni kuwa fiesta,kwa sababu anaogopa aibu y kukosa watu. Ni sheeeeeda

mpumbavu utamjua tu ni msanii gan kanunuliwa na lowassa ??

ccm imekuwa ni genge la matapeli watumiao wasanii kusaka kura
 
Wewe tena ndio mroho kupindukia una haraka ya maisha baba yako kashindwa sifa huna zaidi ya kubebwa mitihani tanga ukiiba ukafukuzwa shule
 
kama Makamba wewe hauna uroho wa madaraka kwa nini usiache kugombea Ubunge?.
 
hata ww makamba n mroho wa madaraka pamoja na ccm yako, ongeleeni sera zenu acheni majungu na mipasho..
 
Wote Makamba na wanaye in waroho Wa madaraka haiwezekani family nzima ipo kwenye uongozi ndani ya chama
 
Jan Makamba nani ndani ya CCM asiye kuwa na uroho wa Madaraka?
 
matusi hayana tija km huwez andika ustarabu acha hatujazoea matusi humu
 
Makambaaa!!! Kweli we ni January!!mwaka ulikuwa haujapata mwelekeo.
 
Babako anakudanganya chama siyo chenu alikuwa kaajiliwa tu jamani!!!
 
Aliyekuwa mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.

Makamba alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. January alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.

“Yale siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika madaraka ya kuongoza nchi,” alisema Makamba.

Alisema kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.

Hata hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.

Alisema CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida katika maendeleo.

Kwa upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema lazima ataipelekea Dodoma hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo yamekuwa yakisemwa kama hisani.

Mavunde aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.

Chanzo: Mwananchi

Chadema kama kweli wanataka mabadiliko wangeganya fair election kumpata mgombea wa urais
lakin uhuni wa yule dj maarufu aitwaye mbowe ndio ulitawala pale kwenye mchakato

Pili
kama chadema wanataka mabafiliko waanze na katiba yao wenyewe isiyofuata misingi ya kidemokrasia na inayopingana na katiba ya nchi(Article 107A) inayoipa mamlaka mahakama kutoa uamuzi wa mwsho katika kutoa haki lakin katiba ya chadema ukishtak chama mahakaman umekwenda maji
Muulize zito kabwe
 
Makamba unatia aibu kijana.kama wewe siyo mroho wa madaraka kwanini ulimuwekea mwanzako pingapizi? Ulitaka uendelee na ubunge wako kwa kuwa wewe ni mroho wa madaraka au kutumiza ndoto
ulizonazo?
Lowassa siyo mroho wa madaraka ila amewapa presha ndio maana mnamwita mroho wa madaraka.angekuwa mroho wa madaraka watu wasinge mkimbilia hata kidogo.
If you have nothing to speak you better shut up

Mtu akikiuka sheria lazima awekewe pingamiz
na pingamiz sio uroho wa madaraka
 
Kumbe demokrasia kwenu ni kubakia kuikubali CCM milele hata kama ukijitambua kuwa ni chama cha familia isiyokuhitaji wala kukuthamini

Familia gan ya mtei na mbowe?
 
Back
Top Bottom