Makamba: Lowassa ni mroho wa madaraka

Makamba: Lowassa ni mroho wa madaraka

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
Aliyekuwa mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.

Makamba alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. January alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.

"Yale siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika madaraka ya kuongoza nchi," alisema Makamba.

Alisema kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.

Hata hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.

Alisema CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida katika maendeleo.

Kwa upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema lazima ataipelekea Dodoma hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo yamekuwa yakisemwa kama hisani.

Mavunde aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.

Chanzo: Mwananchi
 
NI HAKI YA MTU AWAYE YOYOTE KUFANYA MAAMUZI MADHARI HAYUPO TENA CHINI YA WAZAZI/
NI UAMUZI WA MTU BINAFSI!
KUHAMA CHAMA SI DHAMBI!
KWANI WOTE LENGO LAO NI MOJA TU,
**KUMTUMIKIA MTANZANIA**
ii
 
NI HAKI YA MTU AWAYE YOYOTE KUFANYA MAAMUZI MADHARI HAYUPO TENA CHINI YA WAZAZI/
NI UAMUZI WA MTU BINAFSI!
KUHAMA CHAMA SI DHAMBI!
KWANI WOTE LENGO LAO NI MOJA TU,
**KUMTUMIKIA MTANZANIA**
ii

Mmh!!! Wengi wao wapo kwa ajili ya kuyatumikia MATUMBO yao na FAMILIA zao tu nyinyi kama mtaweza mpande maboti mkazame LIBYAAA....
 
Sina hakika sana kama Makamba hajui UKAWA ni mwavuli tu na Lowassa kagombea kwa tiketi ya CHADEMA. ananishangaza anaposema sera za Lowassa ni za CCM na zile za babu Duni ni za CUF!!! Makamba anajaribu kuuhadaa umma wa Tanzania na bado anaendeleza kiburi walichonacho wengine cha kwamba hata iweje hawatakuja kushika madaraka ya nchi hii, kwani nchi hii ya CCM au ya familia fulani fulani na sio watanzania? kuna wakati ni vizuri tukatambua nafasi zetu kama vijana na viongozi ambao taifa linatutegemea kujiepusha na kauli ambazo kesho na keshokutwa zitabaki kuwa msalaba wa ustawi na utimilifu wa ndoto zetu. mh Makamba ni vizuri ukajua Tanzania ni nchi na ina wenyewe ambao kwa pamoja tunaitwa Watanzania
 
Makamba the son of Makamba, Kamba hizo, malofa hawafunguki na Makamba.
 
chadema NI taasisi! yenye viongozi thabiti!
-->>CHAMA KINA TARATIBU ZAKE CHINI YA KATIBU MKUU NDG.WP SLAA,
------>>>YEYOTE AINGIAYE YUPO CHINI YA TARATIBU HIZI,APENDE ASIPENDE!
 
Makamba unatia aibu kijana.kama wewe siyo mroho wa madaraka kwanini ulimuwekea mwanzako pingapizi? Ulitaka uendelee na ubunge wako kwa kuwa wewe ni mroho wa madaraka au kutumiza ndoto
ulizonazo?
Lowassa siyo mroho wa madaraka ila amewapa presha ndio maana mnamwita mroho wa madaraka.angekuwa mroho wa madaraka watu wasinge mkimbilia hata kidogo.
If you have nothing to speak you better shut up
 
Neno Ukawa litakua historia!
 
TULIKUPENDA SANA KUMBE UKO HIVYO UTATUSAMEHE:

Tulimpenda sana, Lowasa na tukamshangilia sana akiwa ccm hatukujua kumbe ni mpenda madaraka hv tena kwa gharama yoyote ile hata kwa wizi ilimradi tu uingie Ikulu nasema NO UTATUSAMEHE HAPA KAZI TU
 
na huyo MAGUFULI kampeni anazopiga kwa gharama zote hizo ni ili aingie wapi!! Chooni au!!??
 
tulikupenda sana kumbe uko hivyo utatusamehe:

Tulimpenda sana, lowasa na tukamshangilia sana akiwa ccm hatukujua kumbe ni mpenda madaraka hv tena kwa gharama yoyote ile hata kwa wizi ilimradi tu uingie ikulu nasema no utatusamehe hapa kazi tu

W ewe na nani mwingingine wenye akili mbovu kama yako?
 
TULIKUPENDA SANA KUMBE UKO HIVYO UTATUSAMEHE:

Tulimpenda sana, Lowasa na tukamshangilia sana akiwa ccm hatukujua kumbe ni mpenda madaraka hv tena kwa gharama yoyote ile hata kwa wizi ilimradi tu uingie Ikulu nasema NO UTATUSAMEHE HAPA KAZI TU

unasubili uambiwe ndo ujue.
 
Back
Top Bottom