Makamba kwanini unamwangusha Rais, kwa hili la uchafu huoni unastahili kujiuzulu?

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Ikumbukwe kuwa toka mheshimiwa rais ameingia madarakani, amekuwa akisisitiza sana suala la usafi hasa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu uliokuwa tishio kwa nchi yetu.
Nakumbuka mheshimiwa rais alidiriki kutenga siku ya uhuru kuwa siku ya kufanya usafi.

Jambo la kushangaza ni kwamba bado usafi hauridhishi katika maeneo mengi ya nchi yetu na hasa katika jiji la letu la Dar es salaam ambalo kwa kiasi kikubwa ndilo linabeba sura halisi ya nchi yetu.

Kilichonisukuma kuanzisha uzi huu ni Maji machafu, meusi, yenye harufu mbaya na kali yanayotiririka katika pembezoni mwa barabara ya Warioba.
Maji haya yanasemekana yanatoka viwandani na yanatiririka kupitia mitaro iliyo pambizoni mwa barabara hii.

Yamekuwa yanasababisha kero kubwa kwa wapita njia hasa sisi watembea kwa miguu kwani harufu yake ni kali sana.

Nilitarajia siku ya mazingira duaniani ingekuwa ni chachu ya kuboresha mazingira yetu na kuyafanya rafiki kwa binadamu. Lakini tumeishia kutumia siku hii kutoa matamko ya siasa yasiyotekelezwa! Ifike mahali tufanye kazi kazi kama serikali inavyohubiri dhana ya Hapa Kazi Tu.

Sasa kutokana na kuonesha wazi kushindwa kushughulikia suala hili la usafi kikamilifu pamoja na kutoa matamko ambayo mpaka sasa hayajatekelezwa, Mheshimiwa Makamba huoni sasa ni wakati wa kuachia ngazi ili wengine wachukue nafasi hiyo na kutatua matatizo yetu wananchi?

taka1.jpg
taka2.jpg
taka4.jpg
taka 6.jpg


Kuna Kipindi Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais anaeshughulikia Mazingira Mh. Luhaga Mpina alitoa siku saba kwa Baraza la hifadhi ya mazingira nchini NEMC, Mamlaka ya Maji safi na maji taka DAWASA, kuhakikisha wanachukua hatua kwa viwanda vinavyotiririsha maji machafu katika mifereji inayopita maji ya mvua.

Kauli hiyo ya Mh. Mpina aliitoa jijini Dar es salaam mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la TPDC Mikocheni na mtaa wa kwa warioba ambapo aliweza kubaini kuwepo kwa viwanda vinavyotumia mifereji ya kupitishia maji ya mvua kuitumia mifereji hiyo kwa kupitishia maji machafu yanayotoka viwandani.

"Na hawa watu wengine wenye makampuni na wenye viwanda hakikisheni mamlaka husika zinafuatilia hili suala kwa kipindi cha wiki mbili na baada ya hapa nitarudi kuja kuangalia kama tatizo hili bado linaendelea" alisema Mpina

Alisema hali hiyo haiwezi kufumbiwa macho kwakuwa madhara yake ni makubwa kwa wakazi waishio maeneo ya karibu na mifereji hiyo ikiwemo kuongeza kasi ya milipuko ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu. Lakini tangu kipindi hicho hakuna kilichoendelea. Hii inamanisha Mawaziri wa Magufuli Wanadharauliwa sana. Lakini tangu aseme hivyo hajawarudi wala hawa NEMC hawajafanya chochote.

Unajua hizi Ofisi za NEMC zipo mikocheni, na huyu Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira NEMC Dr Robert Ntakamulenga, anapita Hii barabara ya Warioba Kila siku asubuhi na jioni, maji machafu anayaona. Hamna chochote kinachofanywa. Haya maji yananuka sana.

Hii ni dharau kwa viongozi waliopo Madarakani. Hawa wakina Makamba kama wameshindwa kuwachukulia hatua NEMC, basi wajitumbue wenyewe ili apatikane mtu mwajibikaji. Haiwezekani uwape watu muda wa kufanya kazi na wasipofanya unaendelea kuwachekea, namna hiyo hii nchi haiwezi kufika.

Rais Magufuli nakuomba Uwatumbue hawa Mawaziri kwani wanakuangusha.
 
Tangu yule blogger amuumbue,February ni kama hayupo serikalini.Nadhani anatamani kupost malalamiko kama raia wengine.
 
Miji mingi imekithiri kwa uchafu na hakuna initiative za kufanya mambo yawe tofauti.
 
Mie naona hilo agizo la mh..kuhusu kufanya usafi kila jmos ya mwisho wa mwezi halitekelezeki mfano hai ...ni huku mkoani hususan mkoa wa rukwa manispaa ya sumbawanga ...mji ni mchafu mno..usafi haufanyiki mji unanuka balaa...
 
Makamba mtoto wa mjini utampaje wizara kama hiyo jiulize mbona makamu wake ndiye upiga kazi ?
 
Kuna Kipindi Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais anaeshughulikia Mazingira Mh. Luhaga Mpina alitoa siku saba kwa Baraza la hifadhi ya mazingira nchini NEMC, Mamlaka ya Maji safi na Maji taka DAWASA, kuhakikisha wanachukua hatua kwa viwanda vinavyotiririsha maji machafu katika mifereji inayopita maji ya mvua.

Kauli hiyo ya Mh. Mpina aliitoa jijini Dar es salaam mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la TPDC Mikocheni na mtaa wa kwa warioba ambapo aliweza kubaini kuwepo kwa viwanda vinavyotumia mifereji ya kupitishia maji ya mvua kuitumia mifereji hiyo kwa kupitishia maji machafu yanayotoka viwandani.

"Na hawa watu wengine wenye makampuni na wenye viwanda hakikisheni mamlaka husika zinafuatilia hili suala kwa kipindi cha wiki mbili na baada ya hapa nitarudi kuja kuangalia kama tatizo hili bado linaendelea" alisema Mpina

Alisema hali hiyo haiwezi kufumbiwa macho kwakuwa madhara yake ni makubwa kwa wakazi waishio maeneo ya karibu na mifereji hiyo ikiwemo kuongeza kasi ya milipuko ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu. Lakini tangu kipindi hicho hakuna kilichoendelea. Hii inamanisha Mawaziri wa Magufuli Wanadharauliwa sana.Lakini tangu aseme hivyo hajarudi wala hawa NEMC hawajafanya chochote.

Unajua hizi Ofisi za NEMC zipo mikocheni. Na huyu Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa mazingira NEMC Dr Robert Ntakamulenga, anapita Hii barabara ya Warioba Kila siku asubuhi na jioni, maji machafu anayaona. Hamna chochote kinachofanywa. Haya maji yananuka sana.

Hii ni dharau kwa viongozi waliopo Madarakani. Hawa wakina Makamba kama wameshindwa kuwachukulia hatua NEMC, basi wajitumbue wenyewe ili apatikane mtu mwajibikaji. Haiwezekani uwape watu muda wa kufanya kazi na wasipofanya unaendelea kuwachekea, namna hiyo hii nchi haiwezi kufika.

Rais Magufuli nakuomba Uwatumbue hawa Mawaziri kwani wanakuangusha.
 
Haya maji yananuka...tena walikuwa wanayachuja lakini tangu hii wiki ianze yanatiririshwa meusiii tena yenye harufu kali. Haya maji yanapita mbele ya nyumba ya mama Ritha Mlaki, kweli mama hawezi mek a phone call akatumia influence kustop huu uchafu? Au kujuana ni kwenye kuombea watoto kazi tu?

Mama Samiah unasali ule msikiti pale mara nyingi tu, kweli maji huyaoni au magari yako ni tinted hadi kwa ndani?
Niishie hapa.
 
wakati tunamlaumu Makamba kuhusu swala ia uchafu na sisi tumejipangaje katika kukabiliana na swala hilo katika maeneo yetu?
 
Mkuu kirerenya afadhali umeandika huu uzi, jamani imekuwa kero katika huu mtaa hapa yani mimi ndio njia yangu napitaga hapa, harufu ya haya maji yananuka balaa halafu kuna mama fulani anapiga chakula kando ya hayo maji na watu wanakula, jamani wahusika lifanyieni kazi hili suala hili haraka...

Hii njia ndio vigogo wengi wanapita hapa...aibuuu hata nyinyi viongozi...mnafunika mcho...
 
Back
Top Bottom