Kinachosumbua nchi yetu ni kukosekana kwa ideology. Hii kukazania uburebure na wakati mwingine kuitaka serikali kuondoa kodi kwenye bidhaa/huduma ni matunda ya utupu huu wa ideology. Suala hapa si kutoa elimu bure ( nina hakika itagharamiwa kwa namna moja au ingine), bali kuhakikisha elimu bora kwa vijana wetu na kuwawezesha kubadilisha maisha yao katika mazingira ya sasa. Tusije tukarudi kulekule tuliko sasa ambapo tunahesabu maendeleo ya elimu kwa kuhesabu vyumba vya madarasa, idadi ya secondary/ shule tulizojenga badala ya kuangalia zao la elimu tunayotoa! Tusifike kuhesabu watoto wanaomaliza sekondari bure hata kama hawana elimu sahihi!