Makamba Hajatulia! - Warioba

Wapo watakaowaamini
 
Makamba asipojiuzulu basi karogwa au ana ugonjwa wa uduvi!

Hivi kweli kwa jinsi hali ilivyo sasa hivi tunategemea Makamba ajiuzulu wakati ndiye anayewakingia kifua mafisadi ndani ya CCM.Sio rahisi Makamba kujiuzulu kwa sababu waliomchagua wanafurahia utendaji wake.

Mabadiliko yatatokea pale tuu wanaCCM wataamua kufanya mabadiliko ndani ya chama chao ili kuendoa fedheha,wasipofanya mabadiliko ya dhati ndani ya uongozi uliopo sasa tena katika ngazi zote hakika CCM itakua historia baada ya muda sio mrefu ujao.
 
😱 Hapo kwenye Nyekundu unamaanisha JK au? maana najua Katibu Mkuu hachaguliwi bali anateuliwa!
 

Mkuu nakubaliana na wewe asilimia mia moja hakuna kurudi nyuma,sio JK au Makamba wote hawafai.
 

Sio sula la kuwaamini sio hoja, hoja ya msingi hapa ni kwamba kuna ombwe la uongozi na katika hili hakuna ubishi.Kama ni hivyo yoyote atakayepatikana mwenye kuonyesha uwezo zaidi ya JK atakubalika hata kama hatakuwa kiongozi bora sana.

Inasikitisha kuona Tanzania kama nchi mfumo wetu wa kupata viongozi umechakaa baada tu ya awamu hii ya nne kuingia madarakani,huu ni wakati muafaka sasa kuandaa mfumo mpya utakao toa viongozi wanaofaa kuliongoza taifa katika wakati huu tulio nao sasa.
 

Jaji Joseph warioba ni mtu mwenye hekima, nafikiri amesema ujumla wa jambo zima, kama wewe ndiyo unamteua mtu akufanyie kazi yako na unamwamini sana, na wengine wakasema ni bogas sasa sijui wewe uliomchangua inakuwaje? nafikiri mmemwelewa ingawa hakufafanua ki uwazi.
 

Hapa wazee ambao hawajatulia wakiwa kwenye send off ya Bintiwe Edo

From Michu
 

Rais alishatamka kwamba urais wake hauna ubia kwa hiyo hatutegemei kwamba aliweza kupangiwa viongozi na hana uwezo wa kuwaondoa. Tukubaliane tu kwamba hataki kufanya hivyo kwa sababu zake mwenyewe binafsi.
 

Hapa si suala la mapambano kati ya nani na nani. Hapa kuna suala zito la mustakabali wa nchi na namna ya kunusuru wananchi wasio na hatia wasije wakapata shida huko baadaye kutokana na viburi na mvutano wa viongozi wanaoangalia maslahi binafsi badala ya kuangalia maslahi ya umma wa Watanzania waliowaweka madarakani.

Mwalimu Nyerere at one point was being counted as a 'lost generation' as you put it, lakini hivi leo Wananchi wanajaa matumaini wakilisikia jina lake likitajwa tu. For your information people of all walks of life are queing to congratulate the "lost generation" for their courageous move of starting to 'bell the cat'!!! Kalaga baho!

Alisema mtu mmoja kwamba misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili ndiyo inayofanya wananchi waendelee kuwa wavumilivu. I agree with him totally.
 

Mkuu FMEs,
Warioba na Wazee wenzake ambao 'wanazunguka mbuyu' sidhani kwamba hawaelewi wanachokifanya, wamekomaa hawa, wanajua waseme nini na wakati gani.

Kama umeona Mzee Warioba amenukuu aliyosema Rais na Waziri Mkuu na kuyafananisha na yale waliyoyasema wao kwenye Kongamano lile kuonyesha kwamba hayana tofauti. Kwa hiyo, ni lipi lililofanya Rais achomekee kwamba anajua maneno mazuri yasingaliweza kutoka kwa hilo genge la Warioba na wazee wenziwe na kwamba kuna chuki binafsi? Maneno ya Rais yanashabihiana na ya Makamba alichoacha kusema Rais ni neno 'wehu'! Yupi mnafiki hapo?

Tusingelitegemea mtu mwenye busara, uelewa na uzoefu wa kisiasa kama Mzee Warioba akatamka moja kwa moja kwamba 'Rais mbona una'tafuna' maneno yako mwenyewe'? Kwa upande mwingine Warioba alikuwa anatoa ujumbe kwamba tunajua kinachoendelea lakini kwa kuwa tunaipenda sana nchi yetu hatutaki kuiingiza nchi kwenye majibizano miongoni kwa viongozi yatakayozidi kuleta mtafaruku. Kwa maoni yangu amempa ujumbe Rais kwamba wao kama Wazee wa nchi hii wanamheshimu kwa hiyo yeye naye anapaswa kufanya hivyo.

Watu wazima wenye akili timamu huwa hawatoboi wala hawapashani mipasho lakini ujumbe hufika kwa namna wanavyotoa kauli zao. Hiyo inaitwa BUSARA!
 

Mkuu nafikiri unakuwa unfair kwa watoto wa makamba, na si kweli mtoto wa kike anachukua tabia ya mama na mtoto wa kiume anachukua tabia ya baba. Watanzania wengi sana tunakuwa so bias kuhusu watoto wa wakubwa, tunawajudge without any evidence. Ingekuwa vinzuri tukaanza kuangalia watu kama individual not mtoto wa nani.
 


Well said Bluray!! Nimebonyeza button ya senksi.
 
mimi hata simshangai huyu bwana..............HE LOOKS MORE LIKE A WITCHDOCTOR than a Secretary General....by the way,ajaribu kuangalia maisha na nafasi yake afta a year...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…