Makamba Hajatulia! - Warioba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba Hajatulia! - Warioba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Dec 10, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Swali: Baada ya kongamano la kumbukumbu ya miaka 10 ya Mwalimu Nyerere, baadhi ya viongozi wamelaani majadiliano, na hata kuwaita majina mabaya baadhi ya washiriki. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba alikwenda mbali zaidi kwa kuwaita wehu. Uliyapokeaje maoni hayo?

  Jibu: Sisi tumesikia matusi aliyotoa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, lakini hayatunyimi usingizi. Makamba si Waziri Mkuu wa Rais (Jakaya) Kikwete, lakini inaonekana anatumia muda mrefu sana kuzungumzia mambo ya Serikali badala ya kujishughulisha na mambo ya chama.

  Kwa muda sasa, kumetokea maneno ya kubeza, kukejeli, matusi kila baadhi yetu tunapozungumzia mambo ya msingi ya kitaifa na hayo yametokea, yamesemwa kutoka Makao Makuu ya Chama, si kutoka serikalini.

  Oktoba, ninyi waandishi wa habari mlituhoji mimi na Salim (DK. Salim Ahmed Salim) ili tutoe maoni yetu kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 10 tangu Mwalimu alipotutoka.

  Baada ya kusema tuliyosema alitokea mtu makao makuu ya chama akatutukana. Hakushughulika na hoja tulizotoa, sisi tulizungumzia mambo mawili makubwa.

  Moja, ni kuporomoka kwa maadili katika Taifa letu, la pili mmomonyoko kwenye umoja wa Taifa, lakini tulitukanwa kwamba sisi ni watu tunaomwandama Rais Kikwete.

  Lakini mwezi huo huo, Rais Kikwete akahutubia Taifa kutokea Butiama akazungumzia mambo yale tuliyozungumza tena kwa ufasaha zaidi kuonyesha kwamba ni matatizo kwenye nchi.

  Alizungumzia kuporomoka kwa maadili, hatari inayoonekana kwenye kusambaratika kwa umoja wetu. Alizungumzia rushwa, akazungumzia ufisadi. Ni yale yale tuliyokuwa tumeyasema. Tulifarijika, tukapumua tukaona kumbe Rais wetu anaelewa haya matatizo.

  Sasa wakati ule tumetukanwa kulikuwa na reaction ya watu mbalimbali baadhi walituambia kwamba yule kijana aliyesema alikuwa ametumwa na Makamba ili atutukane, sisi hatukuamini.

  Kwa sababu ni huyo huyo alikuwa amesema maneno kama hayo huko nyuma sasa tukaambiwa amekuwa anatumwa, hatukuamini.

  Sasa imekuja hii. Wote waliokuwa kwenye kongamano wanajua yaliyozungumzwa na katika majumuisho hayo inaonyesha yaliyozungumzwa ni mambo ya msingi na yamezungumzwa na watu wengi pale, tena kwa makini kabisa, na utaona katika majumuisho kuna sehemu nyingi wanatambua juhudi za Serikali.

  Kongamano limetambua juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya madini, lakini wametoa ushauri namna ya kuboresha zaidi. Wametambua juhudi za Serikali kuhusu umiliki wa ardhi, lakini wamesema juhudi zaidi zinahitajika. Wametambua juhudi za Serikali katika kuboresha elimu, lakini wanasema juhudi zaidi zinahitajika.

  Lakini kubwa zaidi walizungumza sana kuhusu kuporomoka kwa maadili na dalili za kusambaratisha umoja wetu. Sasa haya ni mambo ya msingi na kama nilivyosema Rais mwenyewe alikwishayatambua.

  Hatuoni ni kosa gani ambalo tumefanya kwa kuzungumza haya mambo. Jana (Desemba 6, 2009), nilikuwa kanisani kwetu (St. Alban, Anglikana - Dar es Salaam) kulikuwa na kumbukumbu ya miaka 75, mgeni rasmi ilikuwa awe Waziri Mkuu lakini kwa bahati mbaya akawa amesafiri kwenda Vienna kwa hiyo akamtuma Waziri Marmo (Philip Marmo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Bunge) kusoma hotuba yake, ilikuwa ni hotuba ya Waziri Mkuu iliyosomwa na Waziri Marmo.

  Na sehemu ya hotuba hiyo inasema ifuatavyo; “Kama nilivyoeleza Tanzania ina watu wapatao milioni 40. Watu hawa wana viwango tofauti vya mapato na hili linaeleweka. Hatuwezi kuwa na mapato sawa.

  “Tatizo linakuja pale ambapo tofauti ya kipato inapokuwa kubwa miongoni mwa makundi katika jamii. Lakini tatizo hili linazidi kuwa kubwa pale ambapo tofauti ya kipato inapokuwa kubwa miongoni mwa makundi katika jamii.

  “Lakini tatizo hili linazidi kuwa kubwa pale ambapo ukubwa wa tofauti hiyo unapoongezeka. Madhara ya ongezeko hilo mnayafahamu kwani kuna hatari ya matajiri wachache kuendesha maisha ya masikini walio wengi kwa njia ambayo itazidi kuwaongezea utajiri huku ikiwadidimiza zaidi masikini.

  “Si ajabu matajiri hao wachache wakawa ndio wanaoendesha vyama vya siasa, Serikali, Mahakama, Bunge, Makanisa, Misikiti n.k. Katika hali hiyo Taifa halina usalama.

  “Hivyo hatuna budi kuwa na misingi inayopunguza tofauti kati ya masikini na tajiri. Kama serikali tunazo njia mbalimbali tunazotumia kupunguza tofauti hiyo. Lakini ninaamini madhehebu ya dini nayo yana jukumu la kufanya.

  “Licha ya kuchukua tahadhari yasiendeshwe kwa matakwa ya matajiri hao, yana jukumu la kuona na kuhakikisha kuwa vyanzo vyanzo vya utajiri wa waumini wao ni vya haki na havitokani na mapato haramu au kuvunja amri za Mungu.

  “Hivyo, ningependa kuwaomba viongozi wa dini kushirikiana na mihimili yote ya dola ili kupunguza kuongezeka kwa tofauti ya kipato kati ya matajiri na masikini kwa kuwa mwisho wake si mwema,” anahitimisha kunukuu hotuba ya Waziri Mkuu na kuendelea kusema;

  Sasa haya maneno sasa haya maneno ya Waziri Mkuu hayana tofauti kabisa na yale yaliyozungumzwa katika kongamano. Tulichoona hapa ni kwamba Serikali kama Serikali inasikiliza ushauri. Rais amewahi kuyasema na Waziri Mkuu anayasema.

  Na kongamano lilikuwa linaishauri Serikali, kama Serikali haina tatizo na hayo yaliyosema huko mheshimiwa Makamba ana matatizo gani mpaka atutukane kwamba sisi ni wehu na wahuni.

  Uongozi ni kuonyesha njia, mheshimiwa Makamba ni kiongozi wa ngazi ya juu katika chama, ndiye mtendaji mkuu na ukiwa kiongozi mwenye madaraka lazima uchunge lugha yako.

  Lakini tumeona kwa muda mrefu mheshimiwa Makamba lugha yake ya kawaida ni kukebehi, kubeza na kutukana. Sasa anatoa dira gani kwa viongozi wengine na wananchi kwa ujumla.

  Kwa sababu wananchi na viongozi wengine watafuata mwelekeo wa viongozi wakubwa sasa kama kiongozi wetu wa chama lugha yake ni hiyo, wengine watafuata.

  Na ndiyo sababu unaona siku hizi kebehi, kubeza, matusi kati ya viongozi imekuwa ni jambo la kawaida, viongozi wanatukanana. Katika maneno yake aliyosema hakugusia hoja za msingi na ndiyo inavyokuwa wakati wote tukisema, hawagusi hoja.

  Kongamano limesema; maadili yameporomoka, Makamba anatukana bila kusema kama maadili yameporomoka au hayakuporomoka vivyo hivyo kuhusu hatari tunaziona zinazohatarisha umoja wetu kama ubaguzi huu wa kimatabaka, ubaguzi wa kikabila, ubaguzi wa kidini, ubaguzi wa kimtandao.

  Haya ndiyo tunayosema, atuambie je, ni nini ambacho tunasema hapa ni kibaya kwa Serikali yetu. Sisi haya mawazo ama ushauri tunautoa mara nyingi tu kwa wanaohusika, tunazungumza kwa mawaziri mara nyingi tu, tunatoa hoja nao wanatoa hoja.

  Baadhi ya nyakati wanaona hoja zetu na baadhi ya wakati tunaona hoja zao, ndiyo njia ya kushauriana katika uongozi, lakini wakati wote tunaheshimiana.

  Mawaziri wengi wanatuheshimu sana, tena sana, hata pale ambapo tunatofautiana mawazo heshima ipo. Hawatutukani, hawatukeji, hawatubezi. Na hiyo ni pamoja na Rais.

  Rais pamoja na cheo chake anaheshimu sana watu. Anatuheshimu sana sisi wazee. Hatutukani. Hatubezi, hata pale ambapo tunatofautiana mawazo, Rais anatuheshimu sana, nasi tunamheshimu.

  Na viongozi wengi wa chama ni vivyo hivyo. Katika kongamano lile kulikuwa na viongozi wengi wa ngazi za juu katika CCM. Walikuwapo wajumbe wa Halmashauri Kuu.

  Ukiwachukua Dk. Salim mjumbe wa NEC, Frederick Sumaye, Abdulrahman Kinana, George Mkuchika wote ni wajumbe. Mkuchika amekaa siku ya mwisho tangu asubuhi hadi jioni amesikia na kuzungumza na wanakongamano kwa heshima kabisa.

  Hawa hawana matatizo na walikuwapo pale, hujawasikia wametoka wakatoa matamko. Anakuja mheshimiwa Makamba anaita waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wake mwenyewe alikuwapo kwenye kongamano lakini kwenye mazungumzo na waandishi wa habari hakuwapo. Huyu (Mkuchika) ndiye aliyekuwa anajua nini kimetokea kule.

  Angeshauriana naye angejua nini kimetokea kule, lakini inaonekana mheshimiwa Makamba yeye ana kundi lake ambalo lina lenga watu fulani fulani, wakisema chochote basi lile kundi linakuja kuwatukana.

  Ana vijana wake pale makao makuu na ana mmoja mikoani anaitwa Mgeja, Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Tumeona aliyosema na hata wakati ule ambapo nilisema nikashambuliwa na yeye alijiunga humo na safari hii naye ameingia tena humo.

  Safari hii anasema kama yale aliyosema mwanzo anasema hivi (anasoma gazeti lililomnukuu Mgeja); kauli ya Makamba inaungwa mkono na Mwenyekiti wa CCM, Hamis Mgeja ambaye ameiambia Mwananchi Jumapili kwamba wanaopiga kelele wanasukumwa na chuki binafsi tangu makundi yao yaliposhindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.

  Alieleza kuwa Dk. Harrison Mwakyembe alikuwa kundi la Mark Mwandosya, Anna Kilango alikuwa kundi la John Malecela, Christopher ole Sendeka alikuwa kundi la Sumaye na wamekuwa wakiendelea kuwapotosha Watanzania kwa makusudi.

  Alisema kuwa ni wazi kwamba Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, ambao hata sasa wakati Rais anaelekea kumaliza kipindi cha miaka mitano hawajawahi kuona wala kuzungumzia zuri hata moja la awamu ya nne, walikuwa upande wa Salim hivyo chuki yao inazidi kuwatafuna.

  Huyo ni Mgeja anasema anatufahamu…mimi simfahamu. Sikuwahi kufanya naye kazi, sijui anatufahamu vipi.

  Watu waliogombea mwaka 2005, Malecela, Sumaye, Mwandosya, Salim. Kwa hiyo wale wote anaofikiria kwamba waliwaunga mkono wagombea hao wakisema chochote ni ovyo kwake, wanasema tuna chuki na wivu.

  Hawa wakiongozwa na Mh. Makamba ndio wanaoleta mgawanyiko katika chama, wao ndio wanakundi. Akisema mtu ambaye hayuko kwenye kundi lao wala hawachunguzi waone kilichosemwa…hoja iliyotolewa hapana, ni kutukana.

  Rais Kikwete akisema nchi inakabiliwa na matatizo ya kuporomoka kwa maadili, ubaguzi, rushwa na ufisadi ni sawa. Salim na Warioba wakisema hayo hayo wanaitwa watu wenye chuki na wivu.

  Waziri Mkuu Pinda akisema kwamba tofauti ya kipato kati ya matabaka ni hatari kwa usalama wa taifa Makamba anaona ni sawa. Lakini maneno hayo hayo yakisemwa na Salim na Warioba wanaonekana ni wehu na wahuni.

  Maneno hayo hayo yamesemwa kwenye makongamano na semina nyingi, Bungeni na mahali pengine lakini Mh. Makamba hakuita waandishi wa habari. Lakini yaliposemwa kwenye kongamano la Taasisiya Mwalimu Nyerere ameita waandishi wa habari na kutukana.

  Mheshimiwa Makamba anasema Rais Kikwete ni zaidi ya CCM, Rais ni popular kwa wananchi sawa…lakini ukifika mahali Katibu Mkuu wa chama anasema mtu mmoja ni zaidi ya chama ujue ameshindwa kufanya kazi, kwa hiyo hadhi ya chama imeporomoka.

  Makamba sasa ndiye analeta mgawanyiko ndani ya chama, hawa wote anaowasema Rais hana matatizo nao, Rais alikwisha kuondokana na hili, anafanya kazi nao vizuri tu.

  Kwa sababu kama unasema wale waliowaunga mkono wagombea (2005) wana chuki maana yake unasema hawa waliogombea ndiyo wana chuki.

  Ukisema mimi nina chuki kwa sababu nilimuunga mkono Salim, maana yake Salim ana chuki. Rais hana chuki na watu hawa. Kuna watu ambao hawakumuunga mkono kwenye uchaguzi na anafanya nao kazi serikalini hata Mwandosya yuko serikalini.

  Rais ana wasaidizi wanaojitahidi, ukimwoma Makamu wake (Dk. Ali Mohamed Shein) anafanya kazi. Anazunguka nchi hii kujaribu kusaidia utekelezaji wa sera na anatoa maonyo mengi tu kwa mambo ambayo anaona hayako sawa.

  Ukimwona Waziri Mkuu (Pinda) anafanya kazi kwa uwezo wake kwa commitment kubwa kabisa, na hawa wanasikiliza ushauri wanaopewa. Hawagombani na mtu, wanaheshimu watu, hawatukani watu.

  Makamba ameacha kufanya kazi ya chama ya kuimarisha chama, ya kuunganisha chama anajifanya yeye ndiye Waziri Mkuu wa nchi hii wa kumtetea Rais na kumtetea Rais ni kuwatukana watu, kuwabeza watu na kuwakejeli watu.

  Uongozi wa chama umevurugika, viongozi wanalaumiana, wanatukanana na huyu ndiye mtendaji mkuu wa chama badala ya kufanya jitihada za kuunganisha chama anaendelea na jitihada za kugawanya chama. Hafanyi kazi ya chama, anafanya kazi ya kundi, anaeneza chuki. Yeye na wenzake ndio wanaajenda ya chuki ambayo ni hatari sana kwa usalama wa CCM na nchi.

  Kwa hiyo, kama nilivyosema, tumesikia matusi yake akae huko akifikiri sisi ni wehu na wahuni. Haitunyimi usingizi. Nchi hii ni yetu sote, tuna wajibu wa kutoa maoni yetu, kutoa ushauri wetu bila woga wowote na hayo matusi yake hayatatuzuia kuendelea kutoa ushauri wa ndani au wa hadharani. Tutaendelea kwa sababu tunaitakia nchi hii mema.

  Yakitokea madhara tutahusika, sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Tunakata Tanzania ibaki nchi ya umoja, amani, utulivu na mshikamano. Tukiona kitu chochote kinahatarisha hayo, tutasema.

  Swali: Kuhusu suala la kundi. Rais alikuwa na kundi lake aliposhinda akalivunja na makundi mengine yametangazwa kuvunjwa, unazungumzia kundi gani?
  Jibu: Mimi sijui, ninachosema Rais hana kundi sasa kwa jinsi tunavyomuona. Hana kundi. Kuna mmoja aliniletea ujumbe hapa na kuna wenzangu wamepata ujumbe wa aina hiyo.

  Wanasema hivi mnafikiri Makamba anasema hivi bila baraka (za Rais) za viongozi wake? Kumbe Mimi nasema viongozi wake hawahusiki na haya anayosema (matusi) ni yake kwa sababu Rais tunamwelewa.

  Tunamjua, tumekuwa naye pamoja. Tunajua heshima anayotupa, hatukani, tunamwelewa Rais aliacha yale makundi, kundi lake. Ukiona katika chama na Serikali amewachukua watu ambao hawakuwa katika kundi lake, anao anafanya kazi nao vizuri.

  Ukianza na makao makuu ya chama pale, viongozi wa ngazi za juu si wote waliomuunga mkono wakati wa uchaguzi. Ukiingia serikalini ni hivyo hivyo, kwa hiyo sisi tunaamini hii Makamba anatumia jina la Rais kwa madhumuni yake mwenyewe, sasa hatujui anayemtumikia ni nani.

  Unaona anakumbatia na kutetea sana matajiri, lakini umeona Waziri Mkuu alivyosema ni tofauti kabisa.

  Swali: Ni ushauri wake kuhusu uongozi wa chama chenu?

  Jibu: Kama ninavyosema na kama ilivyokuwa kwenye kongamano, hatutaki kuzungumzia watu, tunazungumzia hoja. Kwenye kongamano tumesema maadili yameporomoka, umoja wetu unahatarishwa na ubaguzi. Haya tumeyasema na tumemwambia Rais aelewe hali hii achukue maamuzi magumu, au serikali kwa ujumla ichukue maamuzi magumu tusiingie hatarini.

  Maana yake nini? Maana yake tunamwambia Rais hali iko hivi inahitajika maamuzi magumu, lakini kwa kusema hivyo tunamwambia ukifanya uamuzi unaungwa mkono, sisi tunamuunga mkono ajue wananchi wanamuunga mkono.

  Kwa hiyo aone hatua zozote anazoweza kuchukua ili turekebishe hali hiyo. Ni kweli tunataka kumsaidia Rais na moja ya namna ya kumsaidia ni kumuonyesha concern kwamba kuna mambo haya yanahitaji uamuzi, sasa ukiyafanya tunakuunga mkono.

  Swali:Kuna hoja kwamba, wakati wenu mkiwa uongozini mlifanya nini?

  Jibu: Wakati wowote ule katika nchi yoyote ile, katika jitihada za kuleta maendeleo kutakuwa na mafanikio na matatizo. Nilimsikia mheshimiwa Makamba akisema kwamba matatizo ya sasa yanayoikabili awamu ya nne chanzo chake ni awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

  Maana yake anasema zile awamu hazikufanya vizuri, ni mawazo yake sigombani kama ana mawazo yake. Lakini mafanikio tunayojivunia yameletwa na nani?

  Tunaposema nchi hii ni ya umoja wa kitaifa yenye amani, utulivu mshikamano nani alileta hayo? Tunaposema maadili yameporomoka maana yake tulikuwa na maadili mazuri, nani aliyaleta hayo?

  Hakuna anayebisha kwamba kwenye hizo awamu za kwanza mwanzo kuna makosa yalifanywa lakini pia kuna mafanikio makubwa yaliyoletwa hiyo ni kawaida katika maendeleo ya nchi.

  Kama mheshimiwa Makamba anataka kutuambia kwamba awamu ya sasa ni mazuri tu hakuna makosa yanayotokea na kama yapo yametokana na hao walioongoza mwanzoni, basi.

  Maana hawa wa mwanzoni kwa kuwa wametoka lakini naye alikuwapo kuanzia awamu ya kwanza mpaka sasa. Yeye anaweza kusema kila alipokaa hakukutokea matatizo na kama yalitokea ilikuwa mwiko kuyazungumzia? Anapenda sana sifa. Makamba alikuwa anawasifu sana viongozi waliopita. Sasa anawalaumu. Hivi Makamba anamsifu kiongozi toka moyoni kwake au ni kutekeleza agenda binafsi. Kumsaidia kiongozi wako siyo lazima kumsifu wakati wote bali pia kutoa ushauri mgumu.

  Chanzo: Raia Mwema
   
 2. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  HAJATULIA, naona anahitaji apepewe ana mapepe
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Makamba hajatulia na WaTZ tushajua hilo. Makamba mara nyingine hajui hata asemalo.
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Makamba shida ni shule na historia yake tangu akiwa jeshini.

  Uliza Jeshini Makamba alipataje cheo cha ukapteni.

  Alikuwa bingwa wa kupeleka maneno NGOME/makao makuu ya Jeshi Upanga.

  Akiwachongea wenzake maneno haya na yale, ilimsaidia kupanda ngazi hadi ukapteni akionekana muadilifu.


  Sasa bado ananufaika na blahblah hadi leo, anakula kuku kwa vinenovineno, hatumtarajii kuacha ktk umri huo,

  Elimu yake inamfanya apwaye sana kujibu hoja kwa hoja, kweli makamba anaweza kusimama na kina Butiku ktk kujenga hoja ? anaweza kusimama na Warioba ama Salim A, Salimu, hawezi ni mwepesi hajai wala hadhi ya kusimama kisiasa mbele ya watu hao hana, huyu ni sawa na ma-messenger wengine pale makao makuu ya chama kielimu, amini nakuambia.
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Makamba ndiyo CORE Problem ya Makundi katika CCM..... Ni Mzigo kwa Chama Chake.
   
 6. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Swala la elimu tunalitambua sana kwamba ni problem kwake....

  Hazimtoshi upstairs...wote tunajua, kwanza ni nature yake...

  kwa kujikomba tu duh balaa mpaka anauzalilisha umri wake, chama chake, hata familia

  yake, ndo mana kwangu inakua ngumu kuamini kuwa mtoto wake atakua na maadili

  ikiwa mzazi wake tu anabihave kiivyo. ukizingatia kwamba mtoto wa kiume huchukua

  tabia kwa babaye na wakike kwa mamaye....thx for the report INVISIBLE....
   
 7. 911

  911 Platinum Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Lakini ni nani aliyemteua Makamba kuwa katika nafasi aliyopo sasa?Je ni muda gani umepita tangu ashike madaraka hayo??Mteuzi wake anaridhishwa na perfomance yake???Muda mwingine tunakuwa tunazunguka tu mbuyu...We all know exactly where the buck stops.Au hatujui?
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani kina Butiku wakipiga kelele kwamba bwana mkubwa amepwaya unadhani wanamuonea, JK katuletea uteuzi wa hovyo zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya taifa hili anzia kwenye chama ishia serikalini , marafiki na washikaji na balance zake anazodai za gender zinatoa tafsiri tata sana.

  Anzia chamani KATIBU MKUU MAKAMBA
  MKUU WA PROPAGANDA TABWE HIZZA
  hao watamshauri nini kisiasa.
  njoo mawaziri Juma kapuya.
  Makongoro Mahanga
  Sofia Simba
  Karamagi
  Msabaha

  Sasa huo ni mfano wa uteuzi wa hovyo aliowahi kuufanya na ndio unao yumbisha nchi yake na hakika kama hatatilia maanani maoni ya kina Butiku na Warioba ataula wa chuya,.

  Njoo kwa majaji ni uvundo mtupu wazee wa IMMA Wakaula, njoo Ubunge wakuteuliwa ndio hao kina Kingunge, njoo Kwa mabalozi kina Adadi Rajab na wenzao, mambo ya ajabu ajabu kabisa.
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Makamba aliwahi kuja Tumaini Iringa kwenye convocation ya mwaka 2007. Akasema kitu kimoja kizuri..... " Mtu yeyote anayetaka heshima kwa nguvu, hununua dharau kwa bei rahisi"
   
 10. M

  Mchili JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Rubish in rubish out. Sio makamba peke yake, wateule wengi wa mkulu wana walakini. Standard zake ziko chini sana.
   
 11. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa alikua na nyodo pale makao makuu ile mbaya.... Kazi yake ilikuwa mademu tu, sitaki hata kujua aliko.
   
 12. E

  Ex-Fisadi Member

  #12
  Dec 10, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa na sofia simba alikuwa receiptionist pale idara ya maelezo. Kwa kweli Kikwete ana kazi kwelikweli!!!!
   
 13. GY

  GY JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Viongozi walikuwa zamani bwana. Huyu Warioba alikuwa waziri mkuu siku nyingi sana na siasa ya nchi hii anaijua. Kiongozi hata kama ulishindwa kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi kwa sababu mbalimbali, tutakusifu na kukukumbuka hata kwa uadilifu wako tu.

  Amechambua vizuri sana, kwa uangalifu, utaratibu, hekima, heshima na busara. Hakukurupuka.

  Masuala yanayosemwa sana hivi sasa ni ya nchi, ni ya kitaifa. Kwanini yajibiwe na chama?????

  Kwanini ufisadi ujibiwe na chama na sio serikali? kwanini ukosefu wa maadili ujibiwe na chama. Kwanini upungufu wa uongozi na uwezo wa kuongoza ujibiwe na chama? kwanini chama kinateka masuala ya kitaifa? ivi nchi hii ingetokea ikaongozwa na raisi aliyeingia madarakani kama mgombea binafsi, nani atajibu tuhuma hizi. Katibu mkuu gani atajibu ufisadi.

  Hatusemi mwanachama fulani wa CCM au mwanamtandao fulani ni fisadi au ni kiongozi dhaifu, tunasema fulani hawezi au hatufai, au kuna tatizo la mmomonyoko wa maadili, kwanini chama kinabeba mambo haya?

  Safi sana mzee warioba, Makamba si waziri mkuu. Yaliyo ya nchi yaachwe yatatuliwe na waliopewa dhamana, ambao ni serikali. Ya kwao ya chama wayamalize kichama. Ufisadi na kuvunjika kwa maadili ya kitaifa pamoja na uwezo mdogo wa viongozi wetu si ya chama, ni yetu wote kama taifa, yajibiwe au yatafutiwe suluhu na waliopewa dhamana
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..inasikitisha, lakini nadhani Mzee Warioba kama siyo muoga, basi atakuwa in denial.

  ..Raisi tuliyemchagua hana uwezo wa kuongoza.

  ..Mateo Qares na Joseph Butiku wameeleza ukweli bila kumung'unya.

  ..Salim na Warioba walikuwa wakijaribu kumzuia Butiku asitoe madukuduku yake ktk kongamano la MNF.
   
 15. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu hapo juu shikamoni sana. Hawa akina Makamba ni JK ndio aliwateua na anawalinda.

  Maropes alinusurika kung'olewa na NEC Vasco DaGama akamwokoa sasa tutawatofautishaje?

  Warioba naye uoga tu unamsumbua sijui anaogopa kufutiwa pensheni yake. Anachanganya sana anaposema Rais anawaelewa wakati Rais huyo huyo wakati anatua nchini ametamka kuwa watu wana chuki binafsi kwa sababu aliwashinda 2005, Pia amesema atawajibu. Atatuambiaje kuwa anawaelewa?

  Naanza kuhisi kuwa ana madoa yake naye na kivuli chake kinamfuata japo aliyosema yana mantiki.
   
 16. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Makamba tunamjua ana matatizo sana lakini je hao wanao mnyooshea kidole makamba (warioba na Butiku) ni wasafi.

  Juzi tu warioba alikuwa kwenye kashfa ya Mwananchi Gold, Butiku mpaka leo hajatueleza anatumia vipi pesa pale Nyerere Foundation.

  Kulikuwa na bahati nasibu ambayo bwana Mustafa Jaffer Sabodo alijitolea kutoa zawadi za bahati Nasibu na pesa zikakusanywa na kwenda nyerere foundation ili wajenge jengo pale karibu na IFM, Cha ajabu pesa hazijulikani zimekwenda wapi na sasa kiwanja wametoa kwa investor wa Kichina.
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  Makamba asipojiuzulu basi karogwa au ana ugonjwa wa uduvi!
   
 18. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Wa kulaumiwa sio Makamba bali ni aliyemteua,naamini kama unamtaka mtu akusaidie kufanya kazi unakuwa tayari umeshampima uwezo wake na unampa kazi,sasa mwenyekigoda alipoangalia akaona mgosi wa ndima anafaa kwa kifupi kifupi mlitegemea upandwe mndimu uote mchungwa?

  Na kwa kuteua viongozi wabovu ina maana hata mkulu uwezo wake unakuwa na uwalakini elimu ya shule za bush na tapa haiwezi kupambanua mambo katika ulimwengu wa sasa
   
 19. M

  Mkuu Senior Member

  #19
  Dec 10, 2009
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kuna mtu hajatulia ni huyo mkuu mwenyewe ambaye anaetuletea huo uoza mashemeji na marafiki na wacheza bao pamoja

  tatizo la kulipa fazila ndio hilo na kupenda ujiko kwa raisi wetu
   
 20. l

  lukule2009 Senior Member

  #20
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani Jamani ndugu zangu tusizunguke mbuyu.. naomba kuuliza hii interview Warioba alifanya kabla au baada ya JK kurudi toka Cuba?

  Kusema Rais hataki makundi Mhesimiwa Warioba ni kutokuona ukweli .. JK mwenyewe amewaambia waandishi kuwa hashangai hayo mliyosema na kwamba mna wivu na akasema kuwa angeshangaa kama mngemsema vizuri .. sasa kwa nini mnazunguka kumlaumu Makamba? Ananbaraka zote za bosi wake

  ...msijidanganye kuwa anaongea bila baraka za Raisi.. mwambieni Rais ukweli wewe JK unagawa chama sio kumrembaaaa wakati ni wazi kabisa hata yeye mwenyewe anamsupport Makamba by the way ndio mana hamtoi hapo kwenye post ya Ukatibu. Mengi nafikiri ameshaelewa hili ndio mana siku hizi yuko kimya

  ...it is clear JK yuko upande wa mafisadi tusizungushane jamani.. asingekuwa huko angekuwa amechukua hatua..MWAMBIENI UKWELI JK SIO KUREMBA .

  Hata wapiganaji nadhani sasa wameelewa kuwa rais hayuko nao .. na by the way aliwahi kusema Diamond pale kuwa .. kusemasema bungeni hakusaidii sana sana mnachafuana tu .. JK mwenyewe alisema .. sasa kwa nini msimwambie ukweli tu .. oooh Rais ni mtu mzuri.. aahahahahah wapi anawang'ang'a tu
   
Loading...